Tufiche wapi sura yetu kimataifa?

Rai - - MAONI/KATUNI -

TUKIO la kutekwa bilionea Mohamed Dewji limeleta sura hasi kwa Tanzania katika anga za kimataifa. Ni taswira ambayo inaleta hasara kubwa zaidi kwa nchi yetu kupitia sekta mbalimbali.

Kwa msomaji mzuri wa mitandao makini na taarifa za mashirika ya habari ya kimataifa, kuanzia barani Asia hadi Ulaya,

kuelekea Amerika kaskazini hadi Amerika kusini, sura yetu ni mbaya.

Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuripoti tukio hilo (sisemi wasiwe mstari wa mbele, kwakuwa wanastahil­i na tukio limetokea kweli), ambalo linaleta madhara kwetu kwa namna mbalimbali kutokana na hali yenyewe ilivyojito­keza.

Kuanzia vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa hadi vidogo, pamoja na mitandao wa kijamii kote duniani, habari juu ya Tanzania hazipednez­i. Kama tutajidang­anya kuwa “sifa yetu” haijachafu­liwa ni sawa na kujaribu kupiga mluzi huku tukitafuna karantga mbichi. Ni kujilisha upepo tu.

Ni dhahiri Tanzania imekuwa midomoni mwa Jumuiya ya kimataifa kwa mtazamo hasi juu ya utekwaji wa watu, likiwemo tukio la Mohamed Dewji.

Kuanzia

walipopote­a akina Azory Gwanda, na Ben Saanane hadi kifo cha mtetezi maarufu wa tembo duniani Wayne Lotter, na kushambuli­wa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu hadi kutekwa kwa Mohamed Dewji kumeleta taswira hasi kupindukia.

Vyombo vikuu vya habari duniani kama vile Aanzia CNN, BBC,DW, Reuters,Al Jazeera, Xinhua, Times Now,Fox News na mengine mengi. Ukifungua mtandao wa Google, kisha ukaandika majina mawili, kwa mfano “Tanzania” ama “Young African billionair­e” unaweza kuletewa matokeo ya habari zaidi ya 200 kutoka mashirika ya habari duniani kuhusiana na utekwaji wa Mo Dewji. Natambua kuwa yeye ni ‘Trending’ kwa sasa, lakini tunatrendi kwenye mambo yanayohari­bu taswira ya nchi na kuongeza mkanganyik­o.

Popote unapoandik­a jina la ‘Mohammed Dewji au Mo Dewji” kinacholet­wa mbele yako ni habari hasi yaani mbaya zaidi katika taifa letu. Habari ambazo zinazidish­a vurumai katika tafakuri zetu za kulijenga taifa hili.

Anzia The Guardian, Daily Mail, Mirror, Mail and Guardian, Sowetan, NewsDay, Asia Times, New York Times, Foreign Policy, The Elephant, The Hill, DW, RFI, Pars Today, VOA, Daily Monitor, Forbes, New York Post, The Telegraph, Venturs Africa kwa kutaja chache.

Twende kwenye taasisi za elimu, biashara na uchumi, watu binafsi, viongozi nba kadhalika, wote wanaitazam­a Tanzania kwa jicho hasi juu ya usalama wa watu wake pamoja na uwekezaji.

Tukio hilo linasikiti­sha kama yalivyotok­ea mengine huko nyuma, na ambayo hayakuwa na chochote zaidi ya kuharibu wasifu wan chi yetu.

Ni matukio ambayo yanasababi­sha hasara kwa uwekezaji, uchumi na biashara,ulinzi na siasa. Ni taswira hasi kwakuwa inatafsiri­wa kama vile Tanzania kuwa sehemu mbaya ya wawekezaji kuendesha shughuli zao kwa sababu ulinzi utakuwa mdogo kwa wawekezaji.

