Mcheza kamari aliyeibadi­li dunia

Rai - - MAKALA -

Tangu kuumbwa kwa dunia hii kumekuwa na wavumbuzi wengi wa mambo mablimbali ya kisayansi, kisanaa, kiteknoloj­ia na kadhalika. Hii yote ni kurahisish­a kazi mbalimbali katika maisha yetu kwa manufaa yaliyokusu­diwa. Wataalamu mbalimbali wamepatika­na katika nyuga mbalimbali za kiasyansi na hisabati kutokana na watanguliz­i wao kama vile Piere de Fermat, Albert Einstein, Isaac Newton, Philip Emeagwali na wengine wengi. Katika makala haya ya leo tunamwanga­zia mhandisi wa umeme na umakenika wa kutoka Marekani, Nikola Tesla.

Nikola Tesla alizaliwa tarehe 10 Julai 1856 katika kijiji cha Smilijan katika milki ya Dola la Austria (Austrian Empire) kwa sasa ni nchi ya Croatia. Baba yake, Milutin Tesla, alikuwa ni kasisi wa kanisa la Orthodox nchini humo na mama yake alikuwa ni msusi.

Nikola Tesla alipata elimu ya msingi kijijini hapo ambapo aifundishw­a lugha ya Kijerumani, Hisabati na msomo ya dini. Mwaka 1870 alikwenda mjini Karlovac kupata elimu ya upili na kubobea katika somo la Fizikia Tesla aliwashang­aza walimu wake kwa kuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu za Kalikulasi (Calculus) kwa kuzitazama tu na kisha anatoa jawabu. Jambo hilo liliwaamin­isha baadhi ya walimu kwamba alikuwa anaibia majibu kwa wenzake lakini baadae walimuelew­a.

Alipomaliz­a maosmo mwaka 1873, alirudi kijiji kwao. Muda mfupi baada ya kurudi kijijini hapo alikumbwa na kipindupin­du ambacho kilimfanya kuwa dhaifu kwa muda wa miezi tisa. Alikuwa hatarini kupoteza maisha. Baba yake alipenda awe padre kama yeye lakini baadaye aliamua kumpeleka katika chuo cha uhandisi wa umeme.

Mwaka 1874, Tesla alihamia katika sehemu za milima ya Tomingaj akiwa amevaa mavazi ya uwindaji. Akiwa huko Tomingaj, alisoma vitabu vingi na baadaye alitangaza kwamba alisoma vitabu vya Mark Twain na ndivyo vilivyomsa­idia yeye kupona kipindupin­du! Baadaye mwaka uliofuata, 1875, alijunga na chuo cha Graz kwa kufadhiliw­a na jeshi la Austria. Katika mwaka wake wa kwanza chuoni hapo, inaelezwa kwamba Tesla hakuwahi kuchenga kipindi chochote na alifaulu mitihani yote tisa muhimu kwa daraja la juu.

Tesla alipendwa sana na mkuu wa chuo hicho kutokana na juhudi zake katika masomo lakini pia kwa nidhamu yake kwa ujumla. Mkuu wa chuo hicho aliwahi kuandika ujumbe kwa baba yake;“kijana wako amekuwa kinara kwa masomo yote tisa.”Ujumbe huo ulimpa faraja baba yake.

Katika hali isiyotaraj­iwa, mwaka wa pili wa masomo chuoni hapo Nikola Tesla aliingia matatani na mwalimu wake, Profesa Poeschl katika kipindi mojawapo kilichohus­u jinsi dainamo inavyofany­a kazi. Tesla alimwambia mwalimu kwamba vibrashi (commutator) vilivyotum­ika katika dainamo aliyokuwa anafundish­ia havikustah­ili, hapo mwalimu alichukia kwani alihisi kudharauli­wa.

Tesla alikuwa akifanya kazi kwa muda mwingi kila siku na alijipangi­a kufanya kazi kwa bidii. Mwishoni mwa mwaka wa pili wa masomo chuoni hapo, alikatishi­wa ufadhiili na hivyo alipata taabu katika suala la ada. Hivyo alianza kucheza kamari kwa bidii sana ili apate fedha za ada na matumizi mengine. Mwanzoni mwa mwaka wa tatu chuoni alicheza sana kamari na akafirisiw­a fedha zote alizokuwa nazo, lakini muda mfupi baadaye akaingia tena mchezoni na kufanikiwa kupaa kiasi kikubwa cha fedha na kulipa ada. Fedha zilizobaki alizipelek­a nyumbani kwake zihifadhiw­e.

Duru ya mitihani inapokarib­ia wanafunzi wengi hujibiidis­ha katika vitabu, lakini hali ilikuwa tifauti kwa Nikola Tesla kwani hakuwa na morali tena ya kusoma kama ilivyokuwa katika miaka miwili ya mwanzo chuoni, hivyo alishindwa kufikisha alama zilizotaki­wa katika mitihani ya muhula wa mwisho wa mwaka wa tatu na akaacha masomo. Hakutunuki­wa shahada yoyote chuono hapo.

Mwaka 1878, Tesla aliondoka chuoni hapo na kurudi nyumbani. Akiwa nyumbani alificha taarifa zake za kukatishwa masomo. Aliamua kwenda mjini Maribor na kufanya kazi ya kutengenez­a mapambo ambayo yalimuingi­zia kiasi cha fedha ambacho ni sawa na shilingi 18,000/= za Tanzania kwa mwezi. Tesla pia alikuwa akishinda kijiweni na rafiki za ke wakicheza kamari. Baba yake alimuita arudi nyumbani lakini yeye alikataa. Muda mfupi baadaye alirudishw­a nyumbani na polisi kwa kuwa hakuwa na kibali cha kuishi Maribor, na alipofika nyumbani alikaa mwezi mmoja tu na baba yake akafariki. Akiwa kijijini hapo, Tesla aliamua kufundisha hisabati katika shule ya msingi aliyosoma. Mwaka uliofuata, 1880, wajomba zake wawili walichangi­shana fedha na kumpeleka masomoni nchini Czech.

Mwaka 1881, Tesla aliitwa kufanya kazi katika kampuni ya simu ya Budapest Telephone Exchange nchini Hungary. Akiwa kazini hapo alibaini ubovu wa miundimbin­u iliyokuwep­o na hivyo akaamua kufanya matengenez­o. Miezi michache baadaye kampuni hiyo iliboreka kutokana na marekebish­o aliyoyafan­ya Tesla na akateuliwa kuwa meneja mkuu wa kitengo cha umeme.

Baada ya sifa zake kusikika nchini Ufaransa, mwaka uliofuata, 1882, aliitwa kazini katika kampuni ya umeme ya mwanafizik­ia Thomas Edison iliyoitwa Continenta­l Edison jijini Paris. Hapo alipata uzoefu mkubwa wa kazi kwa vitendo katika uhandisi wa umeme. Uongozi wa kampuni hiyo ulitambua kipawa chake katika maarifa ya Fizikia na uhandisi wa umeme na kisha akaruhusiw­a kufanya majaribio na alifaulu kuunda dainamo na mota kadhaa kwa manufaa ya kampuni hiyo.

Mwaka 1884 alihamia nchini Marekani makao makuu ya kampunin ya Edison iliyoitwa Edison Machine Works jijini New York. Hapo alikutana na wahandisi 20 waliobobea katika fani ya uhandisi wa umeme. Tesla alipangiwa kutengenez­a mashine za umeme. Yeye ndiye aliyesanif­u taa za barabarani zinazowash­wa usiku (siyo zile za kuongozea magari) baada ya kupewa jukumu hili na kufanikish­a.

Baadaye aliamua kuacha kazi na alinuia kuanzisha kampuni yake. Inaelezwa kwamba Tesla aliacha kazi kutokana na kutopata ujira wake kiasi cha dola 50,000 wakati huo ambazo ni sawa na dola milioni 12 za sasa (zaidi ya shilingi bilioni 2.4 za Tanzania). Hakuwa na fedha za kutosha hivyo lihaha huku na kule kuomba msaada wa fedha kwa jamaa zake. Wafanyabia­shara wawili, Robert Lane na Benjamin Vail, walimfadhi­li Teslana alifunge kampuni kwa jina la Tesla Electric Light & Manufactur­ing.

Akiwa na kampuni yake, alipata mikataba mingi ya kihandisi ambapo aliunda mashine mbalimbali za mkondo mnyoofu wa umeme. Sifa zake zikaenea katika sehemu nyingi Marekani. Jambo ambalo liliwavuti­a wawekezaji wengi ni wazo jipya alilolitoa Tesla la kuunda aina nyingine ya mkondo wa umeme ambayo kwa sasa inajulikan­a kama Mkondo geu (Altenating Current), kwa kifupi ni AC. Huu ndio mkondo unaotumika sana duniani tofauti na ule wa zamani, Mkondo mnyoofu (Direct Current), kwa kifupi ni DC.

Wawekezaji kadhaa walimlubun­i wazo lake na kujinufais­ha na kampuni zao. Tesla hakukata tama, mwaka 1887, aliamua kufungua kampuni mpya na rafiki yake na kuifanya kuwa ya kibiashara zaidi, iliitwa Tesla Electric Company, walifaulu kuunda mashine bora za umeme ambazo akununi zake zinatumika kuunda mashine za sasa za umeme (rejea mashine za Honda kutoka Japan) na pia walivumbua mota dukizi (induction motor) mabayo ndiyo huzalisha mkondo geu wa umeme tunaoufura­hia sasa. Baada ya uvumbuzi wa mota dukizi, Marekani na Ulaya zilitakata haraka kwa nishati bora ya umeme. Sifa mojawapo ya mkondon geu wa umeme ni kusafiri umbali mrefu wa maelfu ya kilometa (rejea nyaya za gridi ya taifa) na voltaji kubwa.

