anachokonoa kutaka kuchokonolewa ili achokonoe zaidi?

Mtanzania - - Jichopevu - Na EVANS MAGEGE

Hivyo kwangu nachukulia hayo yote kama mtu kaamua NXWRD PDRQL QD NXHOH]D ÀNUD ]DNH MDPER OD SLOL LEDUD \D \D .DWLED LQDHOH]HD ZDMLEX ZD NLOD PWX NXIXDWD QD NXWLL .DWLED \D QFKL VDVD QLOLGKDQL PWX NDPD 6SLND DOLSDVZD NXZD PIDQR ERUD NDWLND NXKDNLNLVKD NXZD LEDUD \D LQD\RQLWDPEXD PLPL QD WDDVLVL QLQD\RLRQJR]D LQDKHVKLPLZD NDPD LQDY\RVWDKLNL

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amechokonoa moja ya mihimili mitatu inayounda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siamini kama ni tabia yake ya uchokonozi, lakini kama ni hivyo, labda ni tabia mpya, pia sijua kama anaifanya kwa hamu tu au kujifurahisha ili naye achokonolewe zaidi kwa kusudio la kuendelea kuchokonoa mambo mengine yaliyomo ndani ya mihimili mitatu ya Serikali.

Haihitaji kwenda mbali sana katika tafakuri kwa sababu inawezekana msukumo wake wa uchokonozi umetokana na ‘nyongo’ iliyomjaa tumboni.

Labda analazimisha kuweka kidole kinywani aguse koo ili aitapike na kupata ahuweni kwa afya yake.

Hii ni tafsiri yangu ambayo huwa napenda kuipambanua kwa mtindo huu; CAG ni Profesa Assad na Profesa Assad ni CAG. Vivyo hivyo hata Spika wa Bunge ni Job Ndugai na Job Ndugai ni Bunge.

Nasema hivyo kwa nini? Naanza na Profesa Assad, miaka mitano na miezi takribani miwili tangu kuteuliwa kwake kuwa CAG kafanya mambo mengi, kafanana na majukumu yake, pia kiti chake cha uongozi.

Naweza kusema kwamba muda wote huo kapata uzoefu mkubwa katika nafasi yake, hata sisi wanajamii tumezoea kumuona kwenye nafasi yake.

Tumezoea kumwona katika kujiamini kwake, kujipambanua kwake na pia ni vigumu leo hii kumtenganisha Profesa Assad na jina la CAG, ndiyo maana hapo awali nimesema CAG ni Profesa Assad na Profesa Assad ni CAG.

Kwa upande wake Ndugai, yeye ndiye Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano, ndiye kiongozi wa mhimili huo wa Serikali.

Leo hii tunamtaja Ndugai tukiwa na maana pana ya uongozi wa bunge, si uongozi tu, bali bunge kwa ujumla kwa maana akitoacho kinywani mwake ndicho kinawakilisha sauti ya bunge.

Ndugai, mwenye haiba ya upole na unyenyekevu, ila mkali akiudhika, hivi karibuni ameibukia kwenye vyombo vya habari kujibu mapigo ya uchokonozi wa CAG alioutoa huko ughaibuni.

Ni uchokonozi gani huo? Kauli ya kulitaja bunge kuwa ni ‘dhaifu’ ndio iliyosababisha tafsiri tofauti kwa jamii, huku Spika akiona kuwa imejengwa katika misingi ya kudharau mhimili huo wa Serikali ambao anauongoza.

CAG aliitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mwandishi Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN), ambaye alimuuliza kuwa ofisi yake inafaya kazi vizuri na kutoa ripoti kila mwaka ambazo nyingine zinaonyesha ubadhirifu wa fedha, lakini haionekani kama kuna jambo kubwa linachukuliwa baada ya ripoti hizo kuwasilishwa bungeni.

Akijibu swali hilo, CAG alisema suala hilo kimsingi ni kazi ya bunge; “Kama tunatoa ripoti inaonyesha ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu wa bunge, bunge linatakiwa lisimamie na lihakikishe kwamba pale penye matatizo basi hatua zinachukuliwa.

“Sasa sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini ni jambo ambalo tunaamini muda si mrefu litarekebishika, lakini jambo kubwa tunahisi bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa,” alisema Profesa Assad.

