Mukwanagobe: Mwanajeshi wa kwanza mwanamke Namibia

Rai - - MAKALA - KIZITO MPANGALA

Historia ni darasa kubwa linalotoa mafundisho ya nyuga mbalimbali katika maisha yetu kwa kuwa tunapata nafasi ya kujifunza mambo ya kale na kuhisisha na ya sasa. Katika hilo, mambo mengi ya sasa yanatokana nay a kale amabpo ya sasa yameboreshewa mazingira hasa katika kigezo cha Sayansi na Teknolojia. Historia siyo jambo la kubhatisha ikiwa morali ya kutaka kuijua itawekwa.

Mambo mengi duniani yana mwanzo wake na pia yana mtu au watu wa mwanzo walioanza na baadaye kuendelezwa na wengine. Ni kama vile katika Hisabati mada ya mipangilio na mikururo lazima pawepo na mtajo wa kwanza ili kujuwa mitajo inayofuata kwa tabia ile ile ya mtajo wa kwanza. Hivyo, historia ina manufaa makubwa ili kuboresha mambo mbalimbali kulingana na uga husika.

Katika historia ya mapambano dhidi ya serikali za kikoloni barani Afrika, wanaojulikana sana ni wanaume kuliko wanawake ambao walikuwa na morali ya kupigania mataifa yao. Ni dhahiri kwamba Winnie Mandela anajulikana na wengi duniani kuliko Mukwanagobe au Phila Ndwandwe wa Afrika Kusini. Hailazimishwi kuwa wao wajulikane, lakini kujulikana kwao kunaleta mafunzo mbalimbali muhimu.

Mukwanagobe Auguste ya Immanuel aliyejulikana sana kwa jina la Mueekulu Mukwahepo ni miongoni mwa mashujaa wa taifa la Namibia ambao walipigania taifa hilo wakati likiitwa South – West Africa chini ya Serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini. Mukwanagobe alijitolea kuwa mwanajeshi katika kikosi cha PLAN (People’s Liberation Army of Namibia) kilichokuwa sehemu ya chama cha SWAPO (South-West Africa People’s Organization).

Alizaliwamwakatarehe7mwezi Oktoba, 1937, nchini Namibia. Mwaka 1963, Mukwanagobe aliungana na kikundi cha wanaume kilichoongozwa na mumewe, waliondoka nchini Namibia na kwenda uhamishoni nchini Angola. Wakiwa Angola walivumilia masaibu mengi yakiwemo njaa na vita. Weneyewe walikuwa wanaita “iota yomakatana.” Baadaye wakakata shauri la kwenda nchini Tanganyika (sasa ni Tanzania). Walianza safari yao mjini Cabinda (Angola), hadi nchi Zaire (sasa inaitwa Jamuhuri ya Kidemikrasia ya Congo). Kutoka Zaire walipita nchini Zambia na kuingia Malawi na baadaye Tanzania. Walitumia muda wa mwaka mmoja katika safri hiyo kwani hapakuwa na usafiri wa magari mengi kama ilivyo sasa, hivyo, walilazimika kutembea kwa miguu.

Mukwanagobe au Meekulu Mukwahepo alikuwa ni mmojawapo kati ya wanawake wa Namibia walioondoka nchini mwao na kuishi uhamishoni. Lakini kivutio kikubwa kwake ni kuwa mwanamke wa kwanza mwanajeshi.

Mukwanagobe alipofika nchini Tanzania alijiunga na jeshi la SWAPO na yeye alikuwa mwanamke wa kwanza kujiunga na jeshi katika historia ya taifa la Namibia. Alipata mafunzo ya kijeshi akiwa na SWAPO huko mjini Kongwa mkoani Dodoma, Tanzania.

Aliwahi kueleza kwa nini alipewa jina la Mukwahepo. Alisema “….unajuwa, nilipofika Kongwa kule Tanzania nilikuwa bado msichana mzuri na mrembo. Nilikuwa naviziwa na kutishwa na wanaume wengi. Jambo hili lilikuwa geni sana kwangu kuviziwa. Sasa askari wote waliokuwepo pale Kongwa walipewa majina ya kijeshi ilikuficha yale halisi, basi mimi nikajipa jina mimi mwenyew nikajiita Namubaduka. Lakini wale askari waliamua kuniita Mukwahepo yaani ‘kitu duni.’ Waliniita jina hilo ili kunisumbua kutokana na hali yangu kwani nilikuwa mwanamke peke yangu kambini hapo. Mukwahepo likawa jina langu hadi sasa ingawa nililikataa lakini nilishindwa.”

