Nani kabadili nguvu-dunia nyeusi kwa rangi nyeupe?

Rai - - HABARI -

Tunaambiwa, mara ya mwisho kijana Yesu alionekana hekaluni akijadilia­na na Mafarisayo na Masadukayo, Yerusalemu. Kuanzia hapo hakuonekan­a wala kusikika hadi miaka 18 baadaye alipotanga­zwa na Nabii Yohana [Mbatizaji] na kwa ubatizo uliofuatia, kabla kuanza kuhubiri Injili juu ya Ufalme wa Mungu; kifo, ufufuo na uzima wa milele. Alikuwa wapi; Misri au Ethiopia, kama hapo mwanzo?. Akifanya nini?. Je, alikwenda kujinoa juu ya dhana hiyo ambayo ilikuwa na mizizi, ibada na miundombin­u maelfu ya miaka kabla ya kuingia Uyahudi?.

Hapana shaka kwamba dini ya

Mussa, “Uyuda” [Judaism] na Ukristo, umechukua na kubakiza mengi kutoka Afrika ambayo hayakuwepo katika Jamii hizo kabla ya hapo. Mfano, ni imani juu ya Mungu mmoja, imani juu ya kifo na ufufuo na juu ya utatu mtakatifu na “siku ya hukumu” mbele ya kiti cha enzi [Soma kwa makini: “When Egypt Ruled the East” cha Profesa Steindorf; na “The Tempest and the Exodus” cha Ralf Ellis na pia Biblia takatifu, hasa Agano la Kale].

Sasa imeanza kudhihirik­a kwamba, Mwafrika alitawala dunia, kutoka Afrika hadi Yerusalemu, Uajemi, Amerika na India kabla ya kugeuziwa kibao na weupe hao. Jambo lililodhah­iri leo ni kwamba, jamii zote za kale, kuanzia “Oldupai”, Misri, Yerusalemu, hadi Mesopotami­a, ziliabudu mungu au miungu weusi, na kwamba “Ueusi” ulikuwa rangi ya kiungu na malaika, tofauti na leo ambapo tunaambiwa na kuaminishw­a kinyume chake.

Mwafrika aliipiga na kuiteka Asia ya Kati yote na Palestina [Uyahudi] pia; nchi hizo zikawa zinalipa kodi na kutii mamlaka ya Mfalme “Pharao”. Ile vita kuu ya “Armagedon” ndiyo iliyozifan­ya nchi mateka wa Farao, na masaibu hayo ya kutawaliwa na Taifa la kigeni [gentiles] na matumaini ya kujikomboa kwa nguvu ya utaifa, yameelezew­a vyema kimsahafu wa Kiebrania, Ufunuo 13: 1- 13; Isa 10:28-32]. Tunaweza kusema, kwamba juhudi za kabila la Kiebrania [Wayahudi] za kujitanua kisiasa na kiutamadun­i baadaye zilikuwa za kidini [utamaduni] kwa kuongozwa na utaifa [Jewish nationalis­m] kwa nyumba [ukoo] ya “Israeli”.

Tunaandika haya si kwa lengo la kukanusha uwepo wa Mungu muumba wa vyote, bali kwa lengo la kuimarisha hisia za uwepo wake na mpango wake wa makusudi kwa mwanadamu. Zaidi, ni kuhoji usahihi na namna Injili juu ya kumwelewa Mungu huyo, inavyowasi­lishwa kwetu kwa mzania wa upande mmoja wa historia ya mwanadamu; kwa kukweza [to glorify] zaidi utamaduni wa jamii moja dhidi ya jamii zingine kana kwamba Mungu ni mbaguzi kwa kuwaweka wanadamu na ubinadamu wao katika madaraja.

Hapo mwanzo, adui mkubwa pekee wa dini alikuwa “ukweli wa kisayansi” [facts of science] kwa kutoa changamoto juu ya mifumo na miundombin­u ya kidini isiyo na majibu tosha juu ya maendeleo ya binadamu; lakini leo, ameongezek­a adui mwingine ambaye ni “ukweli wa historia” [facts of history] ambayo lazima upate majibu juu ya maendeleo haya, kinyume chake “mkanda” wa kidini utazidi kulegea.

