‘Ukweli unafichwa kufungwa UCC’

Rai - - MBELE -

KATIKA gazeti la RAI toleo la Alhamisi tarehe 23/08/2018 kuna habari inayozungumzia “mamilioni ya ada yapotea UDSM.” Kwenye habari hii, mwandishi amefanya mahojiano na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Rutinwa kuhusu taarifa hiyo.

Ndani ya mahojiano hayo limeibuka suala la kufungwa kwa baadhi ya matawi ya Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta (UCC).

Katika maelezo yake Prof. Rutinwa ametaja sababu kuu mbili:

Kwanza ni kutii agizo la. Rais Dk. John Magufuli. Huu ni upotoshaji wa kauli ya Rais wetu. Alichoagiza Rais ni Taasisi na Idara za Serikali kuhamisha R¿VL ]DNH WRND NZHQ\H majengo ya watu binafsi na kuhamishia kwenye majengo ya serikali ili kupunguza mzigo wa kodi ya pango (gharama) za uendeshaji) na sio NXIXQJD R¿VL

Lakini UCC ilitekeleza agizo hili kwa kuhamisha matawi ya Mbeya, Mwanza na Arusha ambayo yaliondolewa kwenye majengo ya watu binafsi na kuhamishwa kwenye majengo ya serikali. Wakati huo huo tawi la Mbezi lilishafungwa, sasa sijui hili lilifungwa kwa agizo lipi? Kuna jambo OLQD¿FKZD

Pili ubora wa mafunzo yanayotolewa na UCC yamepitwa na wakati. Hii ni hoja isiyo na mashiko, swali la kujiuliza ni mafunzo gani yaliyopitwa na wakati? Je, ili kwenda na wakati, ukiwa unauza bidhaa au huduma iliyopitwa na wakati XQDIXQJD R¿VL DX XQDEXQL bidhaa/huduma mpya?

Prof. Rutinwa anafanya niamini kuwa management ya UCC iliyopo sasa na Bodi ya UCC zimeshindwa kuwa wabunifu katika kipindi hiki cha ushindani na wao kama wamiliki wamekubali matokeo ya kufunga vituo bila kupata mshauri mtaalamu wa namna gani unainyanyua UCC. Kuna MDPER OLQD¿FKZD

-DPER JDQL OLQD¿FKZD"

Katika notisi ya kupunguza wafanyakazi iliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa UCC Dk. Elinami J. Minja, kwenda kwa

wafanyakazi wote na kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (THTU) yenye kumbukumbu namba CC-70-EJM/ejm/2 ambayo imesainiwa na kugongwa muhuri tarehe 01 Juni, 2018 zimetajwa sababu za kufungwa matawi ya UCC na kupunguza wafanyakazi.

Katika sababu hiyo hakuna sababu alizozitaja Prof. Rutinwa kwenye mahojiano yake. Badala yake notisi imetaja kuwa kampuni imekuwa ikipata hasara katika kipindi cha miaka saba (2010/11 hadi 2016/17) ya zaidi ya bilioni moja na nusu (Tzs 1.5 bilioni). Ukweli ni upi? .XQD MDPER OLQD¿FKZD

Ushirikishwaji wa wafanyakazi

Zoezi la kufunga matawi na kupunguza wafanykazi haliendeshwi kwa kuwashirikisha wafanyakazi, bali kwa vitisho na maagizo toka kwa wakubwa kwenye management. Na iwapo mfanyakazi atahoji kinachofanyika ni kumchukulia hatua za kinidhamu (mfanyakazi huyo) au kumhamisha kituo cha kazi na kumbadilishia majukumu wapo waliohoji waliondolewa kwenye nafasi za ukuu wa idara na kupelekwa kufundisha hizo kozi wanazosema zimepitwa na wakati.

Kama wafanyakazi hatuamini kama kampuni imeendeshwa kwa hasara kwa kipindi cha miaka saba. Tunaweza kuamini ukweli huo iwapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) akipewa jukumu la kukagua na tukaonyeshwa ripoti yake. Sisi tunaamini usimamizi mbovu wa management umesababisha hiyo hasara na management inaamini sisi wafanyakazi ndio tunaosababisha hasara, ukweli unaweza kuwa wapi?

Kipindi cha mwanzoni 2010/2011 tuliongozwa na Prof. Beda, lakini kwa hila aliondolewa kwenye nafasi kwa kuonekana ananufaika sana ndani ya UCC. Akiwemo Prof. Beda wafanyakazi tuliweza kupandishwa mishahara kila mwaka, tuliweza kupata bonus kwa kuvuka malengo ya bajeti na tulikuwa tunapata mishahara kwa wakati. Sidhani kama tunaweza kuwa na hasara halafu wafanyakazi wakaongezwa mshahara.