Mukwanagobe alianza mafunzo ya kijeshi kambini Kongwa, Dodoma Tanzania, mwaka 1965. Kama ilivyokwishasemwa awali kwamba alikuwa ni mwanamke pekee yake katika kikosi hicho kwa muda wote wa miaka tisa aliyoishi nchini Tanzania, yaani tangu mwaka 1965 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1974, alipohamishiwa kambi ya SWAPO iliyokuwepo nchini Zambia kwa ajili ya kulea watoto wa mabini waliopelekwa shuleni na wale walioshindwa kuwalea watoto wao. Baadaye alihamishiwa kambi iliyokuwepo Angola. Aliwahi kunukuliwa akisema “sikutarajia kupangiwa jukumu hilo, lakini nililipokea kwa moyo wangu wote. Nilipofika katika hospitali ya Nyango nilikuta binti mmoja aliyejingua salama lakini alishikwa na homa kali, hivyo, nilikabidhiwa mtoto mchanga nimlee hadi mama yake alipopata ahueni na aliishi name. Idadi ya watoto waliohitaji malezi kutoka kwangu iliongezeka na walinizoea kama mama yao. Siku moja nikiwa mjini Luanda, Angola, nilipata taarifa kwamba mjini Lubango kuna mama amejifungua motto na yeye anaumwa, hakuweza kumlea, nilipewa jukumu la kumlea motto huyo.” Aliongeza kusema “wale watoto ukiwauliza baba yenu ni nani? Walijibu ‘Mukwahepo,’ ukiwauliza tena mama yenu ni nani? Walijibu ‘Mukwahepo.’”

Mwaka 2013, wakati wa uzinduzi wa kitabu kilichoeleza maisha ya Mukwanagobe au Mukwahepo, mgeni rasmi likuwa ni Raisi wa zamani, Dk. Sam Nujoma, yeye alisema “….Mukwahepo alikuwa mwanamke wa kwanza kupata mafunzo ya kijeshi na kuwa mwanajeshi kamili wa SWAPO katika kambo ya Kongwa, Tanzania pamoja na wanajeshi wengine wa kiume. Unaweza kufikiria sasa ni jinsi gani ilikuwa vigumu kwake kuwa mwanamke wa kwanza nap eke yake kati ya wanaume kambini Kongwa mwaka 1965, ambako alibaki kwa miaka 9 hadi mw1ka 1974. Pia, aliishi mjini Mbeya, Tanzania, ilkokuwa kambi yetu ya muda mfupi ambako askri walikuwa wanafanya mazoezi walipokuwa njiani kuelekea Zambia ilikuja Namibia kumtarakanya adui” alisema Sam Nujoma, 2013.

Wakati wa sherehe ya kwanza ya uhuru nchini Namibia, alifika shereheni akiwa na watoto watano ambao aliambatana nao. Watoto hao walikuwa ni miongoni mwa watoto aliowalea akiwa uhamishoni nchini Tanzania. Hii ni kadiri ya kitabu cha Ellen Ndeshi Namhila, Mukwahepo: The Woman Soldier, kuhusu maisha ya Mukwanagobe ambaye alijulikana pia kwa jina la Mukwahepo.

Alikuwa ni kiungo muhimu katika suala la elimu kwa watoto. Hivyo, alishughulika kwa bidii na kufanikiwa kufungua shule kadhaa za watoto katika kambi za SWAPO. Alikuwa mama wa hiyari wa watoto wengi katika kambi za SWAPO.

Kutokana na kutopata elimu ya kisasa, Mukwanagobe au Mukwahepo hakupata ajira popote katika Namibia huru baada ya kuwa askri wa SWAPO. Aliishi maisha duni hadi Serikali ilipoanzisha mfuko maalumu wa mafao ya askari wa zamani naye akiwemo. Mwaka 1995 alitunukiwa medani ya ushujaa na Raisi Sam Shafiishuna Nujoma na alikabidhiwa nyumba mpya ya kuishi.

Mukwanagobe au Mukwahepo alifanyiwa mazishi ya kitaifa na Raisi Dk. Hage Geingob kadiri ya Katiba ya Namibia sura ya 32 ibara ya 8, amezikwa katika eneo la makaburi ya Eenhana tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2018 baada ya kuagwa katika uwanja wa mpira wa miguu wa Eenhana nchini humo. Mukwanagobe anakumbukwa sana kwa uvumilivu wake wa kufanya kazi na kuliletea uhuru taifa la Namibia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.