MCHUZI WA MAYAI

Mtanzania - - Jamil Na Afya -

MAHITAJI

Mayai yaliyochemshwa 6 Mafuta vijiko vya chakula 5 Vitunguu maji vilivyokatwa 2 Nyanya zilokatwa 3 Pilipili za kijani 2 Kitunguu saumu kilichopondwa vijiko vya chai 2

Tangawizi iliyopondwa vijiko vya chai 2

Giligilani ya unga vijiko vya chai 2

Binzari nyembamba ya unga kijiko cha chai 1

Garam masala kijiko cha chai 1 Manjano kijiko cha chai 1/2 Pilipili ya unga kijiko cha chai 1/2 Chumvi kiasi Kotmiri kwa ajili ya kupambia JINSI YA KUANDAA Weka mafuta vijiko vya chakula viwili kwenye sufuria, yakipata moto weka vitunguu.

Kaanga hadi vianze kuwa vya kahawia, baada ya hapo zima moto.

Ipua vitunguu na weka kwenye blenda usage na nyanya na pilipili za kijani.

Usiongeze maji wakati wa kusaga kama itawezekana, ongezea mafuta yaliyobaki kwenye sufuria uliyokaangia vitunguu, yakipata moto weka mchanganyiko wa nyanya na ukaange kwa dakika mbili hadi tatu.

Weka tangawizi na kitunguu saumu na masala zote kaanga hadi uone mafuta yanaanza kujitenga

Weka maji ya uvuguvugu vikombe viwili na acha ichemke kwa moto wa kati.

Kata mayai yaliyochemshwa kati kati na uweke kwenye mchuzi.

Ivisha mchuzi kwa dakika 10 au hadi uwe mzito.

Ipua na mwagia kotmiri kwa juu.

Unaweza kula kwa wali au chapatti.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.