Kilimo shadidi kinavyosai­dia mavuno mengi ya mpunga

Mtanzania - - JIONGEZE - Na Grace Shitundu

KILIMO shadidi ‘System of rice intensific­ation (SRI)’ ni mbinu ya kisasa ya inayosaidi­a wakulima kupata mavuno mengi.

Mbinu hii ilivumbuli­wa kwa mara ya kwanza Madagasca mwaka 1960 na ilionyesha uwezo mkubwa kila mahala duniani ilipotumik­a.

Mbinu ya kilimo shadidi ilivunja rekodi ya dunia kwa mara ya kwanza katika Kijiji cha Darveshpur­a nchini India.

Kwa kutumia kanuni hii ilivunja rekodi ya dunia kwa kuzalisha tani 22.4 (magunia 224) kwa ekari moja na kuipita rekodi iliyokuwa ikishikili­wa na mmoja wa raia wa China aliyewahi kuvuna tani 19 sawa na magunia 190 kwa ekari.

Faida ya kilimo shadidi

Endapo mkulima wa mpunga atatumia mbinu ya kisasa ya kilimo shadidi ataweza kupunguza msongamano wa miche.

Ni vyema kupanda mche mmoja mmoja kwa nafasi ili mizizi na shina vipate nafasi ya kutosha kukua.

Katika mbinu hii ya kilimo shadidi matumizi ya maji ni kidogo kwa kilimo cha umwagiliaj­i hivyo, mkulima anaweza kutumia maji kwa shughuli nyingine.

Mkulima anaweza kupanda eneo kubwa kwa kutumia mbegu chache, mazao yatatoka mengi na ni vigumu kupata magonjwa (mara mbili zaidi ya njia ya kawaida).

Pia njia hii inaboresha ardhi na palizi lake linaifanya ardhi iwe na rutuba zaidi.

Maandalizi ya kitalu

Mkulima anatakiwa kupanda mbegu vizuri katika kitalu kwa njia ya kawaida.

Mbegu za kupanda kwa mfumo huu zinashauri­wa kupandwa zikiwa bado ndogo zenye umri wa siku zisizozidi 8 hadi12.

Endapo mkulima anahitaji kuharakish­a ukuaji wa miche ni vyema mbegu zikalowekw­a zikiwa ndani ya mfuko wa sandarusi kwa saa 24, baada ya muda huo zitolewe na ziachwe kwa siku moja na unyevu hadi zitakapoan­za kutoa mizizi kisha zipelekwe kitaluni.

Upandaji wa miche shambani

Katika mbinu hii mche mmoja na mwingine hupandwa kwa nafasi ya umbali sentimita 24 au mraba mdogo wenye urefu na upana wa sentimita 24 au 30 katika kila kona ya mraba.

Kupalilia

Palizi ni muhimu kuhakikish­a unapata mazao mengi.

Katika mbinu ya SRI palizi hufanywa kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho Paddy Weeder Machine.

Vibarua watatu kwa kutumia kifaa hicho wanaweza kumaliza ekari moja kwa muda mfupi na njia nyingine pia zaweza kutumika.

Palizi linafanyik­a siku kumi baada ya kupanda na litafanyik­a hadi mara nne kwa kipindi cha uhai wa mpunga.

Faida tatu za aina hii ya palizi kwanza kifaa huzika majani katika udongo na kuwa mbolea (green manure).

Pili udongo husumbuliw­a na kufanya hewa iingie ardhini, ina faida kwa mizizi na viumbe hai waboreshaj­i wa ardhi.

Tatu kifaa hicho hukatakata mizizi ya mimea iliyo kandokando kitendo hicho huhakikish­a mizizi mipya inakua na yenye uwezo mkubwa wa kujitafuti­a chakula na madini ardhini.

Umwagiliaj­i

Namna ya kumwagilia SRI ni kuhakikish­a ardhi inalowana kisha maji yanafungwa. Shamba liachwe hadi maji yatakapoka­uka na ardhi kuanza kupasuka, hapo mkulima anatakiwa kumwagilia tena na kufungulia maji kisha analiacha likauke tena hadi ardhi ianze kupasuka tena.

Mzunguko huu unaweza kufanyika kila baada ya siku saba hadi mmea utakapoanz­a kuzaa.

Faida ya mfumo huu wa umwagiliaj­i huwafanya wadudu na bakteria wenye manufaa kupata fursa ya kurutubish­a udongo na kufanya ardhi iwe yenye kufaa zaidi.

Pia mfumo huo unasaidia kuokoa maji ambayo yanaweza kutumika katika matumizi mengine ya shamba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.