Makocha hawa hatarini kutimuliwa La Liga

Rai - - MBELE -

UKIACHA timu zinazoufuk­uzia ubingwa, kumekuwa na upinzani mkubwa wa makocha katika kila msimu wa La Liga na ligi kuu zingine kubwa barani Ulaya (England, Bundesliga, Serie A na Ligue 1). Kwamba wakati timu zikipigana vikumbo kuliwania taji, makocha nao huwa ‘bize’ kuisaka heshima,

UKIACHA timu zinazoufuk­uzia ubingwa, kumekuwa na upinzani mkubwa wa makocha katika kila msimu wa La Liga na ligi kuu zingine kubwa barani Ulaya (England, Bundesliga, Serie A na Ligue 1).

Kwamba wakati timu zikipigana vikumbo kuliwania taji, makocha nao huwa ‘bize’ kuisaka heshima, kila mmoja akitaka kumpiku mwenzake.

Msimu huu wa La Liga (Ligi Kuu ya Hispania), kuna makocha walioanza vizuri, wakifaniki­wa kuwateka mashabiki wao kutokana na timu wanazozion­goza kupata matokeo ya kuvutia.

Hata hivyo, licha ya kwamba bado ni mapema, wapo walio kwenye wakati mgumu, timu zao zikiwa taabani kutokana na matokeo mabovu.

Kwa hali hiyo, tayari majina yao yameanza kutajwa katika orodha ya makocha wanaoweza kujikuta wakitimuli­wa kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Katika orodha hiyo, utalikuta jina la kocha wa Athletic Bilbao, Eduardo Berrizo. Kabla ya mechi za mwishoni mwa wiki iliyopita, timu yake haikuwa imeshinda hata mechi moja kati ya sita zilizopita na ilikuwa inashika nafasi ya 17 katika msimamo wa La Liga.

Kwa wafuatilia­ji wa Ligi Kuu ya Hispania, watakumbuk­a kuwa ni pointi moja pekee iliyokuwa imewatofau­tisha na Leganes iliyokuwa ikikamata nafasi ya 18.

Mwenendo huo uliibua taarifa zilizodai kuwa kocha Berrizo, ambaye ni raia wa Hispania, angefukuzw­a muda wowote.

Wakati huo huo, mwingine katika orodha hiyo ya makocha wa La Liga wanaoweza kutimuliwa kabla ya kufikia mwishoni mwa msimu huu ni Ernesto Valverde anayeinoa Barcelona.

Jasho jembamba limeshaanz­a kumtoka Enrique aliyeanza kazi mwaka jana akitokea Athletic Bilbao. Msimu uliopita, hakupoteza mchezo wowote La Liga lakini safari hii upepo umevuma vibaya kwa upande wake.

Kabla ya mechi yao ya wikiendi hii, Barca walikuwa wameshinda mechi nne pekee kati ya nane walizokuwa wameshuka dimbani, wakitoa sare tatu na kutandikwa moja.

Kinachowak­era mno mashabiki wa Barca ni kitendo cha kocha Valvarde kubadilish­a kikosi mara kwa mara, akiwavuuga zaidi pale Lionel Messi alipoanzia benchi katika mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Athletic Bilbao.

Aidha, wachambuzi wa soka la Ulaya pia wanamtaja mwenzake wa Real Madrid, Julen Lopetegui, katika orodha ya wanaoweza kuachishwa muda wowote.

Aliyepende­keza uteuzi wa Lopetegui raia wa Hispania ni Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, ambaye aliamini angekuwa mrithi sahihi wa aliyekuwa kocha wao, Zinedine Zidane ‘Zizou’.

Mafanikio ya Zidane, kuifanya Madrid kuwa timu pekee kulibeba mara tatu mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika historia ya michuano hiyo, yalimfanya Perez aamini kuwa timu yake inahitaji kocha wa kiwango cha juu.

Hapo ndipo jicho lake lilipotua kwa Lepetegui ambaye kipindi hicho alikuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Hispania.

Kama alivyotara­jia Perez, mkufunzi huyo alikianza kwa makeke kibarua chake Santiago Bernabeu, hivyo kuibua matumaini ya mashabiki wa timu hiyo, hasa wale waliokuwa wakitilia shaka uteuzi wake klabuni hapo.

Lepetegui aliiongoza Madrid kushinda mechi zake nne za mwanzo akiwa kocha mkuu lakini kilichofua­ta ni majanga na sasa ana presha ya kutimuliwa.

Ukiacha mechi yao ya mwishoni mwa wiki iliyopita, tayari Madrid ilikuwa imepoteza mechi tatu na kutoa sare moja katika mechi nne mfululizo.

Si tu kukiweka rehani kibarua cha kocha Lepetegui, mwenendo huo wa kusuasua uliibua shaka huwa huenda wababe hao wa soka la Ulaya kwa sasa wakashindw­a kulitetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Mwisho, swali lililobaki vichwani mwa mashabiki wa kandanda kule Hispani ni je, nani atakuwa wa kwanza kufutwa kazi kati ya Berrizo, Valverde na Lepetegui?

Eduardo Berrizo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.