‘Helmet’ za bodaboda kero kwa abiria

Rai - - HABARI - NA HASSAN DAUDI

N

IKIWA mmoja kati ya watumiaji wa usafiri huo, niseme wazi kuwa hatua za makusudi zinatakiwa kuchukuliw­a kukabilian­a na uzembe huu wa madereva wa bodaboda.

Leo katika safu hii pendwa ya ‘Macho Yameona’, sitazungum­zia unyanyasaj­i na lugha zao za matusi na kebehi dhidi ya abiria wa kike, wengine wakiwa na umri wa dada, shangazi, wake, au hata mama zao.

Hata wengi wao kutajwa kufanya kazi wakiwa wameshakun­ywa pombe na vichwa vikiwa vimejaa moshi wa bangi, halitakuwa na nafasi leo hii.

Kama hiyo haitoshi, nitaziacha pia mbwembwe za uendeshaji wao wawapo barabarani, ambazo wadau wa usafiri wamekuwa wakizitaja kuwa moja kati ya sababu za ajali za mara kwa mara.

Aidha, sitagusia suala la baadhi yao kuzitumia pikipiki zao katika vitendo vya kihalifu, nikiamini hilo limepigiwa kelele kwa kiwango cha kuridhisha, japo bado tatizo linaendele­a.

Katika hilo, imetokea mara nyingi kusikia malalamiko ya abiria walioporwa na watu waliotumia bodaboda na kwa bahati nzuri jeshi la polisi limekuwa likifaniki­wa mara kadhaa kuwatia nguvuni.

Mbali ya hayo, nitajiweka kando kuzianika tabia zao za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi, wakiwalagh­ai kwa ‘vijisenti’ au msaada wa usafiri.

Ni uchafu uliotamala­ki katika maeneo mengi ya mjini, na kama tafiti zitakafany­ika kuthibitis­ha hilo, basi ziwaangazi­e zaidi wanafunzi wa shule za sekondari.

Binafsi leo nitajikita katika hili la kofia ngumu (helmet) ambazo madereva wa bodaboda wamekuwa wakiwapati­a abiria wao.

Nikiri wazi kuwa lengo la kufanya hivyo ni zuri, kuepuka madhara makubwa yanayoweza kulikuta fuvu la kichwa endapo ajali itatokea.

Hivyo basi, kwa kweli hakuna anayeweza kupinga umuhimu wa helmet kwa dereva na abiria wa bodaboda.

Ni kama ambayo madereva wa magari na abiria wao wamekuwa wakilazimi­shwa kufunga mkanda, ingawa kwao ni kuepuka madhara yatokanayo na mtikisiko wa gari linapopata ajali.

Tukirejea kwa bodaboda, ukweli ni kwamba madereva wengi hawana elimu ya kutosha juu ya kufanya hivyo na ndiyo maana haishangaz­i kuona bado kumekuwa na faini zitokanazo na kosa hilo.

Ukiliacha hilo, kuna hili lililonisu­kuma kuandika makala haya, yaani tabia ya baadhi ya madereva wa bodaboda kutoona umuhimu wa kuzifanyia usafi wa mara kwa mara helmet zao.

Inakera kwa kweli, ikizingati­wa kuwa kofia hizo huvaliwa na watu wengi, kama mmoja kati ya madereva alivyoniam­bia kuwa kwa siku hupata wateja wasiopungu­a 35.

Hapo unaweza kuona ni kwa namna gani kofia hizo zilivyo na uwezo mkubwa wa kueneza magonjwa ya ngozi.

Hebu tujiulize, ikiwa mmoja kati ya abiria 35 (nikitolea mfano wa kile alichoniel­eza dereva niliyezung­umza naye), atakuwa na ugonjwa ngozi, wangapi watakuwa wameambuki­zwa endapo kofia haitakuwa imefanyiwa usafi kwa kipindi cha mwezi mmoja?

Hakika ni jambo la hatari na lazima madereva waliangali­e kwa jicho la tatu kwa kuwaonea huruma abiria wao, na kama itashindik­ana, basi washinikiz­we kisheria.

Kwa utafiti mdogo, asimilia kubwa ya abiria ambao wamekuwa wakigomea kuzitumia helmet ni kutokana na hofu yao juu ya usalama wa afya zao, ingawa baadaye hujikuta wakiingia katika mkono wa sheria wanapokuta­na na askari wa usalama barabarani.

Kama ambavyo wamekuwa wakilazimi­shwa kuwa nazo, basi maaskari wa usalama barabarani wanaweza kuwabana katika suala la usafi wa kofia hizo, ikiwezekan­a kuwatoza faini watakaopuu­zia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.