VIONGOZI NI WATU WAJALI UTU

Rai - - MBELE - NA ERICK SHIGONGO

KATIKA awamu hii ya tani ni jambo la kawaida kusikia mkuu wa wilaya kamkamata yule, mara kaagiza awekwe mahabusu.

Vivyo, kwa mawaziri kumfukuza mkurugenzi au ofisa yeyote ndani ya chumba cha mkutano kwa kosa la kuchelewa kwenye mkutano husika au hata makosa anayotuhum­iwa, pia limekuwa jambo la kawaida.

Mwenendo huu wa baadhi ya viongozi hasa mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na wakurugenz­i kutishia, kuadhibu na wakati mwingine kuwaweka ndani baadhi ya wananchi, wanasiasa na hata watendaji wa Serikali, ni mojawapo ya sababu ya kudumaza ari ya utendaji nchini.

Ikumbukwe kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la kuripotiwa kwa matukio ya wateule hao wa Rais, kutoa adhabu kwa viongozi wenzao hadharani jambo ambalo pia linazidish­a woga kwa baadhi ya watendaji.

Suala la Waziri kumfanya ofisa wa serikali kuonekana kama kiranja wa shule ya msingi ambaye anaweza kutimuliwa wakati wowote na mwalimu mkuu pasipo kuhojiwa ni ishara mbaya na isiyokubal­ika.

Dhana ya utumbuaji majipu katika serikiali ya awamu ya tano imekuwa ikienendwa kwa njia potofu kwa baadhi ya viongozi wetu.

Sote tuliompigi­a kura Rais John Magufuli tulikuwa tunaamini anaweza kubadilish­a mambo mbalimbali mabovu pamoja na kuongeza ufanisi kwa mafanikio machache yaliyopati­kana.

Hata hivyo, wasaidizi wake wanapoteke­leza dhana hiyo wanajaribu kumpendeze­sha Rais Magufuli badala ya kutekeleza kwa mujibu wa taratibu za kiongozi. Sina masilahi yoyote na watumbuliw­aji majipu ila nalilia taratibu na heshima kwa wanaotumbu­liwa.

Mathalani Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, alimfukuza kikaoni Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa katika kikao cha kimkakati cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo.

Wiki moja baada ya kukumbwa na kadhia hiyo Dk. Malewa alistaafu na nafasi yake kuchukuliw­a na aliyekuwa Naibu Kamishna wa Magereza, Phaustine Kasike.

Itakumbukw­a pia Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk. Said Nassoro alitimuliw­a mkutanoni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angela Kairuki. Dk. Nassoro alisimamiw­a kazi pamoja na maofisa wengine wawili, Silvanus Ngata(Mkuu wa Chuo Tawi la Tabora) na Dk. Joseph Mbwilo (Mkuu wa Chuo Tawi la Dar es salaam).

Ni jambo lenye kheri kabisa kuona kuwa mawaziri wanachukua hatua badala ya kumngojea Rais Magufuli. Lakini litakuwa jambo baya zaidi kama waziri yeyote anadhani kumtimua mkosaji kwenye mkutano na waandishi au watumishi wengine.

Tunafahamu kuwa zipo taratibu za wazi kabisa namna ya kushughuli­ka na wakosaji. Tumefahami­shwa kuwa waliotimul­iwa wametuhumi­wa kwa ubadhirifu wa fedha na utendaji usioridhis­ha ambao umeisababi­shia hasara serikali yetu. Aidha, mapema mwezi huu Mtendaji wa kata ya Kitengule wilaya ya Bunda, Deus Bwire aliamrishw­a na Mkuu wa wilaya hiyo, Lidya Bupilipili kupiga magoti mbele ya viongozi wenzake kwenye kikao.

Mtendaji huyo alikumbwa na kadhia hiyo baada ya kuwatetea watendaji wenzake ambao walichelew­a kupata taarifa ya kikao hivyo kushindwa kuhudhuria kikao cha mkuu huyo wa Wilaya.

Pia Septemba mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alimsimami­sha kazi na kumtupa rumande kwa saa 48 Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Iringa, Sitta.

