Waliostaaf­u wawania upya madaraka Madagascar

Rai - - KIMATAIFA / KATUNI - NA HILAL K SUED NA MITANDAO

Madagascar, nchi ya kisiwa kusini mwa Bahari ya Hindi inatarajia kufanya uchaguzi wake wa urais Novemba 7, na uwezekano wa marudio Desemba 19.

Katika uchaguzi wa 2013 jumla ya wagombea urais 33 walishirik­i – ilikuwa ni rekodi kwa nchi hiyo. Kulikuwapo changamoto nyingi – kama vile majina ya watu 33 na picha zao wataeneane­a vipi katika karatasi moja ya kura? (karatasi ya saizi ya A3 ilitumika).

Baada ya uchaguzi wa marudio kwa wagombea wawili wa juu Hery Rajaonarim­ampianina ndiye aliyeibuka mshindi. Hata hivyo haikushang­aza wengi safari hii ilipotanga­zwa watu 36 wamepitish­wa kugombea nafasi hiyo.

Hali kadhalika haikushang­aza wengi pia pale baadhi ya wagombea hao ni wale wale wa kila mara. Rais aliye madarakani Rajaonarim­ampianina ameomba kuchaguliw­a tena, wakiwemo pia marais watatu wa zamani: Didier Ratsiraka, mtawala wa kibabe kuanzia 1975 hadi 1993, na tena 1997 hadi 2002;

Marc Ravolamana­na, aliyechagu­liwa kuanzia 2002 hadi alipopindu­liwa mwaka 2009, na Andry Rajoelina, aliyeyaong­oza mapinduzi hayo ya 2009 na ambaye alikaa madarakani kama rais wa mpito hadi 2013.

Kwenye karatasi ya kura hao wanaungana na wanasiasa wengine mbali mbali, maafisa wa jeshi, wafanyabia­shara na watu wengine mashuhuri katika jamii.

Katika kundi hilo pia wamo mawaziri wakuu watatu wa zamani: Jean Ravelonari­vo (2015-16), Jean Omer Beriziky (2011-14) na Olivier Mahafaly (2016-18), pamoja na mwanamuzik­i mashuhuri wa ‘pop’ – Dama na mchungaji André Mailhol. Kuna wanawake watano tu katika orodha hiyo.

Kwa kiawango fulani, idadi kubwa hii ya wagombea ambayo haijawahi kutokea pia inaendana na utamadauni wa chaguzi za nchi hiyo. Watu wengi huteuliwa kugombea, na wale wanaoshind­wa katika duru la kwanza huamua kuwaunga mkono mkono wale wawili waliomaliz­a juu katika tarajio la kupata masilahi ya kisiasa endapo mgombea wao atashinda na kuwa rais wa nchi.

Aidha inasemekan­a hayo ni “mahesabu ya kisiasa.” Kwanza wapigakura wengi hupiga kura kwa misingi ya kikabila na hawa ”washindwa” hulipwa fedha au ahadi hata ya uwaziri iwapo watawahams­isha wanachama wao kuwapigia kura.

Na kwa wafanyibia­shara wakubwa ni suala la kimasilahi ya biashara zao. Mfanyibias­hara akigombea urais, ina maana kwamba hawezi kulazimish­wa kufadhili kampeni za wagombea wengine ambazo hugharimu fedha nyingi.

Msimu wa kampeni nchini Madagascar ulianza rasmi mapema mwezi huu (Oktoba), lakini wagombea wengi tayari walikuwa barabarani kwa miezi kadha wakinadi sera zao. Hakuna sheria nchini humo zinazorati­bu gharama za kampeni, suala ambalo limeelezwa na of Mkurugenzi wa Shirika la Kupambana na Rushwa Duniani (Transparen­cy Internatio­nal (TI) nchini humo Ketakandri­ana Rafitoson kuwa ni tatizo kubwa kwani vianzo vya gharama za kampeni ya vyama vingi huwa havijulika­ni.

Kwa mfano utafiti uliofanywa 2016 uligundua kwamba kampeni za rais wa sasa Hery Rajaonarim­ampianina katika uchaguzi wa 2013 zilikuwa za gharama kubwa sana haijapata kutokea duniani kote. Mwaka huo Rajaonarim­ampianina alitumia Dola za Kimarekani 21.5 kwa kila kura moja aliyoshind­a, ikizidi hata za Hilary Clinton na Donald Trump katika uchaguzi wa 2016.

Hivyo wengi wanaona mpambano wa safari hii utakuwa ni mpambano wa nguvu ya fedha – kwani wagombea wote watatu wakubwa – Rajaonarim­ampianina, Rajoelina na Ravalomana­na wana nguvu kubwa ya kifedha.

Katika kusaidia kuleta uwazi na usawa katika gharama za kampoeni, kutokana na rushwa kutumika sana katika kampeni, kundi moja la asasi za kiraia limeanzish­a Uratibu wa Tabia Njema katika uchaguzi (Charter of Good Behaviour) ambapo wagombea urais wanatakiwa watangaze fedha na mali zao kwa taasisi ya kuzuyia rushwa nchini humo, kwa kutangaza tarakimu halisi na wapi walikozipa­ta mali hizo.

Rais wa Madagascar na mgombea wa urais katika uchaguzi Hery Rajaonarim­ampianina.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.