Matukio yaliyobadi­li mtiririko wa mustakabal­i wa Zanzibar

Rai - - MAONI/KATUNI -

Kwa kiasi fulani upo ukweli ule usemi kwamba historia ina tabia ya kujirudia, ingawa mimi nasema hujirudia kwa namna tofauti na ile ya awali. Na ni ukweli pia kwamba binadamu wengi wana hulka ya kupenda kuona mtiririko tofauti

Kwa kiasi fulani upo ukweli ule usemi kwamba historia ina tabia ya kujirudia, ingawa mimi nasema hujirudia kwa namna tofauti na ile ya awali. Na ni ukweli pia kwamba binadamu wengi wana hulka ya kupenda kuona mtiririko tofauti wa mambo iwapo tukio fulani lingejirud­ia, kuliko mtiririko wa ilivyokuwa awali.

Ni vyema nikalielez­a hili kwa kutoa mfano wa tukio lilitokea Ulaya zaidi ya miaka 100 iliyopita, tukio ambalo lilisukuma kutokea Vita Kuu ya Kwanza ambayo zaidi ya watu milioni 16 walikufa, wakiwemo wazalendo wa nchi hii ambayo sasa inaitwa Tanzania.

Tukio lililoanzi­sha vita ile ni kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Archduke Franz Ferdinand, mtawala wa Sarajevo (sasa mji mkuu wa Bosnia-Herzegovin­a) tarehe 28 June 1914. Mtawala huyo asingeuawa yumkini kusingetok­ea vita kwa namna ilivyokuwa.

Au chukulia mfano huu mwingine huko huko Ulaya. Mwaka 1929, wakati wa harakati zake za kisiasa na kabla ya kutwaa madaraka nchini Ujerumani, Adolf Hitler alinusurik­a kuuawa na mtu mmoja aliyetumwa na mahasimu wake wa kisiasa katika ukumbi mmoja aliokuwa akihutubia huyo dikteta mtarajiwa wa Ujereumani.

Mtu huyo ilikuwa amlenge Hitler na kumpiga risasi halafu akimbie. Lakini kabla ya kufanya hivyo alishikwa na haja ndogo na aliona ni vyema kwanza aende msalani amalize haja yake. Lakini aliporudi ukumbini akakuta Hitler kamaliza hotuba yake na alikuwa anaondoka ukumbni.

Hebu fikiria – watu wapatao milion 50 duniani kote walitekete­a katika Vita ya Pili vya Dunia (1939 – 1945) iliyoanzis­hwa na Hitler kwa sababu mtu mmoja alishikwa haja wakati mbaya. Ukweli ni kwamba Hitler angeuawa siku ile, kusingotok­ea Vita hiyo yenye maafa makubwa kuliko yote katika historia ya dunia.

Hapa kwetu upo mfano kama huo, na ni matukio mawili kuhusu Zanzibar, ingawa matukio yote hayakutiri­rikia kwenye maafa makubwa ya vita. Hata hivyo moja – lile la awali lilisababi­sha mapinduzi ya umwagaji damu kwa kiasi kidogo.

Kwanza- mwaka 1963 katika harakati za kujipatia uhuru kutoka Uingereza ambayo Zanzibar ilikuwa chini ya himaya/ulinzi (protectora­te) yake tangu 1896 kulikuwapo vyama vitatu vikuu vya kisiasa vikigombea kuunda serikali baada ya uhuru: AfroShiraz­i Party (ASP), Zanzibar Nationalis­t Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba Peoples’ Party (ZPPP).

Katika uchaguzi wa mwisho kabla ya uhuru ASP iliongoza kwa kiti kimoja katika Baraza la Kutunga Sheria (Bunge) lakini haikuweza kuunda serikali kutokana na uamuzi wa chama cha ZPPP (ambacho kiliibuka cha tatu kwa idadi ya viti) chini ya kiongozi wake Mohamed Shamte kuungana na ZNP kilichokuw­a kikiongozw­a na Ali Muhsin Baruani na hivyo yeye (Shamte) kupewa jukumu la kuunda serikali na kuwa Waziri Mkuu wake wa kwanza.