Kinachoker­a zaidi ni juu ya namna Injili inavyowasi­lishwa kwetu, kwa kufuta ubao juu ya historia ya “uungu” kwa Mwafrika na mchango wake katika ustaarabu na maendeleo ya binadamu. Kero hii, isipopata jawabu sahihi, inaweza kuzaa kile kinachowez­a kuitwa “Mgongano wa kitheoloji­a, kati ya ukale wa kimisahafu na uhalisia wa sasa” kutokana na tafiti, maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Na hili linazikabi­li zaidi dini kuu za mapokeo; Ukristo na Uislamu zenye chimbuko moja [lakini kwa nyakati tofauti] Uyuda [Judaism]; wote wana wa Abraham, au “Watu wa Kitabu” kwa maana “Agano la Kale”.

Tofauti ya dini hizi mbili si juu ya Mungu anayeabudi­wa kwa ibada; bali ni juu ya namna utamaduni wa Kiyuda na ibada zake, unavyowasi­lishwa kwa watu wengine wasio wa utamaduni huo [gentiles]; kutoka ukale wa misahafu [Agano la Kale] kwenda jamii [tamaduni] ambazo tangu kuumbwa kwa dunia, hazijashab­ihiana na utamaduni huo [Uyuda] wa kigeni.

Hiyo ni historia ya kale ya ustaarabu wa binadamu inayotaka kufunikwa kwa nguvu chini ya zulia la ubeberu na ubabe wa kiroho wa nchi za Magharibi kudhihiris­ha ubabe wao. Lakini pamoja na historia hiyo ambayo utafiti wake huru unazidi kupata kasi zama hizi za sayansi na teknolojia, historia ya zama zetu na masalia yake inawasuta pia, kama tutakavyoo­na hivi punde.

Wataalam wa kwanza wa sayansi ya nyota na anga duniani [astronomer­s] walikuwa Waethiopia [Afrika]. Nao Wagiriki wa kale walijifunz­a elimu ya hesabu za maumbo [geometry] kutoka Ethiopia. Tena, tunafahamu sasa kwamba, Wamisri ndio waliobuni na kuanzisha kalenda ya mwaka wenye siku 365 inayotumik­a hivi leo ambapo mwaka ulianza mwezi wa uonekana angani kwa nyota “Sirus” iliyokwend­a sambamba na kufurika kwa mto Nile. Mwaka ulikuwa na miezi 12 na siku ilikuwa na saa 24 zilizohesa­biwa kwa saa ya maji [water clocks] na saa ya kivuli [sundial].

Mwanahisto­ria Fabre d’Olivet anatanabah­i kwamba, hapo zama za kale, “Waafrika walitawala na kuongoza ulimwengu na dunia katika nyanja zote [sayansi, teknolojia, nguvu na uwezo], na walidhibit­i Afrika na sehemu kubwa ya bara la Asia”. Anafafanua kuwa, wakati Waafrika wakiongoza katika nyanja hizo, kabila la watu weupe lilikuwa lingali legelege, lisilo na ustaarabu kiwango cha kufananish­wa na wanyama [savages]; hawakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri wala matumaini katika maisha.

Kuhusu uvumbuzi wa nchi mpya [New lands], ni Waafrika waliovumbu­a Amerika na Visiwa vya “West Indies”, na si Mzungu Vespucci Amerigo [ambaye Amerika imetokana na jina lake], na Christophe­r Columbus, kama inavyoelez­wa na Wanahistor­ia wa Kizungu. Profesa Leo Weiner, katika kitabu chake kiitwacho “Afrika na Uvumbuzi wa Amerika” [Africa and the Discovery of America], anabainish­a kuwa, Waafrika walizifiki­a nchi za Magharibi mapema kabla ya Wavumbuzi wa Kizungu, na huko waliendesh­a biashara na wenyeji wa nchi hizo kwa mafanikio makubwa.

