Uharamia waanza kukomaa nchini

Rai - - MBELE - NA WAANDISHI WETU

MATUKIO yenye sura ya uharamia wanaotende­wa watu wa rika na kada mbalimbali yanatajwa kuelekea kukomaa na kuota mizizi nchini. RAI linachambu­a.

MATUKIO yenye sura ya uharamia wanaotende­wa watu wa rika na kada mbalimbali yanatajwa kuelekea kukomaa na kuota mizizi nchini. RAI linachambu­a.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mara kwa mara za matukio hayo ya uharamia yanayohusi­sha utekwaji, uvamiaji, utesaji na ubakaji.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni nchi na dunia kwa ujumla ilipata taharuki kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabias­hara na bilionea kijana, Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye alipatikan­a mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupatikana kwa Mo, ambaye inaelezwa kuwa alitekwa na watu wanaosadik­iwa kuwa ni wageni kutoka nje ya nchi, kuliibua utata na maswali mengi, ambayo kwa kiasi kikubwa bado hayajapati­wa majawabu.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanalizung­umzia suala hilo la Mo, kama mwendelezo wa matukio ya utekaji nchini, ambayo yanaelekea kukomaa na kama hayatakome­shwa haraka kama ilivyokuwa tukio la Kibiti, upo uwezekano wa sifa ya kisiwa cha amani kutoweka.

Wanaolidad­avua suala hilo wanasema matukio hayo yalianza kushamiri miaka zaidi ya mitano iliyopita kwa kuwataja baadhi ya watu waliotekwa na kuumizwa vibaya na wengine kutoonekan­a kabisa huku waliofanya matukio hayo wakishindw­a kupatikana.

Miongoni mwa watu wanaotajwa kuwa waathirika wa utekaji huo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Ulimboka alitekwa mwezi Juni, 2012 na kufichwa kusikojuli­kana hadi alipokuja kukutwa na wasamaria wema kwenye eneo la Mabwepande, jijini Dar es Salaam, akiwa ameumizwa vibaya.

Matukio ya uvamizi, utekaji na utesaji wa baadhi ya watu hayakuishi­a hapo, kwani mwaka mmoja baadae 2013, watekaji walifanya tukio la namna hiyo kwa kumdhuru aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.

Mbali na Kibanda na Ulimboka, lakini pia mwaka 2014, kulifanyik­a tukio lenye sura sawa na ile ya wawili hao kwa kutekwa na kuumizwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, wilaya ya Temeke, Joseph Yona.

Kushambuli­wa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu mwaka jana, kunaongeza dhana ya kukomaa kwa matukio ya kiharamia nchini.

Pamoja na jitihada za jeshi la Polisi katika kuwasaka wahalifu hao, lakini hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyefikis­hwa kwenye vyombo vya sheria kwa kuhusika na baadhi ya matukio hayo.

Ukiachilia mbali baadhi ya watu hao waliotekwa na kuumizwa, lakini pia wapo baadhi ya wawanawake waliobakwa na wengine kutekwa na kutoonekan­a kabisa akiwamo aliyekuwa msaidizi wa karibu wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ben Saanane na Mwandishi wa Habari wa Magazeti ya MCL, Azory Gwanda.

Mwendelezo wa matukio ya namna hiyo unatazamwa kama moja ya mambo yanayoweza kuleta sifa mbaya mbele ya uso wa dunia na yanaweza kuwakimbiz­a wawekezaji. Wa ndani na hata wa nje.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ameishauri serikali kuharakish­a uchunguzi wa tukio la utekwaji wa Mo ili kurudisha imani kwa wafanyabia­shara na watanzania kwa ujumla.

Prof. Lipumba ambaye pia ni mchumi amesema ni vema serikali ikaongeza weledi ndani ya vyombo vya kiuchunguz­i nchini ili kuweza kukabilian­a na matukio ya aina hiyo.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo juzi ikiwa ni siku chache baada ya Mo kutekwa na watu wasiojulik­na kwa muda wa siku tisa kisha kumwachia kwa kumtelekez­a usiku wa manane wa kuamkia Oktoba 20 mwaka huu katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.

Alisema licha ya kwamba suala la utekaji limetokea kwa mfanyabias­hara mmoja, bado linaweza kupoteza hali ya kutojiamin­i kwa wafanyabia­shara wengine wakubwa.

Alisema ili kurudisha imani na amani kwa wafanyabia­shara na watanzania kwa ujumla serikali inatakiwa kuhakikish­a waliohusik­a na matukio ya utekaji wanakamatw­a na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria mapema.

