Wawekezaji wa ndani washtuka

IKIWA siku ya saba zimepita tangu kuibuka kwa taarifa za kutekwa kwa mfanyabias­hara na bilionea kijana nchini, Mohamed Dewji (43), baadhi ya wafanyabia­shara wakubwa wameibuka na kutoa neno zito kwa serikali. RAI linaripoti.

Rai - - MBELE - NA WAANDISHI WETU

Nikiwa huku nje ninaona habari kwenye televishen­i kama vile CNN, Aljazeera na mitandao ya kijamii inavyozung­umzia utekwaji wa mfanyabias­hara maarufu.

Ali Mufuruki Lakini kwa nchi za kawaida kama Tanzania au Kenya, suala la usalama linahusika sana katika maamuzi ya wawekezaji kuja kuwekeza. Godfrey Simbeye

IKIWA siku ya saba zimepita tangu kuibuka kwa taarifa za kutekwa kwa mfanyabias­hara na bilionea kijana nchini, Mohamed Dewji (43), baadhi ya wafanyabia­shara wakubwa wameibuka na kutoa neno zito kwa serikali. RAI linaripoti.

Wafanyabia­shara hao wameweka wazi kuwa tukio hilo linawahuzu­nisha na kuwapa hofu.

Katika mazungumzo yao na RAI kwa nyakati tofauti, wafanyabia­shara hao wamesema kuwa tukio la kutekwa kwa Dewji liifungue macho serikali na vyombo vya dola kwa kuchukua hatua za haraka ili lisiwaondo­lee imani wawezekaji waliopo na wanaotaraj­iwa kuja nchini

Miongoni mwa wafanyabia­shara hao ni Mwenyekiti wa Maofisa Wakuu wa Kampuni nchini (CEOrt), Ali Mufuruki ambaye aliishauri serikali isichukuli­e kirahisi matukio hayo ya utekaji kwa kuwa yanaweza kutowesha imani ya wawekezaji kwa Tanzania.

Mufuruki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenz­i wa Vodacom Tanzania, alisema Tanzania ni moja ya nchi zenye sifa za kuvutia wawekezaji kutokana na amani na utulivu, wakiamini usalama wa watu na mali zao upo.

“Nikiwa huku nje ninaona habari kwenye televishen­i kama vile CNN, Aljazeera na mitandao ya kijamii inavyozung­umzia utekwaji wa mfanyabias­hara maarufu.

“Nina uhakika hizi habari hazipokele­wi na jamii ya wawekezaji kwa uzuri na inawezekan­a ikawatisha wakafikiri­a kwamba leo ukienda Tanzania unaweza kufanywa kama alivyofany­iwa Mo dewji.

“Hiki kitu tusikichuk­ulie kiurahisi inabidi serikali ifanye haraka kuondoa tatizo na kutoa taarifa kwa wananchi ili wawekezaji wa nje wajenge imani kuwa Tanzania bado ni salama,” alisema.

TPSF: SERIKALI ISKODOLEE MACHO KODI PEKEE

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye ameunga mkono hoja ya Serikali kuhakikish­a inamaliza tatizo hilo na kufafanua kuwa inatakiwa kuchukua hatua za haraka ili kuondoa hofu iliyoanza kujengeka nchini na kwa baadhi ya wawekezaji.

Alisema mazingira ya biashara au uwekezaji yanategeme­a mambo mengi lakini jambo la kwanza ni amani na utulivu.

Alisema hata alipokuwa kwenye ziara na viongozi hao kama vile Rais mstaafu Jakaya Kikwete, jambo la kwanza analojivun­ia ni amani na usalama kwa kuwa hakuna mwekekzaji anayekwend­a kuwekeza mahali ambapo hakuna usalama.

“Labda kuwe na ‘super profit’ kwa mfano Kongo DRC, wanapigana kila siku ila wawekezaji wapo… ina maana faida wanazopata ni zaidi ya hatari za kiusalama wanazozion­a.

“Lakini kwa nchi za kawaida kama Tanzania au Kenya, suala la usalama linahusika sana katika maamuzi ya wawekezaji kuja kuwekeza, kwa sababu mwekezaji hawezi kwenda kuweka mgodi au kiwanda kesho yake watu waje kuvunjavun­ja na mawe.

“Wanapenda waende kwenye nchi ambazo kuna mifumo imara ya usalama inayolinda wawekezaji na wananchi wake, kwamba ukija unatembea wakati wote na kufanya biashara kihalali kabisa,’ alisema.

Alisema ni kweli suala la utekaji linaweza kuwaogopes­ha baadhi ya wawekezaji hivyo ni vyema kuendelea kuifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na usalama.

“Vyombo vya dola viendelee kulinda wawekezaji na wananchi kwa ujumla ili tuendelee kuwa kivutio cha uwekezaji kwa sababu hadi sasa Tanzania ndio nchi inayoongoz­a katika Afrika Mashariki kwa kupata uwekezaji mkubwa kutoka nje. Tusiharibu sifa hiyo,” alisema.

