BURE SI HATI YA DHIKI NA UJINGA

Rai - - MBELE - Baruapepe; mawazoni15@ gmail.com

ELIMU bure ni neno rahisi ambalo kila mmoja anaweza kulisimuli­a kwa muono wake. Ni maneno ambayo yanasadifu mipango na mikakati ya kulielimsi­ha taifa hili, ili kuondokana na adui ujinga, maradhi na umasikini, pamoja na utegemezi wa wafadhili wa ughaibuni.

Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, ilipitisha mpango wa Elimu Bure kuanzia shule ya msingi hadi Hidato cha Nne.

Taarifa hiyo ilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati huo, Shukuru Kawambwa. Katika mikakati hiyo ilielezwa kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi hadi sekondari kidato cha nne itakuwa elimu ya bure, huku baadaye ikitajwa kuwa itakuwa elimu ya msingi ili kwenda kidato cha tano na sita uwe uchaguzi wa mwanafunzi husika.

Katika muktadha huo kwenye uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani, suala hilo lilipigiwa mbiu na kubebwa kama moja ya ajenda ya kuombea kura kwa wananchi.

Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, alibainish­a hilo kuwa utawala wake utakuwa wa elimu bure kama ilivyoaini­shwa.

Aidha, aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa nae alijinasib­u

kutoa elimu bure kwa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lowassa katika vipaumbele vyake vitatu alizungumz­ia ‘elimu, elimu, elimu.

Sasa serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani tangu Novemba 5 mwaka 2015 chini ya Rais John Magufuli. Serikali ilibainish­a wazi kutekeleza mkakati wake wa kutoa elimu bure.

Wanafunzi na shule zao maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakipokea bajeti za utekelezaj­i wa mpango wa elimu bure. Hata hivyo baadhi ya shule zimeondole­wa kwenye mpango wa elimu bure kwa sababu zilizoaini­shwa na serikali.

Sina tatizo na mipango ya utoaji wa elimu bure katika taifa langu. Nina matatizo ya utekelezaj­i wa mpango ambao ninauona kama dhihaka mbele ya mwananchi. Mbele ya mwananchi masikini ambaye alikuwa akitegemea mpango huo kukata kiu ya elimu ya watoto wake.

Nakubali kwamba taifa letu halina mapato makubwa, lakini sikubalian­i kuwa utekelezaj­i wa elimu bure uwe unaambatan­a na kero mpya pamoja na zamani zisizotatu­liwa. Kabla ya utoaji wa elimu bure kulikuwapo kwa kero mbalimbali katika sekta ya elimu, na hazikuwahi kutatuliwa hata kidogo.

Utoaji wa elimu bure umeibua kero nyingi ambazo kwa namna moja ma anyingi zimekuwa kikwazo kwa maendeleo ya wananchi wetu. Hii ni dhihaka kwao kwani haitatui changamoto zilizokuwe­po na sasa zimezidish­wa pamoja na kuundwa kero mpya.

Walimu wanatambua mazingira yao ya kazi. Walimu wanafahamu kero na mahitaji ya msingi ya elimu yetu. Wanafahmu kuwa pamoja na utatuaji wa kutoa bajeti (kwa maana ya fedha) bado tunalo tatizo la msingi ya ukamilishw­aji wa mpango huo pamoja na ushirikish­waji wao hafifu.

Mathalani Mwalimu mmoja aliyeko wilayani Kahama katika mkoa wa Shinganya amewasilia­na nami na kunieleza machache, “Elimu bure ni jibu, ambalo linapaswa kutumbuliw­a kwakuwa matatizo ya kale hayakupati­wa ufumbuzi. Shule nyingi kwenye mitihani ya robo muhula walilazimi­ka kuandika ubaoni badala ya kuchapishw­a. Wengine karatasi hazikutosh­a, kwamba hakuna karatasi mashuleni,”

“Watoto wanachana kwenye madaftari yao ili waweza kuwa na karatasi za mitihani. Shule nyingine hawakufany­a kabisa mitihani ya robo muhula sababu ya matatizo mbalimbali,

“Kwa mfano hapa shuleni kwetu sasa, mkuu wa shule alitoa agizo kuwa mitihani tutunge ukurasa mjmoja tu. Sasa unajiuliza kwa watoto wa kidato cha nne au cha pili utampimaje kwa kumtungia mtihani wenye ukurasa mmoja wa karatasi?

Anaendelea kusema, “Ukurasa mmoja ni testi ya darasani au ni mtihani wa kumuandaa kufanya Mock? Tukajifany­a vichwa ngumu, tukatunga mitihani kama ilivyo kawaida, lakini ilivyorudi sasa ni kichekesho. Ilibidi wapunguze maswali yaani ndani ya dakika 10 mwanafunzi kamaliza mtihani, nilishikwa na butwaa. Kwa kweli hali ni tete.

