Tukiwa na juhudi tutafanikiwa: Said Abdallah

Mtanzania - - Toto - Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

WIKI inayomalizika leo shule nyingi za serikali na binafsi zimefunguliwa na wanafunzi kurejea shuleni. Totokona limezungumza na mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Kilole iliyopo Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Said Abdallah (11) pichani, ambaye anazungumzia malengo yake kwa mwaka huu.

Anasema amejiandaa vizuri kurejea shuleni na kuendelea na masomo yake ya darasa la nne.

“Wazazi wangu wameniandaa vizuri kuingia darasa la nne na kujiandaa na mitihani ya kufuzu kuingia darasa la tano,” anasema Said.

Anasema katika kipindi cha likizo alikitumia vizuri kwa kusa¿ri kwenda jijini Dar es Salaam kutembelea ndugu na jamaa, lakini kwa sasa amerudi kuendelea na masomo.

“Mwaka huu natamani kuongeza juhudi zaidi katika masomo ya sayansi ili yanisaidie kuwa mhandisi wa magari,” anasema Said.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.