Faini Sh 200,000

Mtanzania - - kanda Ya Ziwa -

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Mji Mdogo Igunga, Joseph Elias amesema kuanzia sasa abiria yeyote atakayebainika kutupa uchafu hovyo katika Kituo Kikuu cha Mabasi atakamatwa na kutozwa faini, ANARIPOTI ABDALLAH AMIRI.

Alikuwa akizungumza na wasafiri, wafanyabiashara na mawakala wa mabasi na magari madogo katika kituo hicho juzi.

Elias alisema kuanzia sasa abiria yeyote atakayeshindwa kuzingatia sheria hiyo atatozwa faini ya Sh 50,000 hadi Sh 200,000 papo kwa hapo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.