Nyota Over Night kutikisa Mbeya kesho

Mtanzania - - Burudani - NA CHRISTOPHER MSEKENA

KUELEKEA tamasha la Nyota Over Night litakalofanyika kesho katika kanisa la EAGT lililopo uwanja wa ndege wa zamani mkoani Mbeya, tayari waimbaji mbalimbali wa Gospo wamewasili jijini humo kukonga nyoyo za mashabiki.

Akizungumza na MTANZANIA jana mratibu wa tamasha hilo, Bahati Simwiche, alisema lengo la Nyota Over Night litajumuisha wachekeshaji na waimbaji wa Gospo watakaotumbuiza kwa mtindo wa ‘playback’ na ‘live band’. “Tamasha litaanza saa 2 usiku na kuendelea kutakuwa na matukio mengi ya kusifu, kuabudu na kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai kwa mwaka mzima huu, waimbaji kama Happy Kamili, Ikupa Mwambenja, Beatrice Swai, Maria Msalilwa, Mnene Makweta, Julius Mgondoy, Mc Joshua, Martin Gwakisa na wengine wengi watahudumu,” alisema Bahati.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.