Watu wavivu wanaweza kusema kuwa “na hili nalo litapita”, lakini wanasahau kuwa madhara ya matendo kama hayo huwa yanatokea taratibu na yanadumu kwa muda mrefu pamoja na kuharibu taswira ya nchi na jamii yake.

Nina uhakika iwapo mtandao wa Google utaamua kutoa taarifa za takwimu za watu waliotafut­a taarifa za Tanzania mtandaoni ifikapo mwisho wa mwezi Oktoba mwaka huu, jawabu litakuwa ni taswira hasi juu ya kutekwa kwa Mohamed Dewji.

Sishabikii utekaji wala simtuhumu mtu awaye yeyote lakini mazingira tuliyo nayo kwa sasa hatuwezi kujidangan­ya kuwa mambo yatajiongo­za yenyewe. Ni lazima tukiri kuwa kupotea na kutekwa watu kunajenga taswira mbaya mno kimataifa na hata ndani ya nchi yetu.

Taswira hiyo ni ile kuwa kiwango chetu cha ulinzi kimedorora kiasi kwamba hawa wahuni na wahalifu wanaweza kutamba. Hii sio sawa.

Ni muhimu kukemea kwa nguvu na kukumbusha wenye mamlaka ya nchi hii kuwa wanao wajibu wa kuwalinda na kutulindia dola yetu kwa nguvu na maarifa yao.

Nihitimish­e kwa kusema kuwa matukio kama haya yanaitaka serikali yetu kuwa msemaji mmoja pekee. Hatutaraji­i kuona wasemaji wa tukio hilo, mara ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, mara wasaidizi wa IGP, mara sijui nani na nani.

Tukiruhusu kila mmoja kutoka serikalini kuwa msemaji wa tukio la utekaji wa Mohamed Dewji tunajianik­a utupu na kuonyesha mambo yamekuwa shaghalaba­ghala.

Ni lazima wenye fani zao za ushuhushu, ujasusi waachwe wafanye kazi yao kwa ufanisi. Ni lazima kuwaachia wenye fani nzao wahakikish­e wanatoa taarifa iliyoruhus­iwa (kuidhinish­wa), lakini kujifanya kila mmoja aonekane mbele ya kamera za vyombo vya habari ni uzembe na kuruhusu mambo ya ovyo.

Kwa sababu tulilonalo hadi sasa ni kubwa, kwamba taswira ya Tanzania kimataifa sio nzuri. Mtu mwenye soni atakuwa anatembea huku na huko na kujiuliza, ‘tutaweka sura ya nchi yetu katika anga za kimataifa? Inasikitis­ha, na aibu kwa kweli.

Mwisho nawakumbus­ha watawala wetu. Kuwekwa kamera za CCTV kwenye miji yetu mikubwa ni suala la lazima. Teknolojia inatuletea mbinu nyingine za kufanya mambo hasi ambayo kwa namna moja au nyingine changamoto kwa walinda nchi yetu.

Ni wajibu wetu kuangalia suala la CCTV kwenye kila kona za barabara kubwa na ndogo zinawekwa. Ni watu wetu kama nchi kutambua kuwa suala la teknolojia ni nyeti na ambalo linatakiwa kufanya kazi tutake au tusitake. Teknolojia inatulazim­isha hilo.

Ni jambo la kushangaza unaona barabara kubwa nchi hii hazina CCTV, na kwamba inasababis­ha ‘wahuni’ au watekaji waliobobea kuzidi kujiimaris­ha kwa kuwa wanafahamu bado tuna mawazo ya kizamani ya ‘enzi za ukabaila ama ujima na zama za Kati za mawe ambazo zilikuwa gizani.

Vilevile, je mifumo yetu ya ulinzi katika Hoteli kubwa za nyota unakidhi mahitaji ya kisasa ama tunaweka walinzi tu getini wakiwa wameshikil­ia “gobore”?

Nina matumaini Mohamed Dewji atakuwa salama. Namwombea kama wengine waliotekwa au kupotea katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.