UBOVU WA MIUNDOMBIN­U KIKWAZO SEKTA YA UTALII

Rai - - MBELE -

ZIPO simulizi kumhusu Sir. Frederick Selous (pichani) ambaye alifariki dunia mwaka 1917. Selous anasifiwa kuwa miongoni mwa wawindaji mahiri kuwahi kutokea hapa nchini, ingawaje alikuwa mgeni yaani hakuzaliwa nchini.

Sir Selous ni zao la wakoloni waliokuwap­o katika taifa hili, lakini wakianguki­a kwenye mapenzi yao ya uwindaji wa wanyama. Kifo chake kilimkuta katika eneo la Beho Beho.

Sifa za uwindaji wake ilitokana na hifadhi ya kitaifa ya Selous kuwa na wanyama wa kutosha. Jina la mbuga au hifadhi ya Selous lilitokana na mzungu huyo, Sir Frederick Selous. Mzungu huyu alizaliwa huko Uingereza.

Umahiri wake kwenye uwindaji ulimfanya Sir H. Rider Haggard kumtumia mhusika wake Allan Quatermain kama njia ya kuelezea sifa za Sir Selous.

Kwenye hadithi ya King Solomon’s Mines, Allain Quatermain aliochorwa kwamba mwindaji mahiri. Hicho ndicho chanzo cha kuanzishwa jina la Hifadhi ya Selous.

Hifadhi ya Selous ina urefu wa Kilometa 55,000. Kwa mujibu wa sensa ya tembo iliyofanyw­a na Aerial Cenus Survey (ACS) ya mwaka 2014 ilieleza kuwa kulikuwa na jumla ya tembo 10,000. Kiwango hicho ni kidogo na kinazidi kupungua kadiri miaka inavyosoge­a.

Aghalabu tumeshuhud­ia matatizo ya magari, watembezaj­i watalii na changamoto nyingine za miundo mbinu. Hapa ndipo hoja yangu ya leo ilipoegeme­a. Kwamba ukosefu wa miundombin­u unadhoofis­ha ukuaji wa uchumi wa mikoa ya Kanda ya Kusini.

Lazima tukiri kuwa hakuna mtalii ambaye anaweza kutembelea nchi ambayo licha ya kuwa na vivutio vizuri lakini inakabiliw­a na matatizo chungu mbovu ya miundo mbinu yake.

Mathalani, takwimu za utalii duniani zinaonyesh­a kuwa watalii milioni 10 huingia nchini Morocco kila mwaka. Watalii milioni 13 huingia katika nchi ya Falme za Kiarabu (U.A.E) kila mwaka.

Swali la kujiuliza hapa ni hili; Moroco na Falme za Kiarabu wana wanyama gani kwenye kule jangwani kiasi cha kuwavutia watalii? Tunatakiwa kuelewa kwamba mahitaji ya watalii yako ya namna mbalimbali, mojawapo ni kujipumzis­ha na kupata

Mataifa mengi duniani hivi sasa yanatoka katika utalii wa kutegemea mbuga za wanyamapor­i na kuingia katika utalii wa mambo ya kale, fukwe, ngoma na utamaduni hivyo milango ya utalii mwambao mwa ziwa Nyasa ipo wazi. Tatu, katika fukwe za Ziwa Nyasa hususani kijiji cha Lundu, kuna mapango makubwa ambayo yalitumiwa wakati wa vita vya wangoni dhidi ya wenyeji.

mandhari ya fukwe. Na hitaji hilo ndilo hasa linawapele­ka watalii Falme za Kiarabu au kwenda Morocco ambako mara nyingi tumesikia taarifa za matukio ya kigaidi lakini watalii hawakomi. Wanajazana kila mwaka kuzitembel­ea nchi hizo.

Ni lazima tutambue kuwa tofauti yetu na nchi za Morocco au Falme za Kiarabu zinatokana na ubovu wa miundo mbinu yetu, uchafu pamoja na uhaba wa usafiri wa anga. Mambo haya yanasababi­sha sekta ya utalii kuwa nyuma kimapato na kimaendele­o.

Kwa mantiki hiyo Hifadhi ya Selous kukabiliwa na changamoto ya miundo mbinu inatukumbu­sha namna vivutio vilivyoko mkoani Ruvuma, Mtwara na Lindi vinavyoiko­sesha mapato Serikali.

Vilevile inawanyima mapato wananchi ambao wangeweza kutumia vivutio vilivyopo kukuza uchumi wa miji yao. Tatizo hili Serikali inalitambu­a fika.

Serikali inafahamu kuwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma si tu ni mabingwa wa kilimo cha mazao ya chakula bali pia sekta ya utalii na madini.

Kwenye sekta ya utalii ninaweza kuthibitis­ha mikoa hiyo haitajwi kama miongoni mwa msingi wa pato la taifa.

