Siku Kambona alipozima maasi kumuokoa Nyerere

Rai - - MAONI/KATUNI - NA NDAHANI MWENDA ndahanimwe­nda66@ gmail.com

WIKI iliyopita tuliangazi­a namna historia ilivyotuel­eza kuhusu nayaka za machafuko

ambazo nchi nnyigi za Afrika zilipitia katika baada ya kupata uhuru. Watawala walipindua­na kupitia majeshi. Na nchi nyingi za Afrika, hasa Magharibi na Kaskazini, zilipitia katika kadhia hii. Nchi kama Misri, Nigeria, Morroco, Algeria, Tunisia, Guinea na nyingine nyingi yalitokea mapinduzi. Katika ukanda wa Afrika Mashariki pia yalitokea lakini haya kuwa kama ya Afrika Magharibi ama Kaskazini.

Tanzania pia yalitokea maasi ya Kijeshi lakini hayakufani­kiwa kwa kiasi kikubwa, Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, inadaiwa aliwahi kutaja kupinduliw­a mara tatu kipindi cha utawala wake. Tunapokumb­uka kifo chake hatuna budi kujikumbus­ha matukio yakiyowahi kumkuta kipindi kuwa madarakani, moja wapo ni maasi ya mwaka 1964. Endelea…

Aliyekuwa Rais wa Ghana, Kwame Nkrumah, katika hotuba yake katika mkutano mmoja wa OAU mwaka 1964, alimnanga Mwalimu kwa kudai kuwa ni ‘kuwadi wa Waingereza’ kwani aliwafukuz­a mwaka 1961, sasa anaombaje msaada tena? Lakini hata hivyo, Nkrumah naye hakupona katika vuguvugu la mapinduzi ya kijeshi yaliyosham­iri barani Afrika. Alipinduli­wa miaka miwili baadaye.

Licha ya kufanya juhudi kutuliza maasi, bado watu wengi hadi leo wanadai Oscar Kambona yeye ndiye aliyeyasab­abisha kwani akiwa Waziri wa Ulinzi alikuwa akitoa ahadi za kuboresha maisha ya wanajeshi bila kutimiza, anatuhumiw­a kuwaingiza jeshini vijana wa TANU (TANU-Youth League) ambapo inadaiwa waliingia bila kufuata utaratibu.

Hata hivyo, katika majadilian­o kati ya Waziri Kambona na waasi, walikubali­na kuongezwa mishahara kutoka shillingi 105 hadi shillingi 150 kwa mwezi, ingawaje waasi walikuwa wakitaka ufike hadi shilingi 260 kwa mwezi.

Hata hivyo, baada ya kuzimwa kwa maasi, Mwalimu alifanya marekebish­o makubwa na kuimarisha Kitengo cha Intelejens­ia ili kuweza kuzuia kupinduliw­a. Nyerere atofautian­a na Kambona Katika kuelekea kujenga Tanzania ya Kijamaa, hapo ndipo Nyerere na Kambona walikuja kutofautia­na. Kambona alikuwa haamini Sera za Ujamaa na alimpinga Nyerere waziwazi—kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri yeye pamoja na aliyekuwa Waziri wa Katiba, Abdallah Said Fundikira III ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Nyerere tangu wakiwa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Kambona alitaka Tanzania itenge baadhi ya maeneo ambayo yatakuwa kama mfano, ambapo kungeundwa Vijiji vya Ujamaa vya mfano kuliko kuwa na Vijijini vya Ujamaa nchi nzima. Hivyo Kambona na Fundikira walipinga mpango wa Nyerere na Kawawa ambao walitaka nchi nzima iwe na Vijiji vya Ujamaa.

Hivyo hadi Azimio la Arusha linatangaz­wa Februari 5, 1967, mawaziri hao wawili hawakuunga mkono. Waziri Fundikira III akaachia ngazi huku Kambona akisalia, lakini kishingo upande.

Mwezi Julai 1967, Kambona aliichukua familia yake na kukimbilia Kenya na baadaye Uingereza.

Waliokuwa wanamuunga mkono wanadai alikwenda uhamishoni baada ya kuwa kupata vitisho kwa kupinga Sera za Ujamaa, lakini upande wa Serikali walidai kuwa alikimbili­a Uingereza kwa madai kuwa mpango wake wa kutaka kumpindua Rais Nyerere ‘ulivuja’.

Katika tuhuma hizo, walio dai kuwa washirika wa Kambona katika mpango huo walikamatw­a na kushitakiw­a kwa kosa la uhaini mbele ya Jaji Mkuu Phillip Telfer Georges aliyekuwa na asili ya Trinidad and Tobago, huku upande wa serikali ukiongozwa na Mwanasheri­a Mkuu Mark Bomani.

Shahidi namba moja wa kesi hiyo alikuwa ni Potlako Leballo, aliyekuwa Rais wa PAC (Pan Africanist Congress) cha Afrika Kusini ambacho kilikuwa na ofisi Dar es Salaam baada ya kupigwa maarufu Afrika Kusini na Rais wake, Robert Sobukwe, kufungwa jela.

Mnamo Juni 14, 1968 Kambona akiwa Nigeria, kwa mwaliko wa Rais Yakubu Gowon, alimtuhumu Nyerere, kuwa yeye na Kawawa walijilimb­ikizia pesa nyingi akijibu tuhuma dhidi yake zilizotole­wa na Nyerere mnamo Januari 12, 1968 akidai kuwa Kambona alikuwa na pesa nyingi kuliko mshahara wake na akafika kuwa aliiba fedha za Kamati ya Ukombozi ya OAU ambayo kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wake.

Pia Kambona alisema Nyerere ni dikteta na alikuwa akichukua silaha za ZAPU (Zimbabwe African People’s Union) na kuwapa waasi wa Biafra iliyojiten­ga kutoka Shirikisho la Nigeria. Nyerere alisahau mchango wa Nigeria alioupata mwaaka 1964 na kuinga mkono Biafra.

Pia Kambona alidai Nyerere hakuwa Mtanzania, bali ni Mnyarwanda na Kawawa alikuwa mkimbizi kutoka Msumbiji na John Malecela ni Mkongo.

Serikali ya Tanzania ilimnyang’anya hati ya kusafiria kwa madai kuwa Kambona hakuwa Mtanzania, alikuwa raia wa Malawi, lakini alirejeshe­wa baada ya watu wengi kuhoji mbona Kambona alipigania Uhuru na kupewa nafasi mbalimbali za uwaziri.

Hata hivyo ripoti za shirika la Kijajusi la Marekani (CIA) za mwaka 2015 zinadai kuwa Kambona alitaka kumpindua Nyerere na aliomba msaada, lakini CIA walikataa kwa sababu Mwalimu Nyerere alikuwa sio mla ‘rushwa’ na alikuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kimataifa.

Hivyo CIA walimshaur­i kuwa kama Kambona alitaka kumpindua Nyerere alitakiwa aunde vikundi katika makambi ya wapigania uhuru, ili wampe silaha ndipo ampindue Nyerere.

Hata hivyo, Kambona aliishi Uingereza kwa takribani miaka 25, alirejea nchini mwaka 1992, baada ya mfumo wa vyama vingi na alikuja kuunda Chama cha TADEA ambacho hata hivyo hakuwa tena na ushawishi na hakufua dafu katika siasa za miaka 1990.

Oscar Kambona katika siku zake za mwisho aliishi kwa shida hadi umauti ulipomkuta Novemba 1997 alikuwa na hali dhoofu.

Mwalimu Nyerere

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.