Kili Marathon yawakumbusha washiriki kujisajili mapema

Mtanzania - - Habari za michezo - Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WAANDAAJI wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon wamewakumbusha washiriki kujisajili mapema kwa njia ya mtandao, zikiwa zimebaki wiki nane kabla ya kufanyika mbio hizo Machi 3, mwaka huu, katika Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU).

Mkurugenzi wa mbio hizo, John Addison, amesema jana kuwa, washiriki wote wanapaswa kufuata utaratibu wa kujisajili kwa njia ya mtandao, kwani hakutakuwa na usajili katika vituo kama ilivyozoeleka miaka ya nyuma.

Alisema mbio zote zinazotambulika kimataifa hutumia mfumo huo ili kuwavuta washiriki wajisajili mapema kuepusha usumbufu dakika za mwisho.

Alisema usajili ulianza mwaka jana kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.kilimanjaromarathon. com kwa kupitia Top Events au kwa njia ya Tigo Pesa kwa kubonyeza *149*20# kwa kutumia namba ya tigo na ufuate maelekezo.

“Kwa ambao hawana nambari za Tigo wanaweza pia kuwaomba ndugu au rafiki zao wenye namba za Tigo kuwafanyia usajili kwa kubonyeza nambari *149*20# na kisha kufuata maelekezo,” alisema na kusisitiza kwamba usajili utathibitishwa kwa wale watakaofanya malipo.

Alisema kwa raia wa Tanzania na wakazi wa nchi za Afrika Mashariki, walitakiwa kulipa bei za kawaida ambazo ni Sh 20,000 kwa mbio za kilomita 42, Sh 20,000 kwa mbio za kilomita 21 na Sh 5,000 kwa kilomita 5, lakini kutokana na punguzo la bei kuanzia Oktoba hadi Desemba 14, 2018 ambapo walilipa Sh 15,000 kwa 42 km, Sh 12,000 kwa 21 km na Sh 5,000 kwa kilomita 5 na kuanzia Desemba 15 hadi Januari 7, bei hizo zilipanda kidogo kufikia Sh 18,000 kwa 42km, Sh 15,000 kwa 21km na Sh 5,000 kwa kilomita 5.

SARAKASI: Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pongwe Jijini Tanga wakionyesha umahiri wao wakati wa hafla ya makabidhiano ya saruji mifuko 50 na matofali 700 vilivyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga, Ummy Mwalimu, juzi kwa ajili ya kuongeza vyumba vya madarasa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.