KWA MBOWE, KUBENEA NA KOMU NI ‘TIMING’

Rai - - MBELE - Ole Mushi. 0712702602.

PAMOJA na madai ya Chadema kusema kuwa CCM inawanunua wabunge wa Chadema lakini naona kwa mbali assumptions nyingine.

Chadema lazima wakubali sasa kuwa wana mgogoro wa ndani ambao kama hawatakaa pamoja na kuelezana ukweli chama kitazidi kudidimia.

Hili la Mbunge Komu na Kubenea linatupa upenyo mpya wa kuchungulia nini kilichopo ndani ya chama. Nachoweza kusema kwa sasa ni kwamba.

Kubenea na Komu wanapaswa kujitathimini kama bado wanatosha kuendelea kuwa Chadema na kuongozwa na Mbowe. Katika kujitathimini huko walenge option 3 za kufanya.

1. Aidha waondoke kabisa kwenye chama na kujiunga na vyama vingine vya siasa. Hili litasaidia mno kwa mustakabali wa maisha yao na siasa zao za baadaye.

2. Wanaweza kuomba msamaha na kuamua kubaki kwenye chama. Hili ni jambo jema ila hawataaminika tena na wanaweza kutengenezewa zengwe la kuwadhuru. Wakiwa ndani ya chama in rahisi zaidi kudhurika kuliko kuwa nje ya chama.

3. Wanaweza kukaa kimya na kuendelea kubaki Chadema. Nitawakumbusha kilichomtokea Mwigamba, Zitto na Kitila. Mbowe si mwanasiasa mwepesi kihivyo, ana uthubutu wa kutake risk anaweza kufanya mawili kuwakuza au kuwamaliza kisiasa. Akiwafukuza itakuwa ni vigumu kukubalika kwenye chama kingine kirahisi.

Kutokana na option hizi tatu kilichobaki hapa kwa pande zote mbili ni timing nani atamwahi mwenzake.

Niliwahi kutoa prediction hapa kuhusu wabunge kadhaa kuhama toka Chadema. Kwenye kundi la kwanza hawa wawili Komu, na Kubenea niliwataja pamoja na Ole Millya. Kama hawa wakiondoka atakuwa amebakia mmoja tu kwenye lile kundi.

Wito wangu kwao, wakati sahihi wa kufanya maamuzi ni sasa wakichelewa kuyafanya kuna watu watayafanya badala yao na yatawagharimu zaidi. Wakikosea ‘timing’ wameisha.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.