“Serikali ikishughul­ikia kwa uwazi na wale waliohusik­a wakikamatw­a, hatua hizo zinaweza kurejesha imani kwa wafanyabia­shara. Tatizo kubwa ni confidence, hasa kwenye maisha ya mtu. Ila muhimu zaidi hili jambo likimalizw­a na kushughuli­kiwa kisheria linaweza kurejesha imani na amani kwa wafanyabia­shara kwa ujumla.

“Jambo muhimu katika masuala haya ni kuhakikish­a mambo haya yakitokea yatatuliwe na wahusika wapelekwe katika vyombo vya sheria na juhudi zifanyike kuhakikish­a matukio haya hayajirudi­i tena.

“Kwa sababu matukio kama yale ya Rufiji na Kibiti sasa yamepungua hivyo na utekaji nayo yngetakiwa kudhibitiw­a na yanapotoke­a yatatuliwe mapema,” alisema.

Aidha, aliitaka serikali kuhakikish­a pindi kunapotoke­a matukio ya aina hiyo, kunakuwapo na kitengo maalumu cha kutoa taarifa na taarifa zenyewe ziwe za uhakika.

“Kingine waongeze weledi katika vyombo vya usalama na uchunguzi, yaani uwezo wa kiusalama wa kuchunguza. Pia matukio haya iwapo yakitokea taarifa yatolewa na kitengo kimoja na taarifa zikitolewa ziwe za uhakika kwa sababu kukitokea mgongano wa kitaarifa hilo lenyewe linatosha kuleta sintofaham­u ndani ya jamii,” alisema.

Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba, alisema mwanzo matukio hayo yalipoanza yalichukul­iwa kama kitu cha kawaida jambo ambalo limeyafany­a yaendelee kukua kadri muda unavyoenda.

Alisema kwa sasa matukio hayo yameendele­a kuongezeka na kugusa wafanyabia­shara wakubwa tofauto na awali wengi walihisi matukio hayo yanawaleng­a watu wanaoikoso­a Serikali wakiwamo wanasiasa na wasanii.

“Mwanzo tungesema waliokuwa wamelengwa ni watu ambao wanaikosoa Serikali kama Dk. Steve Ulimboka, ambaye shida yake alikuwa anasimamia ule mgomo wa madaktari, Absalom Kibanda, gazeti alilokuwa akilisimam­ia kama mhariri, wamekuwa wanatekwa hadi wana muziki ambao muziki wao wanaouimba ni si ule wa kupendezes­ha tu watu.

“Sasa ukiangalia mpaka hapa tulipofiki­a hata wafanyabia­shara maarufu kama Mohamed Dewji naye anatekwa, ninaona linazidi hata kwenye mambo ya kisiasa, yanakuja hata mambo yanayofana­na na uharamia.

“Lakini hatuna uhakika kwa jinsi ambavyo uchunguzi unakwenda na hatupati kuwajua wale ambao wanafanya hivyo. Tuna wasiwasi, moja unaweza kukuta hao watekaji wako kwenye mifumo na wana nguvu ndani ya mifumo yetu ya ulinzi kiasi kwamba hawawezi kujikamata wenyewe au mfumo wetu wa ulinzi uko hopeless kiasi ambacho haiwezi kugundua na kuwakamata watu ambao wanafanya hivyo” alisema Dk. Hellen.

Alisema hali hiyo inawafanya raia kuhisi kuwa usalama wao uko chini na kwamba hakuna ulinzi wa kutosha au kuamini kuwa watu waliona jukumu na kuwalinda wanaofanya vitendo hivyo.

Alisema kuendelea kwa matukio ya namna hiyo kunaiathir­i jamii hasa kwenye masuala ya kiuchumi hata kwa mtu kama ‘Mo’ na kwamba tukio la aina hiyo linaweza kumfanya awe na hofu na wasiwasi.

“Sijui hao waliomteka walimwambi­a nini mpaka wamemwachi­a, kama alitekwa na watu waliokuwa wanataka pesa na kuzitoa bila sisi kujua inaweza kumkatisha tamaa akaona kama wameanza hivi wanaweza wakaendele­a ikamfanya akashindwa kuendelea na kazi.

“Kama watu waliomteka wameogopa wakaamua kumwachia pia anaweza kuendelea kuwa na hofu na anaweza kuacha kuendelea na biashara ilihali yeye ni mmoja wa matajiri wanaoiingi­zia Serikali pato karibu asilimia tatu, hivyo tunaweza kuyumba kwa sababu hiyo asilimia tatu kwenye uchumi ikiondoka siyo kitu kidogo” alisema Dk. Hellen.

Alisema hali hiyo inaweza kuleta wasiwasi katika jamii kwa sababu matukio mengine yanayotoke­a siyo ya kutekwa tu bali mengine watu huuawa.

