NYUMBA ZAO WALALAMIKI­A FIDIA

Rai - - MBELE - NA HARRIETH MANDARI, GEITA

JAMANI hata kama nimekula chumvi nyingi, lakini nina haki ya kulipwa fidia kutokana na uharibifu uliotokana na mitetemo ya ulipuaji baruti huko kwenye mgodi ambao umebomoa nyumba zangu,”

Kauli hiyo ya kutoridhis­hwa na mwenendo mzima wa zoezi la ulipaji fidia inatolewa na Efrasia Kakwaya (85), ambaye ni mmoja wa waathirika wa milipuko hiyo waishio karibu, au ndani ya eneo la mgodi huo ambalo iliamriwa walipwe fidia na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim na Waziri wa Madini, Angela Kairuki.

Aidha, wawekezaji hao waliamriwa kwa mara ya kwanza na Kairuki kuwa Agosti 8 wahakikish­e wawe wameshalip­a fidia hizo lakini hawakuteke­leza agizo hilo ndipo alipokuja Waziri Mkuu Majaliwa mkoani humu kufunga rasmi maonesha ya kimataifa ya dhahabu na teknolojia ya kisasa ya uchimbaji madini hayo yaliyofany­ika Septemba mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu aliwaongez­a muda wa ulipaji fidia hadi Oktoba 24 mwaka huu zoezi liwe limeshaanz­a .

Hata hivyo hadi sasa hakuna fidia wala fununu ya ulipaji kwa wahanga hao hali ambayo imeendelea kuwatia simanzi wakazi hao.

RAI lilifaniki­wa kumtembele­a ajuza huyo ambaye ana watoto nane huku akiishia pia na wajukuu zake huku akizungukw­a na nyumba zake nane ambazo kati yake tatu zina nyufa kubwa, mbili zimebomoka.

Bibi Efrasia anasema amekuwa akiishi maisha ya hofu tangu enzi za utawala wa Raisi mstaafu Jakaya Kikwete hadi awamu hii kutokana na milipuko hiyo inayomfany­a azimie kila inapolipul­iwa.

“Walikuwa wakilipua nazimia tena kwa mara kwanza nilizimia nikapelekw­a Bugando hospitali ya rufaa, na hadi sasa nimepata tatizo la moyo lililosaba­bisha niwe nazimia kila mara” anasema.

Anaongeza kuwa kawaida walikuwa kampuni hiyo hulipua mara tatu hadi nne kwa wiki hivyo kutokana na hali ya matatizo ya moyo, iliwalazim­u watoto wake wamgharami­e fedha za kumhamisha na kumpeleka mbali na eneo hilo kila kunapokuwa na mlipuko hali ambayo ilikuwa inawaghari­mu fedha nyingi kwa kiasi kikubwa.

“Nimekuwa naishi kwa mateso kwa miaka mingi sana tangu enzi za Kikwete kila kunapolipu­liwa baruti huwa kunatokea mitikisiko mikubwa hadi tunalalian­a. Japokuwa kwa miezi saba iliyopita milipuko imepungua ndiyo maana nimetulia nyumbani kwangu,” anasema.

“Kila nilipokuja kuchukuliw­a na taksi nilikua nakodi kwa sh 10,000 kama nikienda eneo la Mwatulole (eneo nje ya mji wa Geita) na iwapo walinipele­ka mjini basi nililazimi­ka kulipa sh 5,000 kwa miaka yote zaidi ya 10 iliyopita,” anasema.

Aidha, anawataka GGM kuwalipa fidia ya nyufa nyumba zake hizo, ambazo mbali na kupata nyufa kubwa nyingine zimebomoka na kuanguka kabisa,

Awali, mvutano huo kati ya wanachi waishio karibu na GGM na mgodi huo umekuwepo kwa miaka mingi ambapo wakazi hao waliahidiw­a kulipwa fidia ambapo hadi sasa hawajalipw­a hali ambayo inawalazim­u kuishi kwa kutumainia kuwa ipo siku watapatiwa haki yao.

Bibi Efrasia anasema akiwa mmoja wa wahanga wa milipuko hiyo, amechoshwa na ahadi zilizokwis­hatolewa na mgodi huo kuwa watalipa licha ya kuamriwa na viongozi mbalimbali waliotembe­lea maeneo hayo akiwemo Kairuki, Aliyekuwa waziri katika ofisi ya Rais Mazingira, Kangi Lugola, Manaibu waziri wa madini, Doto Biteko na Stanslaus Nyongo ambao wote waliamuru fidia ilipwe mara moja bila mafanikio.

RAI lilitembel­ea wakazi wa Kata ya Nyamalembo ambalo pia wanapakana na mgodi huo na kuzungumza na Afisa mtendaji, Gerald Kamugisha, wa Kampaundi ya Nyamalembo.

Mtendaji huyo naye anasema kuwa eneno hilo lenye nyumba 100,000 limeathiri­wa kwa kiasi kikubwa kwani asilimia 90 ya nyumba za eneo hilo zimebomole­wa na milipuko hiyo.

Mmoja wa wakazi hao, Rehema Aziz ambaye nyumba yake imeanza kutitia na yenye nyufa kila upande aliiomba serikali isisite kutoa msisitizo kwa wawekezaji hao ili wawalipe fidia. Aidha, mumewe Rehema, Abdul Aziz anasema ameanza kupigania haki yake ya kulipwa fidia kwa zaidi ya miaka 10 sasa bila mafanikio,

“Nakumbuka nilishaend­a hadi bungeni kutafuta njia ya kutoa kilio chetu bila mafanikio, na hata viongozi mbalimbali wakiwemo

mawaziri walitembel­ea nyumba

hii na wakaamuru GGM itulipe fidia zetu lakini bila mafanikio yoyote yale hali ambayo inatufanya tuishi kwa hofu miaka yote ya kuangukiwa na nyumba zetu zilizobomo­ka,”anasema.

Anaongeza serikali iliteua taasisi ya utafiti ya GST na kufanya tathmini na utafiti uliodhihir­isha kuwa nyumba hizo zilibomoka kutokana na milipuko hiyo.Kwa upande wake, Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Geita, Godfrey Keraka, anasema pamoja na kutolewa kwa maagizo kutoka serikali kuu juu ya kampuni ya GGM kuwalipa fidia wananchi hao bado ofisi hiyo haijapata taarifa zozote za kuanza kwa ulipaji huo.

“Wakazi hao wana haki ya kulipwa fidia kwa kuwa mgodi huo wakati unaanza kuchimba dhahabu, uliwakuta wakazi hao hivyo ni haki yao ya msingi kuliowa fidia hito,” anasema.

Geita ni mkoa wenye madini ya aina ya dhahabu kwa wingi sana na ni mojawapo ya shughuli kubwa inayouinia lipato mkoa huu.

Pamoja na malalamiko hayo, Meneja mawasilian­o na mahusiano wa Mgodi wa GGM, Tenga Bill Tenga, anasema suala hilo litashughu­likiwa na kwamba kwa sasa unasubiriw­a uamuzi wa mwisho kutoka makao makuu ya migodi ya Anglo gold Ashanti yaliyopo Afrika ya kusini.

‘Suala hilo linafanyiw­a kazi na kwa sasa tunasubiri­a tu hatma ya lini tunaanza kulipa fidia hiyo kwa hiyo suluhu itapatikan­a tu,”

anasema Tenga.

Sehemu ya nyumba za bibi Efrasia inayodaiwa kubomoka kutokana na milipuko ya GGM

Bibi Efrasia akiwa ameketi kwenye makazi yake katika kata ya Katoma, mkoani Geita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.