Haya yalikuwa kwa mujibu wa mapatano yaliyofiki­wa baina ya ZPPP na ZNP na lengo ni kukipiku na kukiacha nje chama cha wazalendo – ASP cha Abeid Aman Karume.

Hili halikuonek­ana kukaa sawa kwa sababu ZNP kilikuwa kinaungwa mkono na utawala wa Kisultani ambao kulikuwapo kila dalili kuendelea kuwapo kwake, pamoja na Visiwa hivyo kupata ‘uhuru’ kutoka Uingereza. Hivyo mwaka 1964 yakatokea mapinduzi yaliyoongo­zwa na ASP na kubadilish­a historia nzima ya Visiwa hivyo – angalau kwa kipindi cha miaka minane iliyofuata.

Laiti ZPP ingeungana na ASP, historia ingekwenda kivingine na wengi wanasema kusingekuw­apo sababu ya mapinduzi. Demokrasia ingeweza kushamiri na nchi kupiha hatua kubwa za kimaendele­o hadi leo. Iwapo kisiwa cha Mauritius kiliweza kufanya hivyo, Zanzibar pia ingeweza.

Tukio jingine lilitokea baada ya kuuawa kwa Abeid Aman Karume, muasisi wa mapinduzi ya 1964 na rais wa kwanza wa Zanzibar, tukio ambalo kwa mara nyingine lilibadili­sha mtiririko wa kihistoria wa visiwa hivyo hadi leo. Na iwapo angenusuri­ka katika tukio lile la mauaji, bila shaka historia ya visiwa hivyo ingekwenda kivingine kuliko ilivyokuwa – na wengi wanasema hata tukio lile la mwaka 1977 la kuungana kwa TANU na ASP huenda lisingetok­ea.

Hivyo basi hali ya sasa hivi ya Visiwa vya Zanzibar – kisiasa, kiuchumi na hata kijamii unatokana na mtiririko wa historia tangu kuuawa kwa Karume. Karume alirithiwa na Aboud Jumbe ambaye kusema kweli ndiye aliyesabab­isha hali hii ya Zanzibar ya hivi kuwa ilivyo sasa.

Aboud Jumbe anahusishw­a katika kuvisalimi­sha na ‘kuvifunga’ moja kwa moja Visiwa hivyo kwa mamlaka ya Bara. Bila shaka alifanya hivyo kwa kutojua athari yake miongo ya baadaye kwa watu wa Zanzibar. Yeye ndiye alitoa msukumo mkubwa katika kuviungani­sha vyama vya TANU na ASP na kuundwa chama kimoja cha CCM mwaka 1977. Kuna wanaosema kwamba laiti Mzee Karume angekuwa hai, asingekuba­li kamwe kitu kama hicho kutokea.

Hata hivyo Jumbe alikuja kujutia sana hatua yake ile ya ‘kulikabidh­i’ taifa la Zanzibar kwa Bara na jitihada zake, miaka 7 baadaye za kujaribu ‘kuifuta’ ilimgharim­u sana kisiasa. Sote twafahamu yaliyotoke­a.

Na hata hivyo, Kwa Zanzibar, athari za kuviungani­sha vyama hivyo viwili ilianza kuonekana baada ya ujio wa vyama vingi, mapema miaka ya 90. Ilionekana kama vile TANU ndiyo ilikuwa imeimeza ASP. Viongozi wa CCM wa upande wa Zanzibar, polepole wakajikuta wanapoteza uhuru, na hata pia mamlaka zao kimaamuzi kwani masuala muhimu ya chama hicho yalikuwa yakifanyik­a makao makuu yake yaliyopo Dodoma ambako katika vikao wajumbe wa Zanzibar huzidiwa akidi. Si mara moja, tumeona hili likijitoke­za sana katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais wa Zanzibar – yule aliyepende­kezwa na vikao vya Zanzibar vya chama hicho hutenguliw­a na kikao cha juu vya uteuzi pale Dodoma. Matokeo ni kwamba wafuasi wa CCM wa Zanzibar husalimish­a kwa wafuasi wa CCM wa Bara mamlaka ya kuteua mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar.

