Watu 21 wafa mgodini China

Mtanzania - - Habari za Kimataifa -

WATU 21 wamekufa nchini hapa baada ya ya kufukiwa na kifusi cha mgodi wa mkaa wa mawe.

Kwa mujibu wa gazeti la People’s Daily, ajali hiyo ilitokea juzi katika Jimbo la Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa nchi hii.

Gazeti hilo liliripoti kuwa ajali hiyo ni kati ya nyingi ambazo ziliripotiwa kutokea ndani ya migodi ya makaa ya mawe mwaka jana kutokana na rekodi ya uduni wa usalama.

Taarifa za gazeti hilo zilieleza jana kuwa ajali hiyo ilitokea katika mgodi unaomilikiwa na Kampuni ya Baiji Mining Co Ltd’s Lijiagou yenye makao yake makuu mjini Shenmu wakati wachimbaji 87 wakiwa chini ya ardhi.

Liliripoti kwamba wachimbaji sita waliokolewa lakini wengine 21 walikwama chini ya mgodi huo na 19 ndiyo walikuwa wamethibitishwa kufariki dunia awali wakati jitihada za ukoaji zilipokuwa zikiendelea za kutafuta wengine wawili ambao walikuwa hawajulikani walipo, ingawa baadaye walikutwa wamekufa.

Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Usalama wa Migodini nchini imewaagiza wamiliki wa migodi katika majimbo ya Shandong na Henan, Kaskazini Mashariki mwa nchi, kusimamisha shughuli zao kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi agizo ambalo litadumu hadi Juni mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.