Aliyebaka mtoto afungwa jela miaka 30

Mtanzania - - Leo Ndani - NA MURUGWA THOMAS - TABORA

PATRICK Kabula (24) mkazi wa Chemchem Manispaa ya Tabora, aliyetishia kumuua mtoto wa miaka mitano baada ya kumbaka, amehukumiwa kwenda jela miaka 30.

Adhabu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Jocktan Rushwela baada ya kumtia hatiani mtuhumiwa.

Hakimu alisema hilo ni fundisho kwa watu wengine wenye tabia za ukatili kwa watoto.

Katika kesi hiyo, mahakama iliridhika na ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa Jamhuri ulioambatana na vielelezo vinne ikiwamo nguo ya ndani ya mtoto aliyebakwa ikiwa na damu.

Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamiziwa wa Serikali, Idd Mgeni uliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa sababu vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike vimekithiri mkoani humo.

Katika shauri hilo, ilidaiwa na Jamhuri kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo February 12 mwaka huu kinyume na kifungu 130 (1) na(2)e na kifungu

131 (3) cha kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Ilidaiwa siku hiyo mchana eneo la Mwinyi, mshitakiwa akiwa nyumbani kwake, alimwingilia mwili mtoto huyo jina (tunalo) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri. Ilielezwa na mashahidi kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimwita mtoto huyo na alimvutia nyuma ya nyumba na kumwingilia mwili huku akimtishia asimwambie mtu kwamba angemuua.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.