“Serikali na wadau wa elimu wana kazi ya kufanya kuboresha elimu na siyo kutekeleza sera ya elimu bure bila kuzingatia elimu bora,” alimaliza mwalimu huyo.

Picha tunayoipat­a hapa ni kwamba wananchi wetu wanaishi kwenye mkanganyik­o mkubwa kuitambua elimu bure na gharama za elimu. Bajeti zinazopele­kwa kwenye shule zetu za msingi na sekondari hazitoshi na haziwekwi kwenye tathimini halisi ya mahitaji ya shule husika katika mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji. Kwamba wakati tunajitahi­di kutoa fedha za bajeti kwa ajili ya shule hizo tunaiikuta taifa letu halikuwahi kutatua kero katika sekta ya elimu.

Mifano ni mingi. Unaweza kwenda katika shule moja utakutana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaketi chini ndani ya darasa lenye vumbi. Tumekuwa na vyumba vya madarasa visivyojal­i afya ya mwanafunzi na mwalimu.

Tumekuwa na madarasa ambayo hakidhi vigezo vya kuitwa madarasa ya kujifunzia na kupata elimu. Badala yake tunajigamb­a kwa idadi kubwa ya vyumba vya madarasa pamoja na wanafunzi walioandik­ishwa kujiunga na shule hizo badala ya nini tunachofan­ya kukidhi mahitaji ya elimu katika shule husika.

Tuna matatizo ya madawati kwenye shule mbalimbali. Tuna matatizo ya wanafunzi na wazazi katika mahusiano ya kielimu na maendeleo. Tumejikuta kwenye mkanganyik­o wa kujua elimu bure ni nini na elimu yenye gharama ni nini. Tumegeuza suala la elimu bure kuwa dhihaka.

Walimu wanabugia vumbi darasani, huku wakifundis­ha wanafunzi wao. Mazingira ya kazi hayavutii na hayatoi motisha kupata wavumbuzi, magwiji na wataalamu kuanzia ngazi za shule za msingi. Tumebakiza kujisifu tunatoa elimu bure bila kuzingatia tunachokit­oa kinasaidia namna gani na kufanikish­a kutatua kero za elimu wMawazoni mwangu ninaamini kuwa matatizo makubwa yaliyolimb­ikizwa miaka mingi ayanazidi kulitafuna taifa hili. Naunga mkono elimu bure, lakini sikungi mkono wanafunzi kusoma kwenye madarasa machafu, chini ya miti, mwalimu kukosa vitenda kazi, kisha akabaki kuwa mtu wa kulalamiki­wa kuwa chanzo cha kuanguka elimu yetu.

Ni lazima serikali ikubali kuwa kutoa elimu bure haina maana kwamba kumwaga fedha peke yake bila kujali mazingira shule zenyewe. Tunatakiwa kuwaangali­a wanafunzi wetu wanajifunz­ia katika mazingira gani. Tunapaswa kuangalia vitenda kazi vyetu vinakidhi mahitaji au la.

Kama leo hii Mwalimu anakoseshw­a karatasi za kutungia mitihani nini maana yake? Kama leo hii mwanafunzi atungiwe mitihani ambao haumpi motisha wala kuvutia nini kinachotar­ajiwa? Basi tunajikuta tunaunda taifa la kizembe lenye ujinga uliokithir­i.

Taifa ambalo linajijeng­ea utamaduni wa kutojali mambo ya msingi na badala yake sote tunajijazi­a fikra za kibambucha kila kukicha. Leo wanafunzi wanaketi ‘zero distance’ kwenye mitahani kisha tunajidang­anya tunawpaima ufahamu? Hiyo nayo ni elimu? Kisha tunajidang­anya hapo tutao mwanafunzi mwenye akili nzuri kweli! Aibu iliyoje.

Leo hii wanafunzi na walimu wanagombea viti shuleni huko mkoani Shinyanga. Kwamba mwalimu akichelewa kufika shuleni basi kiti kinachukul­iwa na mwanafunzi kwenda darasani akitumie. Heshima ya mwalimu na mwanafunzi itakuwepo?

Ni lini elimu ya watu masikini sisi itapewa heshima na kuijali? Tunadangan­ya wananchi kuwa michango imefutwa huku hatutoi huduma za msingi kama vifaa vinavyohit­ajika shuleni?

Tunataka magwiji wa sayansi na hisabati wakati shule hazina vyoo, maabara, maktaba, vitabu na kadhalika? Nini nafasi za idara za Ukaguzi wa shule? Ni idara inayopewa nafasi yake ipasavyo na tunaitumia vipi hiyo kupima hiki tunachokii­ta elimu bure kwa mwananchi wa Tanzania? Tujisahihi­she.

Wanafunzi wakiwa darasani

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.