MAISHA NI PAMOJA NA MISUKOSUKO

Rai - - MBELE - NA MUDHIHIR M. MUDHIHIR 0784 307271

Sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu imesheheni misukosuko inayomletea taabu na mihangaiko mingi. Ipo misukosuko inayosababishwa na mahitaji ya msingi katika kujikimu kimaisha kama vile chakula, makaazi na mavazi. Ipo misukosuko inayoletwa na mahitaji ya huduma za lazima kama ile matibabu na elimu. Na ipo misukosuko ambayo ni matokeo ya maingiliano ya kijamii.

Husemwa kuwa maisha ni tamu na chungu, ni raha na karaha, ni furaha na huzuni, ni kicheko na kilio na kwa kweli maisha ni tambarare, milima na mabonde. Maisha hayatabiriki na hugeuka muda wowote kama rangi ya kinyonga. Maisha yanapokuwa vita pigana hadi ushinde na yanapokuwa bahati ifumbate isikuponyoke. Upo hapo!

Ni ujinga uliopindukia mipaka na ubwete wa kutemwa mate po kwa mtu kutamani kupata riziki yake kama jeta. Kijana barobaro unatamani kulishwa kama ulivyokuwa unatiwa chuchu midomoni enzi zile za uchanga! Unatamani utafutiwe suruali na shati kama ulivyokuwa unabadilishwa nepi ulipokuwa unapakatwa mapajani! Huu ni utoto ndani ya ukubwa.

Babu yetu Adam na bibi yetu Hawa walipoondolewa peponi na kuletwa duniani walipewa na maagizo. Moja, watafute riziki kwa jasho lao. Biblia inatuambia kwamba asiyefanya kazi na asile. Koran inatuamrisha tutawanyike katika ardhi ya Mwenyezi Mungu tukajitafutie riziki. Kazi ndiyo uhai na ndiyo maisha. Tazama moyo ukishindwa kufanya kazi uhai hugeuka mauti.

Misukosuko ya maisha si kwenye shida na dhiki tu. Tajiri mwenye mapesa yake hukumbwa na masaibu akakosa furaha na raha akawa anaogelea ndani ya dimbwi la huzuni. Watu wenye majina makubwa na heshima zao hugubikwa na izara ikawaingia fedheha hadi kutamani ardhi ipasuke iwamezee mbali. Misukosuko haina mwenyewe.

Wapo wasaka tonge ambao hulivaa tabasamu kwa raha zao hadi wenye vijisenti vyao wakawa midomo wazi kushangaaa kinachomfurahisha masikini. Hawatambui kwamba mahali inapokaa furaha ya mtu ni ndani ya nafsi yake na siyo machoni na midomoni mwa watu wengine. Anayeyafahamu maisha haiwi shida kwake kuyaishi. Misukosuko ni sehemu ya maisha.

Kwa hivyo ndugu yangu huna chembe ya sababu ya kushika tama au kukipakata kichwa juu ya bega ati kichwa kimevurugwa. Huko ni kuridhia kusumbuliwa na matatizo bandia au matatizo ya kufikirika. Tatizo la kweli likikufika hushiki tama na kuhuzunika. Akitokea nyoka utamuua au utakimbia kujinusuru. Usiyaruhusu matatizo bandia kukutia msukosuko hadi kukujaza msongo wa mawazo.

Wala usishike tama kwa kuiwaza kadhia itakayokufika na huku ukiomboleza ati utauficha wapi uso wako. Kadhia ijayo nayo ni ya kufikirika isiyo na uhalisia, na ikiwa nyoka huyo ni wa kweli basi muda wa kushughulika naye ni huu. Usiiruhusu kadhia ijayo ikutie hofu na kukukatisha tamaa hadi vikakufika vifo vingi bandia na hali kifo chako halisi bado kipo mbali nawe.

Zipo changamoto zinazotokana na matakwa ya kiutawala kama vile kanuni za TFDA, OSHA, Zimamoto na Baraza la Mazingira. Fimbo za wakubwa huwa hazitambui uwezo wa watoto wanaosimama dede wala wanaotembea tete. Kwa mwenendo huu wabanguaji wadogo hasa wale wakulima vijijini hawawezi kusonga mbele. Mimi siamini hata kidogo kuwa ati hamna namna za kuwashika mkono wabanguaji wadogo na wa kati.

Ikiwa vibanda vya mama lishe, vihoteli vya mitaani, wakaanga chips, samaki na mihogo nao wanahusika na vyakula vya wanadamu, kwa nini masharti ya viwango vya vyakula na mazingira yang’ate zaidi kwenye korosho tu? Au tatizo ni hili jina la kiwanda? Mashamsham haya hatuyaoni kwenye vibanda vya kukoboa na kusaga nafaka.