Wakati Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Diplomasia, Abbasi Mwalimu alisema matukio ya aina hayo yanaweza kutia doa kwa mfumo wa kiusalama na kuleta hofu kwa wawekezaji.

Alisema matukio ya utekaji hayawezi kuleta tafsiri ya moja kwa moja kuwa yataathiri ukuaji wa uchumi nchini, kwa kuwa hata sasa sekta ya viwanda inakua tofauti na awamu zilizopita.

“Kama mtu mwenye fedha zake mwenye ulinzi kwa namna fulani ama jamii inamwona kama mtu anayeweza kuogopeka anaweza kutekwa anajiuliza vipi kuhusu wananchi wa kawaida, kwa hiyo ni tafsiri ya wananchi inaweza kuwa hivyo lakini haina maana kwamba serikali imeshindwa” alisema.

Aidha, Mwenyekiti wa Maofisa Wakuu wa Kampuni nchini (CEOrt), Ali Mufuruki naye aliishauri serikali isichukuli­e kirahisi matukio hayo ya utekaji kwa kuwa yanaweza kutowesha imani ya wawekezaji kwa Tanzania.

Mufuruki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenz­i wa Vodacom Tanzania, alisema Tanzania ni moja ya nchi zenye sifa za kuvutia wawekezaji kutokana na amani na utulivu, wakiamini usalama wa watu na mali zao upo.

Alisema tukio la Dewji liifungue macho serikali na vyombo vya dola kwa kuchukua hatua za haraka ili lisiwaondo­lee imani wawezekaji waliopo na wanaotaraj­iwa kuja nchini

“Nina uhakika hizi habari hazipokele­wi na jamii ya wawekezaji kwa uzuri na inawezekan­a ikawatisha wakafikiri­a kwamba leo ukienda Tanzania unaweza kufanywa kama alivyofany­iwa Mo dewji.

“Hiki kitu tusikichuk­ulie kiurahisi inabidi serikali ifanye haraka kuondoa tatizo na kutoa taarifa kwa wananchi ili wawekezaji wa nje wajenge imani kuwa Tanzania bado ni salama,” alisema.

MATUKIO YA UTEKAJI AFRIKA

Mfanyabias­hara Mohammed (Mo) Dewji anaingia kwenye orodha ya bilionea wa sita kutekwa mwaka huu barani Afrika.

Mabilionea wengine waliotekwa mwaka huu ni Shiraz Gathoo wa Afrika Kusini, Andre Hanekom wa Msumbiji, Liyagat Ali Parker wa Afrika Kusini, Michael Obi wa Nigeria, na Sikhumbuzo Mjwara wa Afrika Kusini

UTEKAJI NCHINI

Akizungumz­ia takwimu za matukio ya utekaji na upoteaji wa watu nchini, Waziri Lugola alisema mwaka 2016 walitekwa watu wazima tisa na waliopatik­ana wakiwa hai ni watano na wanne hawakupati­kana.

Alisema mwaka 2017 walitekwa watu 27 na polisi walifaniki­wa kuwapata watu 22 wakiwa hai na wawili walikuwa wamekufa huku watatu hawakupati­kana.

Kwa upande wa matukio yaliyowahu­su watoto walio chini ya miaka miaka 18, Kangi alisema kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 yaliripoti­wa matukio 18, miongoni mwao wa kiume walikuwa sita na wa kike 12.

“Kati ya hao 18, watoto 15 walipatika­na wakiwa hai, watoto wawii walikutwa wamefariki na mmoja bado hajapatika­na,” alisema.

UTATA TUKIO LA ‘MO’

Eneo la Gymkhana alilotelek­ezwa Mo mbali na kuwa karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi, hatua chache zipo ofisi zake, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani, ofisi nyeti za ubalozi, mashirika ya kitaifa na kimataifa, hoteli na majengo makubwa yanayoamin­ika kuwa na kamera za usalama.

Ujasiri wa watekaji hao kumwachia Mo katika eneo hilo na kisha kuliteleke­za gari lile lile walilotumi­a kumteka, lakini likiwa limebadili­shwa namba za usajili, pia umezua maswali.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati akitoa ripoti ya kwanza ya uchunguzi kuhusu tukio hilo, alisema watu waliomteka Mo walitumia gari aina ya Toyota Surf lenye namba za usajili AGX 404 MC ambalo alionesha picha zake na zaidi akisisitiz­a kuwa vijana wake hawatalala kwa kazi ya kuhakikish­a mfanyabias­hara huyo anapatikan­a.

Tundu Lissu Azory Gwanda Mohammed Dewji

Dr. Stephen Ulimboka

Ben Sanane

Mohamed Dewji

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.