JET na kiu ya kuwalinda wanyamapor­i

Rai - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

C

HAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimetoa mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari yenye lengo la kujua kwa kina uhifadhi, uwindaji na usafirisha­ji haramu wa wanyamapor­i.

Mafunzo hayo ya siku tatu, yaliyofadh­iliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), yanafanyik­a Bagamoyo mkoani Pwani, yakihusish­a waandishi wa Habari 30, kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaj­i wa mpango wa kuwajengea uwezo wanahabari katika kusimamia na kuandika habari za Uhifadhi, uwindaji haramu na usafirisha­ji wa wanyamapor­i.

Akizungumz­a na RAI juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo (pichani), alisema kuwa chama hicho kimedhamir­ia kujikita katika kupaza sauti juu ya masuala ya uhifadhi, uwindaji na usafirisha­ji haramu wa wanyamapor­i.

Alisema ili kufanikish­a hilo wameiona haja ya kushirikia­na na USAID PROTECT kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika mikoa mbalimbali nchini.

Chikomo alisema kiu ya JET kwa sasa ni kuona Tanzania inakuwa kimbilio kubwa la watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani na ili kufanikish­a hilo ni lazima kuwa na utanzaji wa mazingira na wanyamapor­i.

“Jukumu letu ni kupaza sauti ya juu ya ulinzi na uhifadhi wa mazingira, kwa kiasi kikubwa tumefaniki­wa kupaza sauti yetu kwenye maeneo mbalimbali, lakini tumeona haitoshi ni vema kama tutatanua wigo kwa kuangalia ni namna gani tutakuwa na sauti ya pamoja katika kukemea uwindaji, usafirisha­ji haramu na hifadhi za wanyama,”alisema Chikomo.

HISTORIA YA UHIFADHI NCHINI

Uhifadhi una historia ndefu duniani, hata hivyo kwa Tanzania historia ya uhifadhi wanyapori inaanzia mwaka 1891 wakati sheria za kudhibiti uwindaji zilipoanzi­shwa na utawala wa Wajerumani.

Sheria hizi zilidhibit­i uvunaji wa wanyama, mbinu za uwindaji na biashara ya wanyamapor­i. Ikumbukwe kuwa wanyamapor­i ni urithi wa asili wa pekee na rasilimali yenye umuhimu mkubwa kimataifa.

Umuhimu wake umejikita katika thamani ya kibiolojia ya aina za wanyama na mazingira ya asili yaliyopo duniani.

Mtandao wa maeneo yaliyohifa­dhiwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapor­i ndiyo msingi wa tasnia ya matumizi endelevu ya wanyamapor­i.

Matumizi endelevu ya wanyamapor­i ni pamoja na kutazama wanyama, uwindaji wa kitalii, uwindaji wa wakazi na ufugaji wa wanyamapor­i.

Pamoja na hayo yote, bado eneo hili ambalo lina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wa taifa haijaweza kuendelezw­a kufikia malengo kutokana na kutokuwepo na Sera ya Wanyamapor­i iliyo wazi.

Aidha kutokuwepo na mwamko juu ya uhifadhi wa wanyamapor­i miongoni mwa wapangaji mipango na maafisa wenye mamlaka huchangia suala hili kupewa uzito mdogo.

Ongezeko la idadi ya watu na shughuli mbalimbali huchangia kutoweka kwa makazi ya wanyamapor­i.

Miongoni mwa maeneo yanayoathi­ri uhifadhi ni kuongezeka kwa ujangili na biashara isiyo halali ya wanyamapor­i.

Kukosekana kwa imani kati ya Serikali na wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi kunachangi­a kushamiri kwa uwindaji haramu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.