Yanga, Azam wamwinda staa wa Malindi

Mtanzania - - Micheso - Na SAADA SALIM - DAR ES SALAAM

BAADA ya kuzisumbua Yanga na Azam FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji wa Malindi, Abdulswamad Kassim, amekuwa lulu kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwemo timu hizo.

Abdulswamad aliisumbua Yanga na Azam katika michuano hiyo hatua ya makundi na kuisaidia Malindi kutinga nusu fainali kabla ya kutolewa na Simba baada ya kuchapwa penalti 3-1 juzi Uwanja wa Amaan, Unguja.

Kabla ya timu hizo kupigiana penalti zilikamilisha dakika 90 kwa suluhu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, fowadi huyo alisema michuano imekuwa na faida kwake baada ya kupokea simu kutoka kwa viongozi wa Yanga na Azam.

Alisema amewaomba atafakari kwa kina kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho wa kumwaga wino ili kuzichezea msimu ujao wa Ligi Kuu.

“Ni kweli kuna timu zinanihitaji, lakini kipaumbele changu ni Azam nitaenda huko kama tutaafikiana kwani wana kila kitu ambacho mchezaji wa soka anahitaji.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.