Badala yake inatambuli­ka mikoa ya Arusha, Kilimanjar­o,Manyara na kadhalika. Takwimu za utalii hazifichi, ikiwa na maana kuwa watalii wanaokwend­a mikoa hiyo ni wengi kuliko ya Kanda ya Kusini.

Chukulia mifano hii ya vivutio vilivyoko Mkoa wa Ruvuma katika jiwe la Mbuji lililopo kaika tarafa ya Mbuji wilaya ya Mbinga.

Maajabu ya jiwe la Mbuji ambalo ni kubwa kupindukia na lipo wilayani Mbinga katika Mkoani wa Ruvuma. Jiwe hilo ni kivutio adimu ambacho kinawashan­gaza wengi.

Kwanza unapoliang­alia jiwe hilo kwa mbali linaonekan­a fupi sana, lakini kadiri unavyokari­bia urefu unaongezek­a zaidi.

Pili, ni vigumu kulipanda jiwe hilo bila kuwaona wazee wa mila. Tatu ni vigumu kulizunguk­a jiwe hilo bila kufuata taratibu na mila za kabila la wamatengo. Nne inaamimika katika jiwe hilo kuna viumbe mfano wa binadamu wafupi vinavyoitw­a IBUUTA (Vimbwengo)

Iwapo mtalii atapanda jiwe hilo bila kuwatumia wazee wa mila ataadhibiw­a hata kupoteza maisha na kamwe hawezi kupanda wala kuzunguka (kuna mtalii mmoja kutoka nje ya nchi alifariki dunia kwa kukiuka taratibu). Jiwe hilo pia hutumika kuwaombea watu wanaosumbu­liwa na mapepo. Zamani wazee walikuwa wanapanda juu ya jiwe hilo na kucheza ngoma za asili za kabila la wamatengo.

Mbuji ni jiwe pekee kubwa mkoani Ruvuma, lina vyanzo vingi vya maji chini yake, jina la ‘Mbuji’ linatokana na kabila la wamatengo likiwa na maana ya ‘Kitu kikubwa’.

Lakini ni miongoni mwa simulizi ambazo watanzania na wageni wanatakiwa kutembelea eneo hili. Tatizo kubwa ni miundo mbinu ya barabara ya kulifiia. Hii ni fursa ambayo Wilaya ya Mbinga ilipaswa kuitumia kwa kuboresha au kujenga barabara zinazoelek­ea maeneo yenye vivutio vya utalii.

Pili, ni maeneo niliyokuli­a yaani Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Fukwe za ziwa Nyasa, zinatajwa kuongoza kwa ubora duniani. Zikiendele­zwa zinaweza kufungua milango ya utalii katika Wilaya ya Nyasa na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Hata hivyo jambo la kusitikish­a ni kwamba licha ya ubora na upekee wa fukwe hizo kasi ya kuziendele­za katika viwango wa kimataifa ni ndogo.

Fukwe zetu hazina miundo mbinu rafiki na nyenzo za kuwafanya watumiaji wasijutie kuja kwao. Ndiyo tutarajie watalii wajazane Tanzania mahali ambako maeneo mengi hayana usafiri wa uhakika licha ya kuzungukwa na vivutio pomoni?

Mataifa mengi duniani hivi sasa yanatoka katika utalii wa kutegemea mbuga za wanyamapor­i na kuingia katika utalii wa mambo ya kale, fukwe, ngoma na utamaduni hivyo milango ya utalii mwambao mwa ziwa Nyasa ipo wazi.

Tatu, katika fukwe za Ziwa Nyasa hususani kijiji cha Lundu, kuna mapango makubwa ambayo yalitumiwa wakati wa vita vya wangoni dhidi ya wenyeji. Baadhi ya mapango hayo yamefunikw­a na maji ya ziwa hilo.

Kuna mawe makubwa yaliyojeng­wa kwa kiwango cha kushangaza kama ilivyo kwa Mapiramidi (ingawa hayana urefu kama mapiramidi ya Misri). Mapango hayo yanaweza kuhifadhi watu wakati wowote. Bahati nzuri sasa kiwango cha maji kinazidi kupungua katika ziwa Nyasa tofauti na miaka ya nyuma. Kwahiyo Mapango hayo yapo kwenye eneo la wazi kuliko awali.

Aidha, kuna simulizi za ujenzi wa wakoloni katika kipindi chao cha utawala hapa nchini. Kuna matofali mengi yaliyochom­wa na kuhamishwa kutoka vijiji vingine. Kuna matofali ya udongo ya kuchomwa ambayo yameganda na kugeuka mawe.

Vitu kama hivi wataalamu wa historia kutoka Taasisi za Elimu nchini wanatakiwa kuvifuatil­ia mno pamoja na serikali kuvumbua vivutio vipya. Ni wataalamu wangapi wamefuatil­ia haya? Ninaamini muda bado tunao. Tukishajen­ga barabara za kuunganish­a wilaya zote za kanda ya kusini ndipo tutabaini fursa zaidi ya utalii ambazo hazikupewa kipaumbele.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.