Kwa nini Ndugai ameamua kujibu mapigo ya uchokonozi wa CAG? Jibu ni rahisi, Ndugai kaibuka kutetea mhimili anaouongoza kwa sababu hata mjadala uliofuatia baada ya kauli hiyo CAG unaakisi kuunga mkono alichokisema CAG.

Maoni ya wafuatiliaji wa mambo, wakiwamo wanasiasa, hasa wale wa upinzani wanaonekana kuunga mkono kauli ya CAG .

Kwa muktadha huo, lugha nyingine naweza kusema kuwa Ndugai naye kaamua kumchokonoa CAG kwa kumtaka afike kwenye Kamati ya Maadili na Kinga ya Bunge Januari 21 kwa ajili ya kumhoji juu ya kauli yake hiyo ambayo inadhalilisha mhimili huo wa Serikali kwamba ilikuwa na maana gani.

Jambo la kushangaza zaidi au ndio kusema; “CAG anachokonoa kutaka kuchokonolewa ili achokonoe zaidi? Siku moja baada ya Spika kutoa mwongozo huo, mambo yaligeuka na kutoa tafsiri ya kwamba jambo hilo hilo limekuwa ni mvutano wa uchokonozi kati ya Ndugai Vs CAG.

Nasema hivyo kwa sababu baada ya Ndugai kutoa mwongozo huo, CAG naye akajibu mapigo kwa kusema hataki kuwa miongoni mwa wavunjao Katiba.

“Mmeuliza kama nitaitikia wito, sitajibu hili, ila niweke rekodi sawa, ule si wito bali ni amri. Sasa kwa kuheshimu Katiba yetu na kwa kuwa sitaki kuwa miongoni mwao waivunjao, niseme hivi, Ibara ya 18(a) inampa kila mtu uhuru wa kutoa maoni.

“Hivyo kwangu nachukulia hayo yote kama mtu kaamua kutoa maoni na kueleza fikra zake, jambo la pili ibara ya 26(1) ya Katiba inaelezea wajibu wa kila mtu kufuata na kutii Katiba ya nchi, sasa nilidhani mtu kama Spika alipaswa kuwa mfano bora katika kuhakikisha kuwa ibara ya 143 inayonitambua mimi na taasisi ninayoiongoza inaheshimiwa kama inavyostahiki.

“Niseme tu nitasimamia ninachokiamini kitaaluma na kizalendo kwa masilahi mapana ya Taifa letu,” alikaririwa CAG na vyombo vya habari. BUNGE ‘DHAIFU’ AU SI ‘DHAIFU’?

Kwa kuwa mjadala wa sakata hili kwenye mitandao ya kijamii umeonekana kuegemea upande mmoja. Yaani namaanisha maoni mengi yamejikita kumtetea CAG, binafsi nimeamua kutoka katika muktadha huo kwa kujielekeza kwenye maswali mengi ambayo najiuliza juu ya tafsiri ya kauli ya CAG.

Kauli ya CAG ya kudai kuwa bunge ni dhaifu ina maana gani? Je, alisema ukweli au si ukweli?

CAG alistahili kuzungumzia majukumu ya bunge angali anajua kuwa jukumu lake ni kuandaa ripoti, kuwasilisha bungeni na kulishauri bunge. Je, kauli yake imevuka mipaka ya kiutendaji?

CAG kabla ya kutoa kauli hiyo alifahamu maana ya uwajibikaji wa pamoja? Kama alifahamu je, amewahi kuzungumza na Spika na kumuelezea maoni yake juu ya utekelezaji wa ripoti na ushauri anaoutoa kwa bunge?

CAG kusema bunge ni dhaifu alimaanisha mjumuiko wa watu wote ndani ya mhimili huo kuanzia Spika, Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri, wabunge wa upinzani, wabunge wa chama tawala?

Je, anaona ushauri unaotolewa na ofisi yake juu ya masuala mbalimbali ya ukaguzi hufunikwa kama ule usemi wa “funika kombe mwanaharamu apite”?

Binafsi naona kabla ya kuingia katika mjadala wa Ndugai Vs CAG, kunahitajika majibu ya kujitosheleza juu ya maswali niliyouliza.

NA EVANS MAGEGE SIMU: 0718814926

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.