Dondoo

Mtanzania - - Burudani -

Chelsea

KIUNGO wa Chelsea, Cesc Fabregas, yupo kwenye mipango ya kuondoka katika kikosi hicho wakati wa Januari mwakani, kutokana na hali hiyo klabu ya Valencia ipo mbioni kuwania saini ya mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona.

AC Milan

NYOTA wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya AC Milan kwa mkopo, anaweza kuonekana moja kwa moja akiwa na uzi wa AC Milan kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya kutaka kumpa mkataba wa kudumu.

Nice

KOCHA wa timu ya Nice, Patrick Vieira, ameweka wazi kuwa yupo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kutaka kumwacha mshambuliaji wao, Mario Balotelli, akiondoka wakati wa Januari mwakani. Wakati wa kiangazi mchezaji huyo alitangaza kuondoka, lakini wakamzuia na sasa ametangaza kutaka kuondoka.

Chelsea

KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Denis Suarez, ameingia kwenye rada za klabu ya Chelsea katika orodha ya wachezaji wanaowindwa wakati wa Januari mwakani, lakini Chelsea itakutana na ushindani kutoka kwa AC Milan ambao wanawania saini ya mchezaji huyo.

Everton

UONGOZI wa klabu ya Everton, unaamini mchezaji wa Barcelona, Andre Gomes, ambaye anakipiga katika klabu yao kwa mkopo, anataka kuitumikia moja kwa moja klabu hiyo. Mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho.

West Ham

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Nantes, Emiliano Sala, ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na klabu mbalimbali barani Ulaya, miongoni mwa klabu hizo ni pamoja na Fulham, Crystal Palace na West Ham.

Guangzhou

KLABU ya Guangzhou Evergrande, ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini China, imeweka wazi kuwa imetenga kiasi cha pauni milioni 13 kwa ajili ya kuwania saini ya nyota wa klabu ya Lille, Thiago Mendes. Hata hivyo, PSG na Monaco wanawania saini ya mchezaji huyo.

Chelsea

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Maurizio Sarri, ameweka wazi kuwa, uongozi wa timu hiyo umekuwa ukipambana kila wiki kuhakikisha mchezaji wao, Eden Hazard, anaongeza mkataba mpya, lakini kuna ugumu kutokana na Real Madrid kuonesha nia.

Real Madrid

NYOTA wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Matteo Kovacic, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Chelsea kwa mkopo, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurudi Madrid kwa siku za hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.