Mechi ya watani wa jadi katika namba

Rai - - MICHEZO - NA MOHAMED KASSARA

01-

Idadi ya bao lililofungwa katika mchezo wa mwisho kuzitunisha timu hizo katika mchezo wa mzunguko wa pili msimu uliopita.

02-

Tofauti ya pointi baina ya timu hizo katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Yanga ikivuna pointi 12 baada ya kucheza michezo minne, Simba ikivuna pointi 10 katika michezo mitano.

03-

Tofauti ya mabao baina ya timu hizo, ambapo Yanga imefunga mabao tisa katika mechi nne, Simba ikifunga mabao sita katika mechi tano.

04-

Idadi ya mechi ambazo Yanga imeshanda tangu kuanza msimu huu

07-

Idadi ya wachezaji wa kigeni waliocheza mchezo uliopita wa Simba na Yanga msimu uliopita, Yanga watatu, Simba wanne.

11-

Idadi ya wachezaji wa Simba katika eneo la kiungo ambao wataitumikia timu hiyo msimu huu.

12-

Idadi ya wachezaji wapya ambao hawakuwepo kwenye pambano la watani wa jadi lililopita.

13-

Idadi ya wachezaji wa kigeni waliosajiliwa na timu hizo kwa ajili ya msimu wa ligi 2018/2019.

15-

Idadi ya michezo ya ligi kuu ambayo Simba ilicheza mfululizo bila kupoteza dhidi ya Yanga , michezo hiyo ilikuwa Kati ya Septemba 1, 2001 hadi April 27, 2008 Simba ilikuwa haijapteza mchezo huo wa Kariakoo Derby

19-

Idadi ya mataji ya Ligi Kuu ambayo Simba imetwaa tangu kuanzishwa mwaka 1936.

22-

Jezi ya John Bocco ambaye atakosa pambano hilo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.

27-

Idadi ya mataji ya ligi ambayo Yanga imetwaa tangu kuanzishwa 1935

29 -

Tarehe ambayo timu hizo zikutana kwa mara mwisho na Yanga kukubali kichapo cha bao 1-0, mchezo huo ulichezwa Aprili 29, mwaka huu.

30-

Tarehe ambayo timu hizo zitakutana katika msimu mpya wa ligi 2018/19, mchezo huo utachezwa Septemba 30, mwaka huu.

36-

Dakika ambayo bao lilifungwa katika mchezo kuzikutanisha timu hizo msimu uliopita.

Idadi ya wachezaji waliosajiliwa na timu hizo kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

60-

153-

Idadi ya siku zilizopita tangu mtanange wa timu hizo kukutana Aprili 29, mwaka huu.

Patrick Aussems

Mwinyi Zahera

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.