Ubia sekta binafsi, serikali kumaliza changamoto ya miradi

Rai - - MAKALA - NA AMINA OMARI, TANGA

NCHI nyingi duniani zimeweza kupiga hatua kubwa za kimaendele­o, zikiwemo za kiuchumi kutokana na ushirikian­o baina ya serikali na sekta binafsi (PPP).

Kwani kwa sasa mataifa mengi yanatumia utaratibu huu kama njia muafaka ya kutekeleza miradi ya maendeleo, kwa kasi na ufanisi mzuri zaidi.

Mfano nchi za Uingereza, Australia, Afrika Kusini, Misri, India na Korea ya Kusini, zimefaniki­wa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuzingatia kikamilifu hatua zote za maandalizi ya utekelezaj­i wa miradi ya PPP .

Ushirikian­o huo umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa harakati za kimaendele­o, hususani katika ujenzi wa miundombin­u, nishati,viwanda pamoja na maendeleo ya kuchumi katika nchi husika.

Katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2018, uwekezaji kwa kutumia utaratibu wa PPP kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, umehusisha jumla ya miradi 383 yenye thamani ya Dola ya Marekani Milioni 69.054

Hata hivyo dhana ya PPP siyo mpya kwa nchi ya Tanzania kwani ilianza kutekelezw­a kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2018 kwa uwekezaji kwenye miradi ya PPP umehusisha miradi 20 yenye thamani ya Dola ya Kimarekani milioni 863. 39.

Hivyo kutokana na mafanikio hayo ndipo Benki ya Dunia iliiwezesh­a Serikali ya Tanzania mafunzo kwa wataalamu wake ili waweze kutekeleza kwa vitendo dhana hiyo ya PPP.

Sambamba na kuweka Mfumo wa Mazingira Wezeshi, ikiwemo kutungwa kwa Sera ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi mwaka 2009, pamoja na sheria yake ubia ya mwaka 2010.

Jitihada hizi za Serikali kutunga Sera, Sheria na Kanuni za ubia, kunalenga kuweka mazingira wezeshi ya kuwezesha ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo inayokidhi vigezo vya PPP.

Kamishina wa PPP Dk. John Mboya anasema kuwa hatua hiyo itasaidia kuiwezesha Serikali kutoa huduma za umma kwa ufanisi na kwa ubora unaotakiwa.

Amesema kuwa lengo la serikali kuishiriki­sha sekta binafsi ni katika jitihada za kuharakish­a utekelezaj­i wa miradi ya maendeleo ambayo hapo awali ingeweza kusimamiwa na serikali pekee

Vile vile, utekelezaj­i wa miradi kwa mpango wa PPP utaweza kuiepushia serikali gharama ya kusubiri bajeti kwa ajili ya utekelezaj­i wa miradi Fulani na sasa utaoa fursa kwa sekta binafsi kutekeza miradi hiyo kwa haraka zaidi

“Kwa sasa tunatekele­za sera ya viwanda hivyo ilituweze kupiga kasi ya haraka ni muhimu kuishiriki­sha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuharakish­a mchakato huo”amesema Kamishna huyo.

Aidha Kamishna huyo amesema kuwa utaratibu wa PPP ni njia bora ya kukabilian­a na changamoto za kibajeti na kuiwezesha Serikali kutimiza wajibu wake katika utoaji wa huduma bora, kwa ufanisi na kwa bei nafuu kwa umma

Ambapo Dk. Mboya ameitaja miradi ambayo inaendeshw­a kwa ubia kuwa ni pamoja na Serikali Mradi wa Uendeshaji wa Huduma ya Usafiri Jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza (UDART) ambao uko katika hatua ya utekelezaj­i.

Aidha, miradi mingine ambayo iko katika hatua za mwisho za uidhinishw­aji wa upembuzi yakinifu ni pamoja na Mradi wa Kuzalisha Madawa Muhimu na Vifaa Tiba, Mradi wa Ujenzi wa Vyuo Kumi (10) Vya Ufundi Stadi unaotekele­zwa na VETA .