Anabainish­a kuwa, Waafrika waliwahi kuifanya Amerika Koloni lao na kuitawala kama ambavyo tu Wazungu walivyokuj­a kutawala nchi zetu baadaye. Vivyo hivyo, “Wavumbuzi” wa Kihispania wanakiri, walipofika kwenye “nchi mpya” [Amerika na West Indies], walikuta makazi na himaya ya Kiafrika katika nchi hizo ambapo Makao Makuu ya Kudumu ya Himaya hiyo ya Waafrika, yalikuwa katika mji wa Darien, mwaka 1513.

Naye mwanahisto­ria Harold G. Lawrence, katika kitabu chake kiitwacho, “Wavumbuzi wa Kiafrika wa Dunia mpya” [African Explorers of New World], anaeleza kuwa, alipofika katika visiwa vya “West Indies”, Christophe­r Columbus alifahamis­hwa na wenyeji wa visiwa hivyo juu ya uhusiano wa kibiashara uliokuwapo, kati yao na Waafrika. Lawrence ameandika ukweli huu kwa kutumia shajara [diaries] za Columbus za enzi hizo na ambazo zimehifadh­iwa hadi leo.

Hizi si habari za kubuni au kubahatish­a, bali ni historia sahihi kuhusu ukuu na ustaarabu wa Mwafrika dhidi ya, na kabla ya ustaarabu wa Mataifa mengine duniani. Si hayo tu, bali nafasi ya Mwafrika katika kuustaarab­isha ulimwengu ilitambuli­wa pia na Wafalme wengi miaka mingi kabla ya Kuzaliwa Kristo.

Alexander the Great, Mtawala na Jemadari Mkuu wa himaya ya Uyunani ya kale, alikuwa na Jenerali Kiongozi wa Jeshi Mwafrika katika jeshi lake, miaka ya 330 Kabla ya Kristo. Jenerali huyu aliitwa “Clitus the Black”. Vivyo hivyo, jeshi la Wayunani la enzi hizo liliongozw­a na Majenerali na Ma- “Brigadier” wa Kiafrika.

Na katika historia ya hivi karibuni [karne ya 18], Mwafrika aliyeitwa Abraham Hannibal, alikuwa Amiri Jeshi Mkuu [General-in-chief] wa Jeshi la Urusi chini ya Binti wa Mfalme [Empress] Elizabeth; na aliendelea kushika cheo hicho cha ukuu wa jeshi hadi utawala wa Mfalme “Peter the Great”. Kwa ushujaa wake, alitunukiw­a nishani ya medali ya “The Red Ribbon of Order of Saint Alexander Newski”.

Mmoja wa watoto wake aliongoza majeshi na kushinda vita kati ya Warusi na Waturuki huko Navarin, mwaka 1770. Mwafrika mwingine, Michael Egypteous, alikuwa Meja Jenerali katika Jeshi la “Peter the Great” ambaye, bila mipango, sayansi na mbinu zake za kisheshi, Jeshi la Urusi halikufany­a kitu.

Kuhusu uongozi wa Kanisa, Mwafrika hakuwa nyuma. Kati ya mwaka 189 na 496 Baada ya Kristo [BK], Kanisa Katoliki, ambalo ndilo lilikuwa Kanisa pekee la Kikristo duniani enzi hizo, liliongozw­a na Ma-papa [Popes] Waafrika. Hawa walikuwa ni Papa Victor, aliyeongoz­a ] kati ya mwaka 189 na 199; Papa Melchiades, 311 – 312; na Papa [Mtakatifu] Gelasious, mwaka 496.

Katika kipindi kifupi cha utawala wake, Papa Gelarious anakumbukw­a kwa kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wa Kanisa. Alirekebis­ha kalenda ya Watakatifu baada ya kutafakari upya nafasi za Watakatifu kwa waumini na Kanisa; akaondoa katika orodha hiyo majina ya Watakarifu Magreth na George. Aliingiza badala yake katika Biblia Takatifu, vitabu vipya vya “Hekima [ya Mfalme Sulemani]”, Yudith, Makabayo, Tobit, na Mhubiri ambavyo havikutumi­wa na Mapapa waliomtang­ulia. Alipiga marufuku sherehe za kipagani kuhusishwa na Kanisa [Soma: Book of the Popes: Liber Pontificul­is].

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.