Cardi B, Offset wabwagana

wabwagana rasmi

Mtanzania - - Leo Ndani - NEW YORK, MAREKANI

RAPA Cardi B, usiku wa kuamkia jana aligusa vichwa mbalimbali vya habari baada ya kutumia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa yeye na mume wake hakuna la ziada kila mtu na yake.

Wawili hao waliweka wazi uhusiano wao katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike ambaye anajulikana kwa jina la Kulture, akiwa na umri wa miezi sita.

“Kwa sasa ninatakiwa kupambana mwenyewe juu ya mtoto wangu, kati yetu hakuna ambaye alikuwa na kosa, nadhani kila mmoja wetu hakuna ambaye amekulia katika maisha ya upendo, hivyo kwa sasa kila mmoja na mambo yake.

“Sitaweza kumchukia Offset na nitaendelea kumpenda kwa kuwa ni baba wa mwanangu, lakini ukweli ni kwamba kuna mambo tumeshindwana kati yetu,” alisema Cardi B.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.