Kipindi cha mwishoni 2010/2011 hadi 2011/2012 tuliongozwa na Dk. Casmir ambaye kwa mara ya kwanza alituaminisha kuwa kampuni imeendeshwa kwa hasara wakati wa Prof. Beda, akatoa ahadi ya kuongeza mishahara kuandaa “Scheme of Service” na kulipa mshahara wa 13 (yaani Disemba, 2012 tungepata mishahara mara mbili). Katikati ya mwaka 2011/2012 alitangaza kupata faida ya zaidi ya milioni 600 na kutoa ahadi kemkem.

Cha kusikitisha “Scheme of Service” ilipoanza kutumika baadhi ya wafanyakazi walipewa nyongeza kubwa ya mshahara wakati wengine hawakuongezwa kitu. Tulipohoji tunaambiwa cheo chake kipya kinastahili mshahara alioongezwa. Ilituvunja moyo sana.

Kipindi cha mwishon 2012/2013 na mwanzoni 2014/2015 tuliongozwa na Dk. Olingeta Mbamba ambaye alijikita zaidi kwenye kurudisha morali ya wafanyakazi. Pamoja na kutopata nyongeza ya mshahara katika kipindi chake lakini alitoa motisha mbalimbali ikiwemo hela kwa kushiriki Siku ya Wafanyakazi na kushiriki Siku ya Wanawake Duniani.

Wakati Dk. Mbamba ameanza kuwashughulikia ZDOLRIDQ\D X¿VDGL QGDQL ya UCC kwa kula ada za wanafunzi na kutoa risiti feki, aliondolewa kwenye nafasi yake na kurudishwa UDBS. Na matokeo yake wale wote waliopelekwa mahakamani walishinda kesi. Kuna jambo OLQD¿FKZD

Alipoondolewa Dk. Mbamba ameletwa Dk. Ellinami Minja, huyu ni tatizo ndani ya Kampuni. Ni mbabe, hataki kukosolewa na si kiongozi UD¿NL QLQDFKRDPLQL QL kwamba yeye tu ndio yuko sahihi na wale wenye PhD holder ndio wanaoweza kumshauri wengine hawana uwezo wa kumshauri.

Tangu ameingia madarakani haonyeshi uchungu iwapo kampuni LWD¿OLVLND DPHNXZD DNLWRD kauli mara kwa mara kuwa UCC ikifa yeye hatoathirika kwa sababu ajira yake ipo UDSM na sio UCC. Vile vile amekuwa akitoa matishio ya kufunga branch LVL\R¿NLD PDOHQJR 1D QL kweli amelifunga tawi la Mbezi japokuwa lilikuwa linaingiza pato kubwa katika kampuni.

Hatujaona juhudi zake za kushirikisha wafanyakazi katika kuikwamua UCC, badala yake anawatumia wateule wake kumshauri na kujenga misimamo. Amejitahidi kuhakikisha anawapa wafanyakazi wakati mgumu ili waondoke kwa kulipa mishahara tarehe 8 hadi 10 ya mwezi unaofuata. Baada ya wafanyakazi kupitia chama cha THTU kutaka mkutano wa kujadili kucheleweshwa mishahara ndio akarudisha ulipaji wa mishahara tarehe 26 ndani ya mwezi husika.

Ndugu mhariri tunaomba kama sehemu ya uandishi wa habari mtusaidie kufuatilia ukweli ndani ya kampuni ya UCC. Sisi wafanyakazi tumeshika makali tukihoji tunabambikiwa makosa ili tufukuzwe kazi na kukosa haki zetu.

Sasa hivi kuna mchakato unaendelea wa kuwapunguza wafanyakazi kama notisi ilivyoeleza, lakini wanakusudia kuminya haki ya malipo stahili. Taarifa za ndani zinadai kuwa mfanyakazi aliyedumu kwa miaka 17 au zaidi atalipwa kiinua mgongo milioni 6 na wengine watalipwa milioni tatu. Hii ni dhuluma na WXQDLVXELUL LOL WX¿NLVKDQH mahakamani.

Binafsi naomba nisijitambulishe kwa sababu za kiusalama, lakini naamini mtaniamini na mtaitoa hii habari ili kusaidia kupatikana ukweli kwa kufunga matawi ya Kituo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu Dar es Salaam (UCC). Mwandishi wa barua hii nimiongoni mwa wafanyakazi wa UCC

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.