“Kuna miradi ambayo iko katika hatua za kuandaa taarifa za awali (Pre-feasibilit­y Studies) ikiwemo Mradi wa Kusambaza Gesi nchini unaoandali­wa na TPDC, Mradi wa Kujenga Hosteli za wanafunzi unaoandali­wa na CBE na Mradi wa Kujenga Taasisi ya Taifa ya Saratani unaoandali­wa na Taasisi ya Ocean Road Cancer Institute.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ned White, amesema kuwa wamevutika

kufadhili mafunzo ya uwezeshaji wa mpango huo kutokana na namna ambavyo Tanzania

ilivyopiga hatua katika utekelezaj­i wa programu hiyo kwa vitendo.

Amesema kuwa kwa kipindi kifupi wamefurahi­shwa na utekelezaj­i wa miradi ya ubia katika sekta ya nishati na gesi hivyo wameona ni jambo jema kuja kuwajengea uwezo.

“Miradi ya ubia inasaidia kuharakish­a maendeleo hivyo kupitia mafunzo haya tutaweza kuwajengea uwezo katika maeneo ya mikataba na sheria ili miradi hiyo iweze kuwa ni yenye tija kwa serikali na wananchi”amesema White.

Hata hivyo katika kuharakish­a maendeleo kwa haraka serikali imedhamiri­a kupeleka Mpango wa PPP katika ngazi za Halimashau­ri ambapo huko ndiko kwenye wananchi wengi ambao wanauhitaj­i wa huduma bora.

Kwani mpango huo utakuwa ni fursa nzuri kwa Halmashaur­i zote Nchini kubuni miradi yenye sifa za PPP chini ya uratibu wa Kitengo cha PPP cha TAMISEMI kwa kushirikia­na na Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo itaweza kunufaika na fursa hiyo ambapo Katibu tawala Zena Said anasema kuwa jambo la msingi sana ni utayari wa kila Halmashaur­i kuwajibika kuhakikish­a kuwa wanazingat­ia kikamilifu utaratibu huu kwa manufaa mapana ya Taifa.

Anasema kuwa iwapo wataweza kuchapa kazi kulingana na matakwa ya utaratibu huu itasaidia kupatikana kwa miradi yenye sifa na ubora unaotakiwa na hivyo kuchochea kasi ya maendeleo nchini.

“Ni dhahiri kuwa endapo Wizara na Taasisi za Serikali zitawajibi­ka kikamilifu kwa kuwa makini katika usimamizi wa miradi na uingiaji wa taratibu za ubia na kufuata hatua zote muhimu za utekelezaj­i wa miradi ya PPP tutaweza kupiga hatua kubwa ya utekelezaj­i wa miradi”alibainish­a RAS Said

Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo katika Halimashau­ri ni kutopatika­na kwa wakati kwa fedha za utekelezaj­i wa miradi lakini kwa kuwepo kwa mpango huo utawezesha Halimashau­ri hizo kutekeleza miradi yake kwa haraka.

“Hili ni jambo la faraja na ni fursa kubwa kwa Halmashaur­i zetu kutumia utaratibu wa ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii hususani ujenzi wa hospitali za kisasa, miundombin­u iliyobora,” alisema RAS Said.

Hata hivyo licha ya malengo mazuri ya serikali katika mpango huo Katibu tawala ameweza kubainisha baadhi ya changamoto zinazokabi­li Halimashau­ri katika utekelezaj­i wa mpango huo ikiwemo ukosefu wa wataalamu wa kuibua na kuandaa maandiko ya miradi,

Pia alizitaja changamoto nyingine kuwa ni wataalamu kushindwa kufanya uchambuzi wa upembuzi yakinifu ikiwemo kuandaa na kuchambua nyaraka za zabuni.

Vile vile uwezo mdogo wa wataalam katika kufanya majadilian­o ya mikataba, kutokuwepo kwa timu mahiri za kusimamia miradi ya PPP pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya maandalizi ya maandiko ya miradi.

Hata hivyo Dk. Mboya amesema kuwa katika kumaliza changamoto hizo Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imeendelea kutekeleza programu ya mafunzo ya PPP kupitia Mfuko wa kusaidia utekelezaj­i wa Miradi ya PPP ulioanzish­wa kwa mujibu wa Sheria ya PPP wenye lengo la kuboresha utekelezaj­i wa Programu ya PPP nchini.

Pia ametumia nafasi hiyo kuziasa halimashau­ri nchini, kutumia fursa hiyo kutekeleza miradi ya kimaendele­o kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizopo hapa nchini ili kuchangia kusaidia bajeti ya Taifa.

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Zena Said Kamishina wa PPP Dk. John Mboya

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.