Alisema taasisi yenye majukumu sawia na TPSF nchini Kenya imekwishaa­nzisha kitengo kinachosim­amia masuala ya usalama na ulinzi wa wawekezaji ambacho kinajumuis­ha vyombo vyote vya dola ikiwamo askari.

“Sisi TPSF tumechelew­a kidogo kuanzisha hicho kitengo ila wenzetu Kenya kwa kupitia taasisi yao ‘Kenya Private Sector Alliance’ wanacho kitengo maalumu kilichoanz­ishwa tangu mwaka 2007 kwa ajili ya kushughuli­kia masuala hayo ya ulinzi kwa wawekezaji,” alisema.

Alisema ni dhahiri kuwa suala la usalama na amani ni jambo muhimu kushinda hata kodi.

Alisema serikali isikodolee macho kukusanya kodi pekee kwani suala la usalama ndio kitu cha kwanza kinachotak­iwa kupewa kipaumbele.

“Nakumbuka Rais Kikwete alipokuwa akihutubia huko nje, alikuwa akilizungu­mzia suala la amani kwa ukubwa kabisa.

“Suala la Mo dewji kweli limeleta taharuki ni ni jambo linalotaki­wa kushughuki­wa haraka ili kuwajengea imani wawekezaji na Watanzania kwa ujumla kwa sababu ikichukua muda mrefu watu wanaweza kuhisi ni namna gani na wao wakitekwa inaweza kuchukua muda kushughuli­kiwa,” alisema.

PROF MOSHI: SERIKALI IFUMBUE MACHO

Mdhahiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Humphrey Moshi alisema suala la utekaji kwa ujumla linakosesh­a amani na halileti ustahimili­vu wa kiuchumi nchini kwani linatia hofu Watanzania na wawekezaji.

Hata hivyo, alisema licha ya kwamba tukio hilo limemtokea mwekezaji mmoja mashuhuri na si matukio ya mfululizo kama ilivyo kwa nchi za Korea, lakini serikali isilifumbi­e macho.

“Tusipuuzie kwa sababu tukio kama hili linaweza kuambukiza na kuendelea, jambo la msingi ni kwamba matukio kama haya ni ya kuepuka na yashughuli­kiwe haraka ili yasiathiri amani na usalama kwa mwekezaji.

“Mwekezaji anapokuja na mtaji wake anataka alindwe yeye, familia na nchi yetu ineemeke, hivyo tukio hili liwe kifungua macho kwa serikali na vyombo vya usalama viwe makini zaidi ili matukio kama haya yasije kuzoeleka,” alisema

ALIVYOTEKW­A

Mo alitekwa na watu wa¬siojulikan­a alfajiri ya Alhamisi ya Oktoba 11, mwaka huu katika Hoteli ya Colosseum, Oysterbay, jijini Dar es Salaam, alikokuwa anakwenda kufanya mazoezi.

Hadi sasa bado haijaju¬likana ni nani hasa aliyemteka na wapi alikofichw­a ingawa taarifa za awali zilisema tukio hilo liliongozw­a na raia wawili wa kigeni.

Watu zaidi ya 20 walikamatw­a kutokana na tukio hilo, huku Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisema hawako tayari kuruhusu vyombo vya kimataifa kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

FAMILIA YA MO

Mapema wiki hii Msemaji wa fa¬milia hiyo Azim Dewji, alitangaza kutoa dau la Sh. bilioni moja kwa mtu yeyote atakayefan­ikisha kupatikana kwa mfanyabias­ha huyo.

Dewji alisema wamefikia hatua hiyo ili kuongeza juhudi za kuhakiki¬sha mtoto wao anapatikan­a mapema.

MATUKIO YA UTEKAJI AFRIKA

Mfanyabias­hara Mohammed (Mo) Dewji anaingia kwenye orodha ya bilionea wa sita kutekwa mwaka huu barani Afrika.

Mabilionea wengine waliotekwa mwaka huu ni Shiraz Gathoo wa Afrika Kusini, Andre Hanekom wa Msumbiji, Liyagat Ali Parker wa Afrika Kusini, Michael Obi wa Nigeria, na Sikhumbuzo Mjwara wa Afrika Kusini

UTEKAJI NCHINI

Akizungumz­ia takwimu za matukio ya utekaji na upoteaji wa watu nchini, Waziri Lugola alisema mwaka 2016 walitekwa watu wazima tisa na waliopatik­ana wakiwa hai ni watano na wanne hawakupati­kana.

Alisema mwaka 2017 walitekwa watu 27 na polisi walifaniki­wa kuwapata watu 22 wakiwa hai na wawili walikuwa wamekufa huku watatu hawakupati­kana.

Kwa upande wa matukio yaliyowahu­su watoto walio chini ya miaka miaka 18, Kangi alisema kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 yaliripoti­wa matukio 18, miongoni mwao wa kiume walikuwa sita na wa kike 12.

“Kati ya hao 18, watoto 15 walipatika­na wakiwa hai, watoto wawii walikutwa wamefariki na mmoja bado hajapatika­na,” alisema.

Mohamed Dewji

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.