HISTORIA HAIWEZI KUMTENGA KIRILO JAPHET

Rai - - MBELE - MARKUS MPANGALA

Katika historia kuna matukio mbalimbali yaliyofanyika kwenye taifa hili. Leo tumwangalie Kirilo Japhet ambaye alitoka katika Mkoa wa Meru. Historia tunayoandika hapa leo ni kutokana na andiko la kitafiti la Dk. Simeon Mesaki wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Andiko la Dk. Mesaki, ‘Recapping the Meru Land Case, Tanzania’ lilichapishwa katika jarida la Global Journal of Human Social Science Economics, Vol. 13 la mwaka 2013.

Katika jarida hilo ndipo mwanazuoni huyo anatueleza namna gani ni muhimu kumkumbuka Kirilo Japhet. Dk. Mesaki. anaeleza mgogoro wa ardhi uliowakumba wananchi dhidi ya uliokuwa utawala wa Ujerumani na baadaye Uingereza kama msimamizi wa Tanganyika kwa niana ya Umoja wa Mataifa.

Anasema, mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Meru dhidi ya wakoloni ulisababisha zaidi ya watu 25 kutiwa mbaroni mwaka 1938.

Wakati ukitafutwa utatatuzi wa suala hilo ndipo jina la Kirilo Japhet lilipoibuka. Kisha suala la utatuzi lilifikishwa kwenye Baraza Kuu ambalo lilitakiwa kutoa suluhisho.

Kirilo alikuwa mwakilishi wa wakulima wa Meru katika mgogoro huo wa ardhi. Kipindi hicho Tanganyika ilikuwa inasimamiwa na Uingereza.

Umoja wa Mataifa uliipatia Uingereza dhamana ya kuisimamia Tanganyika mara baada ya Ujerumani kushindwa vita.

Kutokana na wananchi kuwa na mgogoro na serikali ya usimamizi (Uingereza) kama ilivyoanzia enzi za Ujerumani, basi wakulima waliamua kutuma mwakilishi wao kwenda Umoja wa Mataifa kulalamikia jambo hilo.

Kirilo alikuwa Mtanganyika wa kwanza kwenda Umoja wa Mataifa na kuwakilisha wananchi wa Meru. Historia inatueleza kuwa na Japhet Kirilo aliweza kuhutubia Umoja Mataifa na kuelezea kile kilichokuwa kikiendelea Meru na wakoloni kwa nyakati tofauti.

Kirilo alikwenda Umoja wa Maifa mwaka 1952 kwa niaba ya Wameru. Miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyojitokeza kwenye safari hiyo ni kuongezeka msukumo wa madai ya uhuru kwa kuunganisha jitihada za viongozi wa kikabila na wale walioanza mchakato wa kuunda TANU.

Katika sehemu ya utetezi wake kuhusu wakulima hao pamoja na kusisitiza mapambano ya uhuru wa Tanganyika. Kirilo alifanya jitihada kubwa kisiasa hapa nchini na tangu wakati wa mgogoro wa ardhi wakati wa uongozi wa Mangi Sante kule Meru.

Katika kipindi hicho inaelezwa kuwa kulikuwa na wasomi wengi katika utawala huo. Baada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa, Japhet Kirilo alimpa mwaliko Anton Nelson ili aje Meru kumsaidia kuwafundisha wananchi wake katika masuala ya elimu na kadhalika.

Mwaka 1954 kabla ya Tume ya Umoja wa Mataifa kuitembelea Tanganyika, Mwalimu Nyerere na S. Kandoro walimuomba Japhet Kirilo kufanya ziara kote nchini kwa mwamvuli wa TANU ili kuwaelezea matatizo ya ardhi yaliyokuwa yakiikabili Meru kwa wakati huo.

Katika kipindi hicho TANU ilikuwa imefungiwa kufanya shughuli za kisiasa na Uingereza. Japhet Kirilo alizaliwa mwaka 1921 na kufariki dunia mwaka 1997.

Jina lake kamili ni Kirilo Japhet Ayo, alizaliwa katika kijiji cha Poli, Nkoaranga ambapo sasa ni wilaya ya Arumeru. Baba yake aliitwa Nganayo au maarufu Ngura Ayo, ambaye alikuwa kiongozi wa jadi kijijini hapo na wakulima wa zao la kahawa wa Meru.

Kirilo alifariki dunia Mei 30, 1997, na kumwacha mkewe, Ndeleto Kirilo. Alicha watoto sita, ambao kati yao wannne ni wasichana.

Watoto wake wawili wa kiume Zakaria Kirilo na Jefferson Kirilo wanaishi Marekani. Anna Kirilo ni mtoto wake wa kike ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Mount Meru.

Katika maisha yake Kirilo alifanikiwa kupata elimu yake kwa miaka nane na alisomea ualimu katika Chuo cha Marangu. Baadaye alifanya kazi serikalini akianzia Mpwapwa, mkoani Dodoma na Arusha.

Wakati alipoteuliwa kuwa mwakilishi wa wakulima waliokuwa kwenye mgogoro mjini Meru, Kirilo alikuwa na miaka 31. Pia alikuwa mashuhuri wakati akiongoza tawi la chama cha TAA akiwa Katibu Mkuu.

Kirilo alikuwa shupavu katika ujenzi wa hoja katika vikao mbalimbali vya Baraza vya wilaya kuanzia mwaka 1950 na kuwa alama bora kwa wananchi wa Meru.

