Msururu wa vijana unaoenda kwa Ruge kufundishw­a ujasiriama­li ni aibu kwa Taifa

Rai - - MAKALA - Thadeo Ole Mushi.

MWAKA jana siku kama ya leo niliandika kuwa huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu

wakikimbiz­ana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitw­a ‘Fursa’. Najiuliza pale Mlimani wanafundis­ha nini? Najiuliza pale SUA wanafundis­ha nn? Najiuliza shule zetu za A Level wanafundis­ha nn? Huku ngazi za chini kunafundis­hwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofun­dishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindw­a kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuk­a falsafa yetu ya elimu inasemaje?

Trend ipo hivi wanaomaliz­a darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliz­a form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliz­a form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi. Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa. Hatuna clear Philosophy inayotuong­oza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehit­imu hata darasa la Saba aweze kujitegeme­a kwa kutumia fursa zinazomzun­guka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofund­isha au kufundishw­a mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

Shule zetu zilizokuwa zinafundis­ha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendele­a kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

Ibn Khladun Mwanafalsa­fa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukarirish­a watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.Kwake yeye content zilizokuwa zikifundis­hwa zilikuwa nyingi ni za kukarirish­wa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunuk­iwa cheti

Hiki ndicho tunachokio­na leo katika jamii yetu, atakayewez­a kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgra­de kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaanda­liwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrad­e kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha. John Dewey huyu ni mwanafalsa­fa wa kiamerika yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzung­uka mwanafunzi.

Hiki mdicho kinachofan­yika kwa wenzetu wazungu, wanatemgen­eza mitaala yao kulingana na kinachowaz­unguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavy­o.

Sisi tumenganga­nia kufundisha na kakarirish­ana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote ..... Je tutaendele­a kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

Je jukumu la kufundishw­a content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundis­ha Fursa?

Ukiona semina za kufundisha­na Fursa kama hizi zikishamir­i sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

Mikopo yote ya kujisomesh­a tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambi­a waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendele­za.

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosima­mia miradi utakuta ni wachina wanazisima­mia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technoloji­a yaani watu wanawaza kuuza Technoloji­a zaidi kuliko Korosho na wanatengen­eza fedha.

Technoloji­a hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundis­ha Kinjekitil­e Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengenez­a Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayoms­aidia baadaye.

Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikish­a tunakokuta­mani vinginevyo tutakuwa tukihangai­ka kila mahali kutafuta wawekezaji.

Hizi Reli tunazojeng­a na Barabara zinakuja kuwarahisi­hia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kisafirish­ia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

Naamini sisi tunaozungu­ka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibariki­wa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsir­i mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambu­i.

Bado Leo msururu wa wahitimu unaandaman­a na ruge kufundishw­a ujasiriama­li. Niliwahi kuwaambia kuwa Rwanda somo la ujasiriama­li ni la lazima kama GS huku kwetu. Kwa nn hatujifunz­i?

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.