Waziri Lukuvi na zigo la kaya 100 Tegeta

Rai - - MAONI/KATUNI - NA MWANDISHI WETU

KAYA zaidi ya 100 katika eneo la Tegeta A, Goba – wilayani Ubungo jijini Dar es

Salaam, wamemuomba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aingilie kati mgogoro wa ardhi uliodumua kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Wakizungumza na RAI hivi karibuni, wananchi hao wamesema ikiwa mamlaka zinazohusika hazitaingilia kati mgogoro huo, makazi yao yatakuwa shakani kwa kile walichoeleza, kuna dalili za ukandamizwaji wa haki na sheria za nchi.

Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya maandamano ya amani katika eneo hilo, wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe wa wazi kwa viongozi wa Serikali akiwemo Rais Dk. John Magufuli, wakazi hao wamesema hadi juzi, nyumba 48 zimeandikwa makatazo yanayowaataka wasiendeleze ujenzi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mwafaka wa Viwanja hivyo, Venance Mpihigwa alisema walipigwa na butwaa baada ya kukuta nyumba zao zikiwa zimetakiwa kubomolewa huku nyingine zikiandikwa zisimamishwe ujenzi.

Alisema, awali eneo hilo lilikuwa na mgogoro kati ya wananchi na familia ya mtu aitwaye Seif Ngane lakini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori alifika na kuumaliza mgogoro huo kisha kuwaamuru wananchi kuendelea kujenga kwa kuwa walikuwa na uhalali wa umiliki.

“Mpaka sasa nyumba 48 zimeshaandikwa zisimamishe ujenzi, lakini nyumba ni nyingi sana. Ni nyumba zaidi ya 100. Unajua sisi tuko eneo hili kihalali, na tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye kuna wakati alifika eneo la tukio ikiwepo familia ya Ngane iliyokuwa ikidai eneo hilo ni lao lakini mwisho wa siku, kwa vielelezo tulivyonavyo, aliamuru wananchi waendeleze makazi hayo.

“Cha ajabu sasa kuna watu kutoka Manispaa ya Ubungo ambao bado wamekuwa wakituletea usumbufu akiwemo Kamishna Mteule wa Ardhi Wilaya yai Ubungo, bwana Edward Mrando. Usumbufu huo ulitulazimu tufanye jitihada za kutaka kumuona Waziri Lukuvi ili ajue kwamba kuna watendaji wake huku chini wanasumbua raia,” alisema Mpihigwa.

Alisema, wakati wakiwa katika harakati za kutafuta namna ya kumfikia Waziri Lukuvi, wakashangaa gari likiwa na watu wapatao nane na askari wawili, wakifika katika eneo hilo na kuanza kuandika nyumba zao SIMAMISHA UJENZI.

“Tumeshangaa kuona watu wamefika kwenye eneo letu na kuanza kuandika nyumba zetu zisiendelezwe ujenzi, nyingine zibomolewe. Ni jambo la kushangaza, maana sisi tuna vibali vyote halali vya kukaa hapa.

“Tunajiuliza maswali mengi bila majibu; hivi inawezekana vipi mtu au familia moja imiliki eneo la zaidi ya ekari 100 jijini Dar es Salaam? Siku zote hao watu walikuwa wapi, hadi tumenunua, kujenga na wengine tayari tunaishi hapa? Tunamuomba sana Waziri Lukuvi asikie kilio chetu aje atusikilize,” alisema Mpihigwa.

Katika kutafuta uhalali wa watu hao waliofika kwenye maeneo yao na kuyawekea makatazo, Mpihigwa anasema walifika manispaa kuuliza kama watu hao walipewa baraka huko, lakini hawakupewa majibu yanayoeleweka.

Mkazi wa eneo hilo, Benitho Chiwinga ambaye nyumba yake imeandikwa ‘SIMAMISHA UJENZI’ huku akiwa tayari anaishi katika nyumba hiyo, alisema anashangazwa kuona mambo yanafanyika kienyeji bila kufuata utaratibu.

“Kuna mambo ya ajabu sana yanafanyika huku na ni vyema Lukuvi akajua. Hivi from no where unakuta nyumba ambayo umeihangaikia kwa muda mrefu, leo anakuja mtu na kuandika bomoa kienyeji tu, haya yanawezaje kufanyika kwenye nchi hii inayoongozwa na Rais anayejipambanua kututetea wanyonge? Lukuvi njoo Tegeta A, Kulangwa. Watendaji wa Manispaa ya Ubungo wanakuharibia kazi,” alisema Chiwinga.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Godwine Msosi alisema anaamini Ngane ameingia tamaa na kuamua kushirikiana na baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Ubungo wasio waaminifu ili kuwatisha wananchi hao wajipatie fedha.

“Unajua huyu bwana Ngane alikuwa na

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.