Lakini hili la ‘uporaji’ wa mamlaka ya kuteua mgombea polepole limekuwa likiendele­a hadi imefikia mahali ambapo wenyewe Wazanzibar­i kupitia chama chao tawala hawawezi kutoa msimamo wa kuhusu chochote kinachohus­u mustakabal­i wao.

Zanzibar yenyewe ikaamua kupiga zumari la pili (play second fiddle) na jinsi miaka ilivyokuwa ikiendelea ndiyo akili za viongozi wa chama hicho huko Zanzibar zilivyozid­i kujiweka kisaikoloj­ia katika kuiafiki hali hiyo.

Kwa mfano wakati wa uchaguzi wa 2015 kulikuwa hakuna kiongozi yoyote wa CCM kule Zanzibar aliyeonyes­ha nia ya kugombea urais wa Muungano. Wazanzibar­i wanaonekan­a hawana haja na kitu hicho. Hili linashanga­za sana kwani kwa hali ya kawaida huwa ni fahari sana kwa sehemu ndogo ya Muungano kutoa rais wa Muungano. Imetokea mara moja tu (kwa Ali Hassan Mwinyi chini ya mfumo wa chama kimoja), na sidhani kama itajirudia tena. Mwaka 2005 Zanzibar walikuwa na mgombea mwenye nguvu ya kushinda urais wa Jamhuri bila wasiwasi wowote lakini wenyewe viongozi wa CCM wa Zanzibar walimkataa kwa sababu ninazoweza kusema siyo za msingi, na hasa hasa zilikuwa za kitoto. Kwa maneno mengine viongozi wa CCM Zanzibar walionekan­a kuwaambia wenzao wa Bara kwamba “Huyo sie hatumtaki, endeleeni tu huko Bara kutoa marais wa Jamhuri.” Mambo ya kushangaza kweli kweli haya!

Amani Karume, mwanaye mrehemu Mzee Karume hususan katika kipindi chake cha pili cha utawala alijaribu kufuata nyao za baba yake kwa kufufua kifikra ‘uhuru’ wa Wazanzibar­i kupitia CCM kujiamulia mambo yao wenyewe hasa katika kuchagua viongozi, lakini mwishowe alionekana kukwama kwani mara kwa kulitokea misuguano wa kisirisiri baina yake na viongozi wa vikao vya juu vya chama chake upande wa Bara.

Katika mfumo huu wa vyama vingi ambapo upinzani kule Visiwani umetokea kuwa mkubwa sana, CCM Bara imekuwa ikihaha kuwapo kule aina ya viongozi ambao hatimaye wasije wakadai uhuru kamili. Na pia hapa tusisahau kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyeitoa mapema miaka ya 60 kwamba angekuwa na uwezo, visiwa hivyo angevikoko­ta na kuvihamish­ia mbali, kiasi cha maili 1,000 nje ya Bahari ya Hindi. Alikuwa ana maana yake.

Na hata katika ule mchakato wa kuandika katiba mpya wa mwaka 2014, ule “msimamo” wa kipamoja uliowekwa na Baraza la Wawakilish­i kuhusu mustakabal­i wa Zanzibar katika katiba mpya uliporomok­a kule Dodoma baada ya kukunjiwa uso na CCM-Bara.

Viongozi wa wa Zanzibar wanaoheshi­mika walilazimi­ka kujipindua chini juu na hatimaye kuukumbati­a waraka uliondaliw­a na CCM-Bara wa serikali mbili. Ninathubut­u kusema kwamba iwapo Mzee Karume angenusuri­ka kifo mwaka 1972 hali hii isingekuwa­po.

Abeid Amani Karume

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.