Simba SC waliishika hapa JS Saoura

Mtanzania - - Mbele - Na GLORY MLAY

Na BADI MCHOMOLO - DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba juzi ilianza vizuri michuano ya Klabu Bingwa Afrika, baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura hatua ya makundi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba wameingia hatua hiyo ya makundi baada ya kuwaondoa wapinzani wao, Nkana FC, kwa jumla ya mabao 4-3. Mchezo wa kwanza Simba ilifungwa mabao 2-1 huko Zambia, huku marudiano Simba ikishinda 3-1 na kukata tiketi ya kuingia hatua ya makundi ambayo mchezo wao wa kwanza ulikuwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa.

Mipango ya Simba ni kuhakikisha inashinda michezo yao yote ya nyumbani dhidi ya wapinzani wao kwenye kundi D, ambalo lina wapinzani wake kama vile Al Ahly, Vita Club na hao JS Saoura.

Mipango yao imeanza kufanikiwa katika mchezo huo wa kwanza. Kilichowafanya waweze kufanikiwa ni pamoja na: Maandalizi Lengo kubwa la Simba na kocha wao, Patrick Aussems, ni kuhakikisha wanaweka historia kubwa kwenye michuano hiyo baada ya kutoshiriki kwa muda mrefu, kutokana na mipango hiyo waliamua kufanya maandalizi ya hali ya juu kwa kikosi chao chote kukipeleka Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo fainali zake zimefikia mwisho jana, huku Simba ikiingia fainali dhidi ya Azam FC.

Kombe la Mapinduzi ilikuwa ni sehemu sahihi kwa Simba kufanya maandalizi kutokana na muda walioupata, kikubwa walipeleka kikosi chote kwa ajili ya kutaka kutengeneza umoja kwa wachezaji ambao watawatumia kwenye mchezo huo wa jana.

UBORA WA KIUNGO

Hii ni sehemu mojawapo ambayo Simba wanajivunia kuwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu, kuanzia wale wanaocheza kwa ajili ya kulinda mabeki wao pamoja na wale ambao wanaongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.

Aina hizo mbili za wachezaji kila mmoja alitekeleza jukumu lake kama alivyopangiwa na vile inavyotakiwa kwa ajili ya kuhakikisha timu inafanya vizuri katika idara zote.

Tukianzia viungo wachezeshaji, Clatous Chama alikuwa kwenye ubora wake ambao Simba walikuwa wanautarajia kuuona akiufanya katika kuwachezesha washambuliaji John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi.

Hata hivyo, Chama alicheza kama kiungo anayetokea pembeni, lakini alikuwa mchezaji huru ambaye alionekana kila sehemu katika eneo la katikati, huku akipishana na Hassan Dilunga, lakini Chama alionekana kuwa na madhara zaidi kwa kuwa muda mwingi alikuwa anapambana kuhakikisha pasi zake zinawapita mabeki wa JS Saoura na kuwafikia washambuliaji.

Dakika 45 za kwanza pasi za Chama zilionekana kudhibitiwa na mabeki hao, lakini mipango ikawa mingi kwa Simba na hatimaye wakawa wanatumia mipira mirefu ambayo iliweza kuleta madhara.

Jonas Mkude bado amekuwa kwenye kiwango kilekile cha ubora wake katika safu ya kiungo, akihakikisha yeye na James Kotei wakiwalinda walinzi wao wasipate kazi kubwa ya kupambana na washambuliaji wa JS Saoura.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi kwamba Simba SC ilikuwa bora sana katika safu ya kiungo, ambapo walikuwa wachezaji wanne kwenye eneo hilo; Chama, Mkude, Kotei na Dilunga, kila mmoja alifanya kazi yake kwa ubora wa juu na hata pale walipofanya mabadiliko ya kuingia Mzamiru Yasini kuchukua nafasi ya Dilunga.

MECHI ya kwanza ya mahasimu Simba Queens dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Lite iliyochezwa jana Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ilimalizika kwa Simba Queens kuibuka na ushindi mnono wa bao 7-0.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikishambulia kwa zamu lakini upepo ukabadilika na dakika ya 21, Mwanahamis Omary aliipatia Simba Queens bao la kuongoza kwa shuti kali. Dakika nne baadaye, Violeth Nicholas, akapachika bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shamila Nassoro.

Simba Queens waliendelea kulisakama lango la Yanga Princess na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 29 likifungwa kwa shuti kali na Mwanahamis Omary, akimalizia kazi nzuri ya Violeth Nicholas.

Huku zikiwa zimesalia dakika tano kipindi cha kwanza kumalizika, alikuwa Mwanahamis Omary kwa mara nyingine tena alifunga bao la nne baada ya kuwachambua mabeki wa Yanga Princess.

Hadi mapumziko, Simba Queens walikuwa wanaoongoza kwa bao 4-0 na wakarudi kwa kasi kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 48, nahodha wa Yanga Princess, Flora Kayanda, alijifunga akijaribu kumrudishia mpira kipa wake.

Mwanahamis Omary alifunga bao la sita dakika ya 50 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Amina Ramadhani, huku mabeki wa Yanga wakiwa wamezubaa. Bao la saba la Simba Queens lilifungwa dakika ya 54 na Amina Bilal kwa shuti kali.

Akizungumza na MTANZANIA mara tu baada ya mchezo kumalizika, kocha wa Simba Queens, Omary Mbweze, alisema walipania kushinda mchezo wa jana na walitumia udhaifu wa wapinzani wao.

“Yanga wana wachezaji wazuri lakini upungufu wao upo katika safu ya mabeki ambayo tumeyatumia na tukashinda, mchezo ulikuwa mzuri na kila mchezaji ameonyesha kiwango chake,” alisema.

Naye, kocha wa Yanga Princess, Khamis Kinonda, alisema wachezaji wake hawana uzoefu wa ligi hiyo ndio maana wamefungwa mchezo huo.

“Simba ina kikosi kizuri ambacho kinauzoefu wa ligi tofauti na sisi, tumejitahidi kwa uwezo wetu lakini bahati haikuwa yetu,” alisema.

FURAHA: Wachezaji wa Simba Queens, wakipongezana baada ya timu hiyo kupata bao wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Yanga Princess uliochezwa Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana. Simba Queens ilishinda mabao 7-0

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.