Marekani na kura ya maoni kwa rais aliye madarakani

Rai - - MAKALA/KATUNI - NA HILAL K SUED

Jumanne ijayo Novemba 6, 2018 Marekani itafanya uchaguzi mdogo (mid-term election). Uchaguzi huu huitwa hivyo kwa sababu hufanyika kila katikati ya kipindi cha miaka minne baada ya ule uchaguzi wa urais – ambao ndiyo huitwa Uchaguzi Mkuu.

Uchaguzi mdogo unajumuish­a uchaguzi wa Wajumbe wote 435 wa Baraza la Wawakilish­i (House of Representa­tives), na takriban theluthi moja ya Wajumbe 100 wa Baraza la Senate – yaani takriban wajumbe 33 au 34. Hawa kipindi chao cha Useneta ni miaka sita hivyo kila miaka miwili – yaani wakati wa uchaguzi mkuu na uchaguzi mdogo viti vya maseneta theluthi moja huwa wazi ni hivyo uchaguzi hufanyika.

Aidha majimbo 36 kati ya 50 ya nchi hiyo huchagua Magavana wao wa majimbo (State Governors) katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo na wengine waliobaki (magavana 16 huchaguliw­a wakati wa uchaguzui mkuu.

Katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo majimbo kadha hufanya uchaguzi wa wawakilish­i wao katika mabaraza ya wawakilish­i na ya maseneta katika ngazi za majimbo, pamoja na mabaraza ya manispaa ya miji mbali mbali na mameya.

Kwa kawaida uchaguzi mdogo huamsha idadi ndogo ya wapigakura ikilingani­shwa na uchaguzi mkuu. Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita uitikio wa wapigakura wote waliojiand­ikisha umewahi kufikia kati ya asilimia 50 hadi 60 wakati wa uchaguzi mkuu, kwa uchaguzi mdogo uitikio umekuwa hauzidi asilimia 40.

Kikawaida katika uchaguzi mdogo chama tawala (kwa maana chama ambacho rais ndiye yuko madarakani) hupoteza viti vya mabunge yote mawili na hivyo wapinzani kuongeza nguvu katika uwakilishi.

Hivyo mara nyingi chaguzi ndogo huwa kama kura ya maoni kwa utendaji wa rais au wa chama kilicho madarakani na mara kadha maoni huwa ni kupoteza uungwaji mkono kutoka kwa wananchi.

Katika kipindi cha miaka 21 iliyopita chama cha rais kimekuiwa kikipoteza wastani wa wajumbe 30 wa Baraza la Wawakilish­i na Maseneta wanne katika chaguzi ndogo. Ni katika chaguzi ndogo mbili tu ambapo chama cha rais kilifaniki­wa kuongeza viti katika mabaraza yote hayo mawili.

Sasa hivi uwakilishi kivyama katika mabaraza yote mawili ni kwamba katika Senate chama cha Republican (chama cha rais) kina viti 51 (katika viti 100) na Democratic wana viti 47. Kuna viti viwili vinashikil­iwa na chama cha Independen­t. Kwa upande wa Baraza la wawakilish­i, Republican wana Viti 235 na Democratic viti 193 – na kuna viti 7 vilivyo wazi.

Tafiti mbali mbali zilizofany­wa zinaonyesh­a kwamba iwapo uitikio unakuwa mkubwa kuliko wastani – kwa mfano kuanzia asilimia 70 na kuendelea, chama cha Republican hakiwezi kushinda uchaguzi, si wa rais wala wa mabunge hayo mawili. Inasadikiw­a kwamba uwiano wa ufuasi wa kivyama kati ya Democratic na Republican nchini humo ni 2:1 – yaani takriban theluthi mbili ya wananchi wote wa Marekani wenye uwezo wa kupiga kura hujitambul­isha kama wafuasi wa chama cha Democratic.

Kinachotok­ea kwa Republican kuwapiku Democratic mara kwa mara ni uitikio wa upigaji kura siku ya kupiga kura – wafuasi wengi wa chama cha Democratic huwa hawaendi vituoni kupiga kura siku ya kupiga kura. Hii inatokana na sababu kadha.

Kwanza kabisa wengi wao ni wafanyakaz­i katika sehemu za miji mikubwa na wanajishug­hulisha katika kutafuta vipato vya kuendesha maisha yao hivyo hawaoni sababu ya kuondoka makazini mwao kwenda vituoni kukaa foleni kusubiri kupiga kura.

Pili, katika hilo hilo la kwanza kwa kiasi kikubwa sana linachangi­wa na kwamba siku ya kupiga kura, ambayo kikatiba imepangwa kuwa “Jumanne ya kwanza baada ya Jumatatu ya kwanza ya Novemba” ni siku ya kazi, na siyo sikukuu ya taifa (public holiday).

Zimekuwepo jitihada za muda mrefu, hasa kutoka kwa viongozi wa chama cha Democratic za kutaka marekebish­o katika Katiba ya kuifanya siku ya kupiga kura kuwa siku ya mapumziko. Mara nyingi wazo hilo limekuwa likipingwa na viongozi wa Republican kwa hofu kwamba linaweza kuwaathiri katika chaguzi.

Sasa hivi kuna msukumo mpya wa kuifanya siku ya kupiga kura kuwa ya mapumziko, msukumo unaoendesh­wa na Bernie Sanders, Seneta wa Jimbo la Vermont tangu 2007.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.