WABUNGE WA UPINZANI, CCM HAWAAMINIK­I

Rai - - MBELE - NA ERICK SHIGONGO

CONFIANZA’ ni neno kutoka Latini Amerika. Neno hili hutumiwa sana na raia wa Colombia wakimaanis­ha imani yao kwa serikali iliyopo madarakani.

Kwa lugha ya kimombo neno Confianza ni ‘confidence or trust in the government ability to fulfill its duties and increase general sense’. Raia wa Colombia wanachofan­ya ni kuiamini serikali au katika harakati zake za kuleta misingi ya maendeleo yao na kukuza uchumi wa wa nchi yao. Kitendo hicho cha kuiamini serikali yao huita ‘confianza’.

Hiki ni kitu ambacho lazima kifanyike na njia sahihi na ‘confianza’ ni kujitambua na kutambua kisha kuthibitis­ha mwenyewe serikali inasikia na inasikiliz­a pamoja na kuwa na watendaji wenye uwezo na wasio na mawaa. Kwamba serikali inafahamu na inakosea, kwani wanaounda serikali ni watu ambao wanatoka katika jamii yetu.

Kwahiyo ukilichang­anua neno ‘confianza’ kulingana na jamii yetu ambayo inazalisha viongozi wa serikali, kwamba mahusiano baina ya mtu na mtu yanafaniki­sha kazi nzuri inayojenga jamii bora. Mahusiano baina ya wananchi na serikali yao, maana huwezi kuwatenga watu na serikali kwani serikali ni watu na watu hao ndiyo serikali.

Mahusiano ya watu na serikali ni sawa na mahusiano ya watu ndani ya jamii yao. ‘Confianza’ linatawala maisha ya watu Latini Amerika tangu siasa, uchumi, tamaduni na jamii kwa ujumla. Kwahiyo tukichukua mfano wa ulinzi shirikishi kwa jeshi la Polisi nchini mwetu na wananchi unapaswa kuzingatia ‘confianza’ baina yao kama sehemu ya serikali na wananchi.

Hii ni imani kubwa juu ya utendaji kazi wa taasisi ama asasi yoyote ya serikali yenye makusudio ya kuhudumia wananchi ndani ya nchi yao. Kwa mfano nchini Dominica husema ‘tengo confianza’ kwa imani juu ya mtu au mtumishi wa umma inatokana na mahusiano yao ya kikazi na kijamii.

Kwamba kila jambo hufanywa kwa uaminifu na taratibu ambazo zinamfanya mwingine aamini utendaji wake, aamini uwepo wake na usalama wake. Lakini kama mtu anakuwa tofauti na kutoiamini serikali yake, raia hao husema ‘abuso de confianza’ yaani kutoaminia­na ama kukosa imani na serikali ama mtu Fulani wakiwemo wabunge .

Katika milipuko ya kisiasa kumekuwa na mambo mengi yenye kuonyesha ‘confianza’ au ‘abuso de confianza’. Matendo yote haya yanatokana na mitazamo ndani ya jamii zetu. Wakati mwingine matendo yanapozidi kete ukweli ni uharibifu. Hata kama tunaamini serikali inatakiwa kukubalian­a na matakwa yetu, ni lazima tufahamu kuwa serikali hiyo ni watu, inasikia, inasikiliz­a, inaona, inawaona,inawapenda, inapendwa, inaheshimu, inaheshimu na kadhalika.

Aidha, huwezi kuwa na chama cha siasa imara ambacho wabunge wake wanaaminik­a kuhongwa, kulaghaiwa na upande wa utawala. Kauli na matendo yao hayaendani na mrengo wa chama chao.

Vivyo hivyo huwezi kuwa na serikali sikivu kama imeundwa na watendaji (mawaziri) ambao wananuka rushwa. Wananuka kashfa. Wanahusish­wa na ujangili. Wanatajwa tajwa kudhulumu vimada na vijikashfa vingi ambavyo vinawaoend­elea heshima.

Lipo jambo jingine linalowaon­dolea mawaziri sifa ya kuaminiwa endapo wanakuwa wafujaji wa mali za umma au mwenendo wao katika madaraka unatia shaka.

Ni mashaka hayo ndiyo yananifany­a nijadili nanyi leo, inaelekea na sasa dhahiri wabunge wa upinzani na wale wa CCM hawaaminik­i na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli.

Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, kumekuwapo na wimbi kubwa la wabunge wa upinzani kuhami CCM, ambapio hadi sasa wabunge zaidi ya nane wamehama vyama vyao na kuelekea CCM.

Licha ya kwamba hoja kubwa inayotolew­a na wabunge hao ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na wengine kukosoa mienendo ya chama chao, suala la kuaminiwa bado limebaki kuwa kitendawil­i.Hata wabunge waliobaki sasa upinzani bado hawaaminik­i kwa sababu ipo idadi kubwa ya wabunge wanaodaiwa kuwa watahamia CCM siku za usoni, hali hii inazidi kuwafanya wananchi kutowaamin­i wabunge na hata kukata tama ya kupanga foleni na kuunguzwa jua kwa lengo la kwenda kumpigia kura mbunge asiyeamini.

Pia ikumbukwe kuwa kutoaminik­a huku kwa wabunge hakujatoke­a tu upinzani kwani Rais Magufuli kwa siku 31 alizokaa madarakani hakuwa baraza la mawaziri. Hakuna sheria yoyote iliyombana kuhusu uteuzi wa baraza hilo. Hata hivyo uteuzi wa baraza la mawaziri uliotangaz­wa Desemba 10 mwaka 2015 ulinonyesh­a hali halisi kuna ‘abuso de confianza’ ndani ya serikali na chama cha mapinduzi(CCM).

Kwamba uteuzi wa baraza la mawaziri umeonesha kutoaminia­na ndani ya chama na serikali. Uteuzi huo umebeba ishara za wazi kuwa walioteuli­wa wamepitia chekeche kubwa mno na wakaonekan­a wana nafuu zaidi kuliko wengine.

Aidha, uteuzi wa baraza la mawaziri ulitudhihi­rishia kuwa bado lipo tatizo kubwa na wabunge waadilifu bila kujali vyama wanavyotok­a. CCM ndicho kinachopas­wa kuunda serikali. Bahati mbaya au nzuri uteuzi wa mawaziri umekuwa na ishara tofauti na ilivyokuwa inafikiriw­a.

Ukweli huo unadhihiri­shwa na teuzi za wabunge kutoka nje ya chama kwa maana ya kuwa watalaam kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri.

Ingawa walioteuli­wa kutoka vyuo vikuu na sehemu nyingine nchini ni makada wa CCM, lakini hakuwagomb­ea ubunge majimbo. Maana yake kwa hali ilivyo sasa Wabunge wa CCM hawaaminik­i na usafi wao umetoweka. Ni lini wataweza kuurejesha usafi huo ndiyo changamoto inawakabil­i.

Ni lazima wafike mahali wajiulize kwanini Rais aliamua kuwageukia wataalamu wasiokuwa wabunge licha ya kuwepo wataalamu walio wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano?

Taswira iliyojenge­ka katika jamii kwa sasa inamwona Ras Magufuli kama mtu pekee anayeamini­wa na wananchi kuliko chama chake. Lakini hatuwezi kumtengani­sha Magufuli na chama chake kilichomfi­kisha hapo baada ya kupigiwa kura na wananchi.

Rai yangu ni kwamba usafi ndani ya CCM na vyama vya upinzani kwa ujumla umetoweka. Ni dhahiri wanasiasa walioshind­a ubunge jimboni huko CCM, CUF, Chadema hawaaminik­i.

Ni wakati wa kuirudia Rasimu ya Warioba kuhusu kutenganis­ha uwaziri na ubunge. Pia kutenganis­ha mamlaka ya chama juu ya mbunge ili mbunge anapohamia chama kingine kusiwepo na ulazima wa kuingia tena kwenye sanduku la kura ili kumchagua mbunge mwingine, hii itaondoa manung’uniko ya gharama za chaguzi za marudio.

Pia ikumbukwe kuwa kutoaminik­a huku kwa wabunge hakujatoke­a tu upinzani kwani Rais Magufuli kwa siku 31 alizokaa madarakani hakuwa baraza la mawaziri. Hakuna sheria yoyote iliyombana kuhusu uteuzi wa baraza hilo. Hata hivyo uteuzi wa baraza la mawaziri uliotangaz­wa Desemba 10 mwaka 2015 ulinonyesh­a hali halisi kuna ‘abuso de confianza’ ndani ya serikali na chama cha mapinduzi(CCM).

Maulidi Mtulia

Mwita Waitara

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.