Viongozi wa vyama vya michezo wanatakiwa kuwa wabunifu

Mtanzania - - Tahariri - Na JENNIFER ULLEMBO -DAR ES SALAAM -John Addison

TUNAPOZUNGUMZIA maendeleo ya michezo nchini, inamaanisha michezo yote, kuanzia soka na ile midogo midogo.

Tukiwa tumemaliza wiki chache tangu kupokelewa kwa mwaka mpya, tayari baadhi ya vyama vya michezo vimeanza kuomba msaada katika mashindano mbalimbali ambayo yatafanyika mwaka huu.

Ukweli upande wa maendeleo katika michezo mbadala na soka hapa nchini kwetu tupo nyuma sana, daima tumekuwa tukisubiri matokeo mabovu na kutoa lawama. Umefika wakati wa viongozi husika wa vyama vya michezo kujiwekea mikakati ya kusaka fedha, kuacha kutegemea udhamini.

Udhamini umekuwa ugonjwa sugu kwa kila chama cha michezo hapa nchini, jambo ambalo limekuwa likikwamisha mambo mengi ndani ya chama husika.

Tumeshuhudia vyama vikishindwa kuendesha mashindano, sababu kubwa ni kukosa wafadhili, pia timu kushindwa kuweka kambi, kujiandaa vya kutosha.

Ikiwa michezo mbadala inahitaji kupiga hatua na kuleta maendeleo, lazima viongozi wanaobeba dhamana ya kuongoza wajitume wenyewe binafsi.

Imekuwa jambo la kawaida kushuhudia viongozi wakibweteka na kujikuta wakitoa lawama kwa serikali pindi wanaposhindwa kufanikisha mashindano au kufanya ovyo.

Serikali imekuwa ikibebeshwa lawama kwa kushindwa kuzisaidia timu za vyama mbalimbali kushiriki mashindano ya kimataifa.

Lakini ukweli ni kuwa unatakiwa kujisaidia mwenyewe, ndipo utafute msaada kutoka kwingine, lakini hili viongozi wa vyama vya michezo hapa nchini hawalitambui.

Viongozi wa vyama vya michezo mnatia aibu, miaka mingi sasa mmefadhiliwa, lakini jambo la ajabu ni mnaposhindwa kujiongeza na kutafuta mbinu zenu wenyewe.

Michezo ni ajira na burudani, mtaendelea kushuhudia mataifa ya wenzetu wakipiga hatua na kusonga mbele, huku wakifanikiwa katika mashindano mbalimbali makubwa duniani. Mataifa mengine yamekuwa yakiwakilishwa na wachezaji lukuki pindi wanapopata nafasi ya kushiriki mashindano yoyote makubwa.

Upande wa Tanzania, timu zimekuwa zikiwakilishwa na wachezaji wachache, huku sababu kubwa ya kushindwa ikiwa ni kukosekana kwa fedha za usafiri na huduma nyingine.

Umefika wakati viongozi wa vyama kusimama, kutafuta vyanzo vya kujiingizia kipato kwa ajili ya timu husika, kuacha kutegemea misaada, ambayo mara kwa mara imekuwa ikishindwa kutimizwa na kupelekea timu kushindwa kutimiza malengo.

Kwa wasio na nambari za Tigo wawaombe ndugu au rafiki zao wenye Tigo wafanye usajili kwa kubonyeza nambari *149*20# na kisha kufuata maelekezo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.