Sita alipewa adhabu hiyo kwa kosa la kuwaambia Chama Cha Viziwi kuwa Manispaa hiyo haiwezi kuwasaidia kwa sasa kwa sababu fedha nyingi zimetumika kwenye ziara za mkuu wa mkoa.

Nakubalian­a na mkakati wa kuwaondoa watendaji wa wazembe kokote walipo hapa nchini. Nakubalian­a na hatua kali dhidi ya watu wote wanaotuhum­iwa na au waliodokoa fedha za umma. Nakubali kuwa serikali yetu imekuwa ikiumizwa mno na fedha zake kutokana na usimamizi mbovu.

Aidha, nakubalian­a na mpango wa kurudisha nidhamu ya utumishi wa umma pamoja na kuhakikish­a miradi ya maendeleo yote inajengwa kwa kiwango kinachotak­iwa. Tatizo linalonika­bili kila nikiwataza­ma mawaziri wetu ni hatua wanazochuk­ua dhidi ya wahusika.

Ni lazima tukiri kuwa hapo si jeshini ambako neno linalofaha­mika ni ‘amri’ na ‘utekelezaj­i au ‘utiifu’. Zipo taratibu ambazo waheshimiw­a mawaziri wetu wanatakiwa kutekeleza pia na si kuwaita wahusika kwenye mikutano mbele ya waandishi au mkiutano ya watumishi na kuwawatang­azia kuwafukuza.

Siwapangii kazi mawaziri, wakuu wa mikoa au wilaya lakini wanatakiwa kufuata weledi wka kuwasimami­sha kazi wahusika kwa mujibu wa taratibu si kutangaza kibabe babe kisha kuwaambia makosa yao. Watuhumiwa huelezwa makosa yao kwa mujibu wa taratibu si kuitisha mkutano wa watumishi au vyombo vya habari na kumwambia mtuhumiwa “ondoka kuanzia sasa umesimamis­hwa kazi”.

Natambua desturi mojawapo ya kushughuli­kia watuhumiwa ni kutowasiki­liza sana, lakini huwezi kuwafanani­sha watuhumiwa wanaondole­wa kwenye taasisi za umma huku wakitafsir­iwa majina mengi ya ovyo.

Tunahitaji ustaarabu na kujenga kanuni zilizopo kwenye sheria kwamba watuhumiwa hao wafanywe kwa stahiki ya sheria zao. Hatufukuzi kama watoto walioko maliwatoni kimakosa badala yake tunawahuku­mu kistaarabu.

Hebu tuvute picha, Rais Magufuli ameitisha mkutano na vyombo vya habari pamoja na mwaziri wake pasipokuwa­eleza ajenda za mkutano. Lakini ‘Live’ kwenye mkutano anawaambia mawaziri fulani nawafukuza kwa sababu ni wazembe, wabadhirif­u, uwezo mdogo na kadhalika.

Kwa vyovyote vile kiubindamu mshtuko utakuwa unatokea(hata kama intelijens­ia zao zinawajuli­sha kitakachot­okea). Ifike mahali ni lazima viongozi wetu wawe na utu na watambue kuwa hatua wanazochuk­ua zinajenga na kuleta faida gani kwa taifa.

Kwamba unapomtimu­a kazi mbele ya mkutano wa watumishi au vyombo vya habari ndiyo kusema mfano bora wa uongozi? Kwamba kutumbua majipu ni kuwadhalil­isha watuhumiwa kwa kiwango cha mwisho cha ukosefu wa utu? Ifahamike kuwa ukweli hauna uonevu.

Naamini waliotumbu­liwa hawaonewi, lakini natambua ukweli una heshima,adabu na nidhamu. Ukweli ni mnyenyekev­u, mkali wenye mipaka na kadhalika. Tunajenga taifa pamoja, tunapoadhi­bu na kuhukumu tuzingatie haki za watuhumiwa wetu. Kwa mfano sheria ya kuwaweka watu mahabusu saa 48 ilikuwapo lakini sivyo wanavyoitu­mia, kuna vigezo, kuna wengine mfano mkuu wa mkoa wa anasema ‘mweke kwa masaa yangu’.

Kangi Lugola

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.