Safari ya Mgonahazeru kwenye muziki toka 1980-2019

Mtanzania - - TATA - Inatoka uk i Na VALERY KIYUNGU

WINGU zito la majozi lilitanda Januari 3, mwaka huu baada ya kusambaa kwa taarifa za kifo cha mwanamuziki nguli wa dansi nchini, Abdallah Mgonahazeru kilichotokea katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipolazwa kwenye wodi la Kibasila akipatiwa matibabu ya tezi dume.

Mgonahazeru aliyezaliwa 1964 na katika uhai wake kuwa kiongozi wa bendi, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji wa sauti ya kwanza na ya pili alizikwa Januari 4 mwaka kwake Kinore, mkoani Morogoro na mamia ya watu

AINGIA RASMI KWENYE MUZIKI

Mgonahazeru alianza kujishughulisha na muziki mwaka 1980, wakati huo akiwa na bendi ya Cuban Marimba iliyokuwa na makazi yake Morogoro Mjini, ikiwa chini ya umiliki wa marehemu Juma Kilaza.

Hata hivyo hakuweza kudumu kwa muda mrefu katika bendi hiyo, kwani mwaka 1983 alihamia Mzinga Troupes, akiwa kama mwimbaji chipukizi kundini hapo ambapo alifanya maonyesho kadhaa na bendi hiyo.

Kama kauli mbiu ya baadhi ya wanamuziki inayodai kuwa, kuhama bendi moja kwenda nyingine ni kusaka maisha bora zaidi, Mgonahazeru mwaka mmoja baadaye aliipa kisogo, Mzinga Troupe.

Mwaka 1985, mwanamuziki huyo alisafiri hadi Dar es Salaam na kujiunga katika bendi ya Chamwino Jazz, ambayo ilikuwa inamilikiwa na mwanamuziki John Luwanda, iliyokuwa na makazi yake katika ofisi za Chama cha Mapinduzi, Tandale.

Katika bendi hiyo Mgona alishiriki kuimba nyimbo nyingi kama vile Narudi Morogoro na Nitaoa Mke Gani, ambazo zilitungwa na John Luwanda na kuwa kivutio kwa wapenda dansi katika kumbi za burudani.

ATIMUKIA VIJANA JAZZ

Mwaka 1988, alijiunga na Vijana Jazz ambayo ilikuwa ikiongozwa na marehemu Hemedi Maneti na ujio wake uliiwezesha bendi hiyo kumudu vyema upinzani wa bendi nyingine kama vile Sikinde, Msondo Ngoma, na Oss wana Ndekule ambazo zilikuwa zikishindana wakati huo.

Ni kutokana juhudi za Mgonagazeru za kuimba, huku akicheza, kuliwezesha bendi ya Vijana Jazz kuzoa mashabiki wengi katika kumbi nyingi ukiwamo ule Vijana Hostel.

Mwaka mmoja baada ya kujiunga katika bendi ya Vijana Jazz, Mgonahazeru alitunga wimbo uliojulikana kama Ngapulila Namba 2, ambao ulikuwa ni mwendelezo wa kibao Ngapulila Namba 1 kilichotungwa na marehemu Adam Bakari maarufu kama Sauti ya Zege.

Baada ya wimbo huo mwanamuziki huyo ambaye pia alijulikana kwa jina la Mgona, alishiriki kuimba nyimbo nyingi za bendi hiyo, baadhi ya nyimbo hizo ni Mke Mkubwa ambao uliwagusa zaidi mashabiki wanawake.

WANAMUZIKI WALONGA

Wanamuziki Athumani Saburi na kiongozi msaidizi wa bendi ya Vijana Jazz kwa nyakati tofauti wameliambia MTANZANIA kuwa Mgonahazeru enzi za uhai wake alikuwa kipaji na uwezo wa kipekee katika muziki. Walisema kuwa uwepo wake kwenye bendi uliweza kuongeza idadi ya mashabiki wa bendi, hususan kwenye kumbi ambazo walikuwa wanatumbuiza.

Mwaka 1985, mwanamuziki huyo alisafiri hadi Dar es Salaam na kujiunga katika bendi ya Chamwino Jazz, ambayo ilikuwa inamilikiwa na mwanamuziki John Luwanda, iliyokuwa na makazi yake katika ofisi za Chama cha Mapinduzi, Tandale.

Mgonahazeru

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.