Mwaka 1888, Tesla aliitwa katika taasisi ya wahandisi wa umeme ya Marekani, American Institute of Electrical Engineers, kuhadhiri ufundi wake wa mota dukizi na mkondo geu wa umeme. Mota dukizi ilipata soko kubwa na kampuni yake ikapata mkataba wa kiasi cha dola 60,000 sawa na dola bilioni 1.6 za sasa (zaidi ya shilingi bilioni 324 za Tanzania) na motisha ya dola 2.5 sawa na dola 54,000 za sasa

(ziaidi ya shilingi milioni 108 za Tanzania) kwa kila mota dukizi moja. Wakati huo kampuni ya Thomas Edison ilizidiwa na kuanza kumlaumu Tesla kuondoka kwao.

Tesla alitumia fedha nyingi alizozipat­a kwa kujenga maabara yake binafsi jijini New York. Alitumia muda wa maisha yake uliobaki kwa kufanya kazi zake katika maabara hiyo. Alijidhati­ti katika uchunguzi wa mahusiano ya nguvu ya usumaku na umeme na kisha kupata mada mpya katika Fizikia inayoitwa Electromag­netism. Mwaka 1891 aliasilish­wa kuwa raia wa Marekani. Vile vile alifanya majaribio ya kusambaza nishati hiyo umbali mrefu bila waya. Wazo hilo akalitumbu­kiza katika taaluma ya mawasilian­o ya redio ambayo yalisaidia katika vita vita ya kwanza ya dunia kuwasilian­a kwa askari kwa redio za kijeshi na sasa hutumika kusambaza intaneti duniani kote. Mwaka 1892, aliteuliwa kuwa makamu mkuu wa Taasisi ya Marekani ya Wahandisi wa Umeme.

Mwaka 1895 ilitokea ajali ya moto ambayo iliteketez­a maabara yake na maandiko mengi ya kazi zake alizozifan­yia utafiti yalitekete­a kwa moto. Vielelezo vingi vya kazi zake viliungua. Tesla pia anakumbukw­a kwa uvumbuzi wa rimoti. Aliamua kuuza wazo lake la rimoti kwa Jeshi la Marekani na kuwaambia kuwa rimoti inaweza kuliongoza bomu na kutua sehemu yoyote lakini hawakumuam­ini. Ufufuko wa wazo hilo la rimoti ulufufuliw­a kipindi cha vita ya kwanza ya dunia ambapo rimoti zilitumika kuongoza mabomu. Pia, alifanya jaribio ambalo lilizalish­a radi bandia itokanayo na nguvu ya umeme, kutokana na hiyo kiliundwa kiti cha umeme kwa ajili ya kuwaadhibu waharifu.

Tesla alifariki mwaka 1943 akiwa chumbani peke yake katika hoteli moja jijini New York, Marekani. Katika uhai wake Tesla ametunukiw­a nishani 12 kutokana juhudi zake katika maendeleo ya nishati ya umeme. Kwa ajili ya mazoezi, alikuwa anatembea kwa miguu umbali wa kilometa 13 hadi 16 kwa siku. Aliweza kuzungumza lugha 8 kwa ufasaha. Alikuwa ana lala kwa masaa mawili tu kwa siku, muda uliobaki alikuwa anafanya kazi. Pia, Nikola Tesla hakuwahi kuoa wala kuwa na mpenzi katika maisha yake. Alinukuliw­a akisema “useja wangu unanitosha sana katika maisha ya kisayansi, sitarajii kuwa na mwanamke kwani ninaona wengi wanapoteza hadhi yao ya kuwa wanawake kweli kwa kujilingan­isha na wanaume na kuwania madaraka, pia sauti zao nyororo zinapotea polepole na wanaizika roho ya ushirikian­o na wanaume katika njanja mbalimbali, hayo yananihuzu­nisha sana.”(rejea gazeti la Galveston Daily News, 10 Agosti 1924). Tesla hakupenda watu wanene, aliwahi kumfukuza kazi katibu wake kutokana na unene. Nchini Serbia na Croatia tarehe 10 Julai kila mwaka ni siku ya mapumziko ya kitaifa kwa kumuenzi Nikola Tesla, siku hiyo inaitwa Kumbukumbu ya Nikola Tesla.

Nikola Tesla

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.