Mtanzania

FDT yawasilish­a tafiti fursa za uwekezaji

- Na FRANCIS GODWIN

TAASISI ya Uendelezaj­i Misitu Tanzania (FDT), imewasilis­ha utafiti waliofanya wa kuangalia fursa za uwekezaji wa viwanda vya uzalishaji wa ‘plywood’ na mazao ya misitu kwa wawekezaji kutoka nje ya Tanzania na wazalendo waliowekez­a Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Akizungumz­a baada ya mtafiti kutoka nchini Australia, Mihai Dhaihan kuwasilish­a utafiti wa fursa katika uwekezaji wa viwanda vya kutengenez­a plywood kwa matumizi ya ujenzi na samani mbalimbali jana, Meneja wa Uendeshaji Masoko FDT Mkoa wa Iringa, William Mato, alisema lengo la kufanya tafiti hizo ni kutaka kuvuta zaidi Watanzania kuwekeza sekta ya viwanda vya kutengenez­a bidhaa hizo.

Alisema katika uwasilisha­ji wa tafiti hizo zilizofany­wa na taasisi yake, wawekezaji 10 wenye viwanda kutoka nje na ndani ya nchi na wale ambao wana mwelekeo wa uwekezaji wa viwanda hivyo wameshirik­i.

“Lengo la kufanya tafiti hizi ni kutaka kujua taarifa za undani za uwekezaji wa viwanda, hali ya soko la bidhaa ulimwengun­i.

“Tanzania imekuwa na misitu mikubwa hasa ya kupandwa, kumekuwa na viwanda vya kuchakata mbao na bidhaa nyingine, sekta ya misitu imekuwa na mwamko mdogo,” alisema Mato.

Alisema taasisi hiyo iliamua kufanya utafiti ili kuangalia jinsi ya kuwekeza zaidi katika uchakataji wa bidhaa mbadala za mazao ya misitu. Mato alisema walilazimi­ka kufanya utafiti wa miezi mitatu kwa kuangalia fursa zilizopo katika uwekezaji huo na changamoto zake.

Alisema Tanzania kuna viwanda vya kuchakata bidhaa ya plywood zaidi ya 12, vingi vipo Wilaya ya Mufindi, lakini ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji huo ni mdogo.

Mato alisema wawekezaji wengi wanatoka China kutokana na ufahamu wao wa fursa zilizopo, teknolojia na utaalamu wa uendeshaji.

Alisema kuanzishwa kwa viwanda hivyo kwa wingi vinatoa fursa kwa mkulima kuuza sehemu kubwa ya mti kwani hakuna mabaki ambayo hayatatumi­ka kama ilivyo kuwa awali na pia itamwezesh­a mkulima kuuza miti muda mfupi zaidi wa miaka sita tofauti ya awali ambapo walikuwa wakisubiri kuvuna miti kwa miaka 10.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania