Walioachan­a miaka 40 iliyopita waoana tena

Rai - - AFRIKA -

JUMATANO ya wiki iliyopita, ndoa ya wawili hao ilikuwa gumzo katika Ukumbi wa Manor Gatehouse ulioko mjini Dartford, Uingereza. Si kwamba sherehe ya harusi yao iligharimu fedha nyingi, bali kuoana baada ya kuachana kwa kipindi cha miaka 40 ndiko kulikowaac­ha hoi wengi.

Charlie, babu mwenye umri wa miaka 88, na Audrey Hailes (83), ndiyo walioitiki­sa mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari ulimwengun­i kwa kitendo chao hicho.

Kwa mara ya kwanza, wawili hao walioana mwaka 1955, miezi michache baada ya katika moja ya kumbi za starehe huko Peckham, eneo lililoko Kusini mwa Jiji la London, Uingereza.

Hadi wanatengan­a mwaka 1978, Charlie akitajwa kuwa sababu, tayari walishabah­atika kuwa na watoto sita, ambao wote walikuwa ukumbini wiki iliyopita kuwashuhud­ia wazazi wao wakirudian­a baada ya miongo minne.

Maisha yakaendele­a kwa Charlie kuona mwanamke mwingine na Audrey kuolewa, ambapo hata hivyo ‘wavamizi’ hao walifariki miaka michache baadaye.

Katika mahojiano yake na gazeti la News Shopper, mtoto wao wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 47, Ian, anasema si mzee Charlie wala ‘bi mkubwa’ Audrey aliyekuwa amefurahia kuachana kwao.

Kwa maelezo yake mbele ya waandishi wa gazeti hilo, Ian anasema tangu kufariki kwa mke wa pili wa Charlie, walibaini kuwa mzee wao huyo amepoteza furaha,hali ambayo pia ilimtesa mama yao.

“Tukamwambi­a baba, ‘hauna furaha, hivyo kwanini usirudiane na mama.’ Hapo ndipo ilipoanzia. Hakuna kati yetu aliyekuwa akifikiria kuwa wataoana tena,” anasema Ian aliyekuwa mpambe wa baba yake katika harusi ya wiki iliyopita.

Anaongeza kuwa ‘kufufuka’ kwa ndoa ya wazazi wake baada ya miaka 40 kupita ni tukio analoweza kulifanani­sha na filamu.

Akisimulia ilivyokuwa ukumbini siku hiyo, Ian anasema ukumbi ulifurika na muziki jazz ulichezwa kwa kiasi kikubwa siku hiyo kwani ndiyo waliokuwa wakiusikil­iza wazazi wake walipokuta­na enzi zile. Tukio hilo la Audrey na mumewe Charlie linafanana na lile la wanandoa, Neville (81) na Barbara Pearce (79), ambao waliachana na kisha kurudiana miaka 35 baadaye.

Wao walikutana mwaka 1953 na kufunga ndoa miaka mitatu baadaye lakini waliachana mwaka 1977 na ndipo Neville alipooa mke mwingine ambaye pia alikuwa akiitwa Barbara.

Kama ilivyokuwa kwa Audrey na Charlie, Neville na mke wake wa kwanza walikutana katika moja ya kumbi za starehe ambako kila mmoja alikwenda kutazama sinema na walifunga ndoa mwaka 1956.

Baada ya kuachana wakiwa na watoto wawili, David na Susan, wakiutaja ujana kuwa ndiyo zilizochan­gia, Neville alioa mwanamke mwingine, ambaye hata hivyo alifariki.

Haikuchuku­a muda kabla ya Neville kurejea kwa Barbara ambaye naye alimpokea. Hapa Barbara anasimulia ilivyokuwa na hata kukubali kwake kurudiana na mumewe huyo wa zamani.

“Sikusema ndiyo haraka, nilimwambi­a aniache nifikirie kwanza. Lakini niliona si jambo baya. Tumepoteza muda mwingi kutokuwa pamoja.”

Pia, alipokuwa akihojiwa na gazeti la Daily Mail mwaka jana, alisisitiz­a kuwa utamu wa ndoa umeongezek­a mara dufu tangu walipooana kwa mara ya pili. “Hivi sasa (ndoa) imekuwa rahisi mno. Tumegundua kuwa kuzeeka pamoja kutafufany­e tuwe tofauti na awali,” alisimulia Barbara.

Ndoa yao ya pili baada ya miaka 35 ikafungwa katikika Kanisa la Mtakatifu Thomas mjini Gawber na sasa wanaishi Barnsley, London.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.