EAC imchukulie hatua Nkurunziza

Rai - - MAONI/KATUNI -

INASIKITIS­HA kwamba serikali ya Burundi chini ya uongozi wa Rais Pierre Nkurunziza, haikuhudhu­ria kwanye hitimisho la mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo katika kipindi cha 2015/16.

Kutokana na juhudi za viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), serikali ya Burundi ilikubali kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mustakabla­i wa kisiasa, na kutuma wawakilish­i katika mikutano yote iliyosimam­iwa na Rais mustaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa niaba ya Msuluhishi Mkuu, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Wananchi wa nchi wanachama wa EAC, tulitiwa moyo na kuamini kwamba mazungumzo hayo yakimalizi­ka, amani itatawala Burundi na hivyo kuleta maelewano miongoni mwa waananchi wake. Aidha tuliamini kwamba Burundi ikitulia, EAC utakuwa imebakiwa na kazi moja tu — ya kuwaungani­sha wananchi wa Sudani Kusini ambao hawajawahi kufurahia matunda ya uhuru wao, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo anzishwa na makundi kinzani ndani ya nchi hiyo. Rais Nkurunziza, alileta msigano baada ya kunogewa madaraka na kutaka kubadili Katiba ya nchi, kinyume na mapatano ya Arusha ya mwaka 2000. Japo alifanikiw­a kufanya hivyo kwa hila, wananchi wa Burundi na wadau wa demokrasia na utawala bora ndani na nje ya Burundi hawakufura­hishwa. Matokeo yake vurugu kubwa ziliikumba nchi hiyo na watu kuuwawa na wengine kukimbilia uhamishoni.

Tulikuwa na matumaini kwamba, Nkurunziza angekuwa amejifunza na angeendele­a na mazungumzo hayo mpaka yafikie mwisho mzuri. Tumeshitus­hwa na taarifa kwamba katika mazungumzo ya mwisho yaliyofany­ika Arusha kwa muda wa siku tano mwezi huu, serikali ya Burundi haikuwakil­ishwa, kitendo ambacho kinatafsir­iwa kwamba ni ujeuri, ufidhuli na dharau kwa viongozi wa EAC.

Wananchi wa Burundi sasa kwa pamoja wasimame kidete na kuinesha serikali ya Burundi ya sasa — kwamba wamechoka na vurugu na ngonjera za kisiasa — kwamba wanataka kufaidi amani na utulivu uliopo katika nchi jirani wa wanachama wa EAC kwa jumla, ili nchi zetu hizi zianze kwa pamoja safari mpya kielekea kwenye mwongo mpya — wa kuijenga Afrika Mashariki upya na kufanya shughuli za kiuchumi, kibiashara na kijamii kwa pamoja.

Tunamponge­za Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ambaye alikubali, kwa niaba ya Rais Museveni na kwa niaba ya marais wengine wa EAC, kuubeba mzingo wa kutafuta suluhu ndani ya Burundi. Tunasikiti­ka kwamba Rais Nkurunziza, ameonesha tabia ya ulaghai, na hivyo kuwacheza shere viongozi wenzake na wana Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kama serikali ya Burundi itaendelea na mchezo huu, tunashauri kwamba katika kikao kijacho cha wakuu wa EAC, wachukue uwamzi wa kuisimamis­ha Burundi uwanachama.

Wananchi wa EAC wangependa kubadilika na kufanya mambo tofauti na huko nyuma — ambako viongozi wachache, wenye maono mafupi na ubinfsi, walitukati­sha ndoto ya kuwa Jumuia moja. Nkurunziza ataondoka, Burundi itabaki. Asiwakatis­he taamaa wananchi wa Burundi kwa kuwa king’ang’anizi wa madaraka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.