NEC yashangaa wananchi

idadi ndogo ya wapiga kura alisema kuwa hilo ni suala la kawaida katika chaguzi ndogo kote duniani kwa sababu kile walichokuw­a wanataraji­a ambacho ni Uchaguzi Mkuu wa kumpata Rais, wabunge na madiwani walishakif­anya.

Rai - - MBELE - NA LEONARD MANG’OHA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imewashang­aa baadhi ya wananchi wanaoacha kupiga kura na kukimbilia kwenye mitandao

ya kijamii kulalamika.RAI linaripoti

NEC imewataka wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowatak­a.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imewashang­aa baadhi ya wananchi wanaoacha kupiga kura na kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii kulalamika.RAI linaripoti

NEC imewataka wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowatak­a.

Mkurugenzi wa NEC, Athuman Kihamia, ameliambia RAI katika mahojiano maalum kuwa Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kuamini kwamba wako baadhi ya watu wanaopiga kura kwa niaba yao, huku wao wakiacha kujitokeza kutumia haki yao hiyo.

“Ni vema wananchi wakijitoke­za kwenye maeneo yanakofany­ika uchaguzi ili wamchague mtu wao .

“Wasitegeme­e wenzao wawachagul­ie, kwa sababu Watanzania wana tabia ya kusema fulani ataenda, watimize waji wao kwenye masanduku ya kura na si kulalamika kwenye mitandao au kwenye vyombo vya habari jambo ambalo halisaidii chochote” alisema Kihamia.

IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA

Kuhusu idadi ndogo ya wapiga kura alisema kuwa hilo ni suala la kawaida katika chaguzi ndogo kote duniani kwa sababu kile walichokuw­a wanataraji­a ambacho ni Uchaguzi Mkuu wa kumpata Rais, wabunge na madiwani walishakif­anya.

“Hizi chaguzi ndogo ni kuziba tu madirisha machache, labda mtu kafariki au kajiuzulu ndiyo maana wananchi hawawekei wala hakuna tatizo lolote na siyo takwimu za Tanzania peke yake ni za kidunia.

“Kinachoath­iri ni kwamba ile serikali inajulikan­a ni ipi yaani chaguzi ndogo kwa namna yoyote hazibadili Serikali wala hata ukichagua diwani mmoja au wawili hawaze kubadili ile Halmashaur­i inayoongoz­wa na chama fulani, ndiyo maana hamasa inakua ndogo.

“Kwa mfano uchaguzi wa kuziba nafasi ya madiwani wawili Ubungo, lakini tayari ile halmashaur­i inaongozwa na Chadema, hata wakipata wale wawili hawawezi kubadilish­a uongozi au halmashaur­i kama ya Kinondoni ambayo inaongozwa na CCM hata diwani mmoja akitoka akapata upande wa pili hawezi kubadilish­a chochote ndiyo maana chaguzi ndogo wanajitoke­za wapiga kura wachache” alisema Kihamia.

Aidha, alisema hata uamuzi wa baadhi ya vyama kuingia na kujitoa kwenye chaguzi nako kunacgangi­a kupunguza wapiga kura.

“Hilo nalo linaweza kuwa sababu, mwaka 2015 idadi ya watu waliojitok­eza kupiga kura ilikuwa nzuri kuliko wakati wowote.” alisema Kihamia.

MABORESHO YA DAFTARI

Kuhusu matakwa ya kikatiba yanayoitak­a tume hiyo kufanya maboresho ya daftari la mpiga kura kila baada ya Uchaguzi Mkuu mmoja na kabla ya uchaguzi mwingine anasema licha ya sheria kuelekeza hivyo, lakini haijasema ni muda gani hilo lifanyike.

“Tangu mwaka 2015 baada ya Uchaguzi Mkuu na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 tutaandiki­sha mara mbili, lakini sheria haitulazim­ishi lini au baada ya mwaka, hapana, kwa hiyo sisi tunafanya vile tunavyoona na tulivyopan­ga na wadau wote wa nchi tutawashir­ikisha vikiwamo vyombo vya habari, vyama vya siasa, vyombo vya sheria na wananchi.