Sisemi kwamba vyombo hivi vilivyoundwa kisheria na vinavyofanya kazi muhimu ya kulinda afya ya walaji na bidhaa za nchi yetu, na vinavyolinda wafanyakazi na mazingira yake, visitimize wajibu wao. Hata kidogo! Ninachosema ni kuviomba vyombo hivi vijishughulishe kidogo ili vione sababu na namna ya kutunisha misuli yao.

Japowapowanaosemakwamba soko la korosho zilizobanguliwa nalo ni changamoto, binafsi nasema hapana. Soko bado ni kubwa hapa ndani, Afrika Mashariki, nchi za SADC na huko duniani. Masuala ya soko yasitutie hofu kiasi cha kututoa nje ya shabaha yetu ya kuliongezea thamani zao la korosho. Tukaze buti hakuna kurudi nyuma.

Changamoto kubwa tuitarajie kutoka kwa wabanguaji wakubwa duniani. Kwao wao ubanguaji wa korosho ni chanzo cha uhakika cha ajira kwa raia wao. Ni chanzo kikubwa cha mapato ya ndani na chanzo muhimu cha fedha za kigeni. Korosho zetu ndiyo bora zaidi duniani, na wao miaka nenda miaka rudi ndiyo wanunuzi wa korosho zetu ghafi. Hawatokaa kimya, tujiandae.

Siishi kujiuliza kwa nini waliouziwa viwanda vyetu vya kubangua korosho hawabangui. Halafu ni kwa nini miongoni mwao ni wanunuzi na wasafirishaji wakubwa nje ya nchi korosho ghafi. Najiuliza pia kwa nini tozo ya kusafirisha korosho ghafi nje ya nchi (export levy) haileti matarajio yetu ya kuimarika ubanguaji hapa nchini. Maswali haya yanayo majibu.

Hapana! Hatuna sababu ya kuendelea kuuza nje ya nchi korosho zetu ghafi. Waziri Tizeba umefanya jambo jema kukaa meza moja na wabanguaji wa korosho ili kujua kulikoni. Picha inayonijia kichwani ni ile ya wewe Waziri Tizeba kuambiwa kuwa ubanguaji korosho hapa nchini hauwezekani. Kutamani kubangua korosho hapa nchini ni kutangaza vita ngumu ya kiuchumi.

Kukutana na wabanguaji korosho ni kama kupeleka sampuli za mgonjwa wako maabara. Utayatambua matatizo yanayomsibu mgonjwa wako. Je, utaishia hapo? Hapana! Yafikishe matokeo ya maabara kwa jopo la madaktari. Mheshimiwa Waziri madaktari wako ni wataalamu wako. Ni suala la uamuzi tu ndilo litakalofanikisha ubanguaji wa korosho zetu.

Kikao chako Waziri Tizeba na wabanguaji wa korosho hapa nchini si jaribio la kwanza. Yamekuwapo majaribio kadhaa ambayo hayakuzaa matunda. Tunahitaji kufanya uamuzi kama tulivyofanya wakati wa kuanzisha viwanda hivi wakati wa awamu ya kwanza. Tuwasikilize wabanguaji, tuwashike mkono na tuweke dhamira, ubanguaji unawezekana Tanzania.

Katika hoja zangu humu utaona Mheshimiwa Waziri kuwa sikujielekeza sana kwa wabanguaji wakubwa. Nimefanya hivyo kwa kutambua kuwa hawa wakitaka na wakiamua kubangua korosho wanaweza kufanya hivyo. Serikali inahitaji tu kuwa karibu nao kwa ajili ya mashauriano katika kuzikabili changamoto zitakazokuwa zinaibuka hapa na pale. Mitaji si suala gumu sana kwao.

Nimejielekeza sana kwa wabanguaji wadogo kwa sababu kwanza wanayo nafasi kubwa na muhimu katika kufanikisha dhamira ya ubanguaji korosho na kuwaongezea kipato. Pili, kuanzisha vikundi hivi, kuviwezesha visimame na viwe endelevu vinahitaji utashi wa serikali. Waziri Tizeba umeonyesha nia na wataalamu hawana budi wakuunge mkono.

Bodi ya Korosho na Tume ya Ushirika ni wasaidizi wako wakuu katika suala hili. Kwa sisi tuliokaribu na vyombo hivi tunaziona ishara za mvutano usio na tija. Watanzania hatuhitaji kufahamu ni nani mkubwa kati ya hawa wawili. Tunachohitaji ni mahusiano yenye afya yatakayowezesha utendaji wa pamoja katika kuleta ustawi wa Tasnia ya Korosho nchini.

Misukosuko ya maisha si kwenye shida na dhiki tu. Tajiri mwenye mapesa yake hukumbwa na masaibu akakosa furaha na raha akawa anaogelea ndani ya dimbwi la huzuni. Watu wenye majina makubwa na heshima zao hugubikwa na izara ikawaingia fedheha hadi kutamani ardhi ipasuke iwamezee mbali. Misukosuko haina mwenyewe.

Wakulima wakibangua korosho

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.