Katika kipindi hicho TANU ilikuwa imefungiwa kufanya shughuli za kisiasa na utawala wa mkoloni wa Kiingereza. Japhet Kirilo alizaliwa mwaka 1921 na kufariki duniamwaka 1997.

Jina lake kamili ni Kirilo Japhet Ayo. Alizaliwa katika kijiji cha Poli, Nkoaranga ambaposasa ni wilaya ya Arumeru. Baba yake aliitwa Nganayo au maarufu Ngura Ayo, ambaye alikuwa kiongozi wa jadi kijijini hapo na wakulima wa zao la kahawa waMeru.

Kirilo alifariki dunia Mei 30, 1997, na kumwachia mkewe, Ndeleto Kirilo watoto sita wakiume na wanne ni wasichana. Bahati mbaya watoto wawili wa kiume walifarikidunia.

Watoto wake wawili wa kiume Zakaria Kirilo na Jefferson Kirilo wanaishi Marekani. AnnaKirilo ni mtoto wake wa kike ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya MountMeru. Katika maisha yake Kirilo alifanikiwa kupata elimu yake kwa miaka nane na alisomea ualimu katika chuo cha Marangu. Baadaye alifanya kazi serikalini akianzia Mpwapwa, mkoani Dodoma na Arusha.

Wakati alipoteuliwa kuwa mwakilishi wa wakulima waliokuwa kwenye mgogoro mjini Meru, Kirilo alikuwa na miaka 31 tu. Pia alikuwa mashuhuri wakati akiongoza tawi la chama cha TAA akiwa Katibu Mkuu.

Kirilo anaelezwa kuwa shupavu katika ujenzi wa hoja katika vikao mbalimbali vya Baraza vya wilaya kuanzia mwaka 1950 na kuwa alama bora kwa wananchi wa Meru.

Babayake Ngura Ayo licha ya kuwa kiongozi wa kijadi, pia alikuwa mweka hazina wa kanisa huko Meru. Mzee Ngura Ayo anatajwa kuwa mkulima wa kwanza kununua Trekta mwaka 1935 na kuwa mkulima wa kisasa.

Dk. Mesaki anamwelezea Kirilo Japhet kama miongoni mwa wapigania uhuru wasiokuwa na woga kipindi hicho. Alifanya kila njia kuhakikisha waafrika wenzake wanapata haki zao za msingi.

Hata hivyo, kama walivyo viongozi wowote, Kirilo Japhet hakukosa tuhuma kutoka kwa wakulima wenzake na wananchi wa Meru.

Mara baada ya kuwasili Meru akitokea Marekani, Kirilo Japhet alituhumiwa kutafuna fedha za misaada za ushirika. Jambo jingine baya lililowahi kumtokea ni kitendo cha kumiliki ekari 60 za ardhi, na kumfanya Kirilo kuwa mkulima wa kiwango bora wakati huo. Hata hivyo, ardhi hiyo ilimsababishia matatizo makubwa na kugharimu nafasi yake ya uongozi ndani ya chama na ubunge kwa madai alikuwa bepari (mnyonyaji).

“Nilikuwa mbunge kati ya mwaka 1971 na 1974. Nilituhumiwa kuwa na fedha nyingi, na nililazimishwa kuuza mashamba yangu ikiwa ni sharti la kuendelea na ubunge.

“Lakini nilikataa sharti hilo kutokana na kiasi na faida za kulima kahawa kwa wakulima wa Meru kilikuwa kikubwa. Hivyo alichagua kuwa mwakilishi wa wakulima wa kahawa katika maeneo mbalimbali Afrika,”

Kirilo alikuwa mstari wa mbele kuendesha harambee ili kupata fedha za kuwasomesha nje ya nchi vijana wa Meru. Miongoni mwa walionufaika na harambee hizo ni Peter Kishuli Pallangyo, Eliawira Ndossi, Moses Ndosi, Mathias Kaaya, Mike Urio, Ndewira Kitomari.

Hivyo Kirilo alichagua kuishi na wakulima wenzake kuliko sharti la kuuza mashamba yake (AMHT3, 1988). Kwa utawala wa kikoloni, Kirilo Japhet alikuwa raia mkorofi na mwanasiasa hatari.

Lakini Kirilo alikuwa akifanya kazi kubwa ya mapambano ya uhuru na wakati wa shughuli zake aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali hapa nchini chini ya mwamvuli wa TANU.

Kirilo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU katika jimbo la Kaskazini. Kirilo Japhet baada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa alibaki nchini Marekani kwa mwaka nzima akijifunza mambo mbalimbali.

Kirilo alifanikiwa pia kukusanya michango mbalimbali ya kifedha kutoka nje ya nchi na kujenga shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi kwa wakazi wa Meru. Kirilo pia alishiriki kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na Jenerali Mrisho Sarakikya.

Katika kipindi hicho inaelezwa kuwa kulikuwa na wasomi wengi katika utawala huo. Baada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa, Japhet Kirilo alimpa mwaliko Anton Nelson ili aje Meru kumsaidia kuwafundisha wananchi wake katika masuala ya elimu na kadhalika.

Japhet Kirilo, (kulia), akizungumza na mmoja wa viongozi wa serikali ya kikoloni Ralph Bunche

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.