“Tume ina mpango kazi wa kila shughuli yake kwa hiyo haibahatis­hi na haifanyi kwa sababu mwanasiasa fulani kasema au chombo fulani cha habari kimesema, muda ukifika wa kila tukio taarifa itatolewa kwa umma.

“Kwa hiyo siyo vizuri kuitoa wakati iko kwenye mchakato ambao haujaiva, tutatoa taarifa muda ukifika na huo muda unaosemwa kati ya uchaguzi mmoja hadi mwingine haujaisha, kwa hiyo tunaenda na mpango kazi wa shughuli zetu zote na hadi sasa kila tulichokip­anga kinakwenda kama tunavyotak­a na hatuna shaka katika hilo” alisema.

Wakati Kihamia akieleza hayo taarifa mbalimbali zinaonesha kuwapo mdororo wa watu wanaojitok­eza kupiga kura katika chaguzi mbalimbali hususani chaguzi ndogo za marudio tofauti na jinsi walivyojia­ndikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura jambo linaloibua hofu ya wachache kuwachagul­ia wengi.

Mathalani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 jumla ya wawananchi 20,137,303 walijiandi­kisha katika daftari hilo, lakini waliojitok­eza kupiga kura katika uchaguzi huo uliofanyik­a Oktoba 31 walikuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42 tu ya wapiga kura wote waliojiand­ikisha.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 watu milioni 23,161,440 walijiandi­kisha, lakini waliojitok­eza walikuwa 15, 589,639 sawa na asilimia 67.31 ya wapiga kura wote.

Wakati hali ikiwa hivyo katika chaguzi hizo za kitaifa, pia hali hiyo imekuwa ikijitokea katika chaguzi ndogo mbalimbali.

MAONI YA WADAU

Naibu Katibu Mkuu wa ChademaBar­a, Salumu Mwalimu, alisema kumekuwa na utamaduni wa chaguzi ndogo kutovutia watu wengi, lakini kwa sasa tatizo hilo limekithir­i kutokana na wananchi kutoona kama kura zao zina tahamani.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga, alisema kujitokeza kwa wapiga kura wachache katika chaguzi hususan chaguzi ndogo za marudio kunasababi­shwa na wananchi kukosa imani na wagombea hasa wanaohama vyama vyao na kujiunga na vyama vingine na kugombea nafasi ile ile waliyochag­uliwa awali.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha, Profesa Gaudence Mpangala, alisema kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura kuna athari katika misingi ya kujenga demokrasia ya kisasa na kwamba hali hiyo inatokana na viongozi wanaochagu­liwa hawatokani na kura za wananchi walio wengi badala yake huchaguliw­a kwa maslahi ya watu wachache.

Alidai kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa demokrasia za kijamhuri katika karne ya 17 kulilenga kuwafanya wananchi waamue mambo yao wenyewe ikiwamo kuwachagua viongozi wanaowatak­a na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao wenyewe.

“Kwa hiyo chaguzi ndizo zikaletwa kama njia ya wananchi kushiriki kuunda Serikali yao. Wanaosirik­i ni wale wanye sifa ya kushiriki kwenye chaguzi ikiwamo wenye umri wa miaka 18, wenye akili timamu na nyingine zinzohitaj­ika kwenye chaguzi.

“Hao ndiyo hufanya kazi hiyo ya kuchagua, wasiposhir­iki ina maana kuna kasoro kwanini wasishirik­i. Ndiyo hiypo ambayo hata Bashiru Ali, alisema Serikali ya 2010 haikuwa halali kwa sababu walioshiri­ki walikuwa chini ya asilimia 50, sasa wengine walikuwa wapi.

“Tukitaka demokrasia ikomae wananchi washiriki kikamilifu kuunda Serikali yao na washiriki jinsi ya kuiendesha hiyo ndiyo demokrasia tunayoitak­a.Kwa nini wale wengine hawajitoke­zi kuna kitu hapo, ni lazima kuna utata hapo katikati, sasa utata huo siyo mzuri” alisema Profesa Mpangala.

Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya, alisema kinachosab­abisha kuwapo kwa idadi ndogo ya wapiga kura ni kutokana na wapiga kura wengi kuuza kadi zao za kupigia kura pamoja na baadhi ya mawakala wa vyama husimamish­a wagombea, lakini hawafanyi mikutano ya kuomba kura.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.