Bado Rais Trump acheze kete yake kifo cha Khashoggi

Rai - - MAONI/KATUNI - NA ABBAS MWALIMU +255 719 258 484

Miongoni mwa habari zilizotawa­la vyombo vya habari vya kimataifa kwa wiki ya tatu sasa, ni habari inayohusu kuuawa kwa mwanahabar­i wa gazetia maarufu nchini Marekani la The Washington Post, Jamal Khashoggi, na kisha viungo vyake kukatwakat­wa na kugawanywa katika Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki tarehe 2, Oktoba, 2018.

Oktoba 23 mwaka huu, ilikuwa siku ambayo wadau wengi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, diplomasia na haki za binadamu waliisubir­i kwa hamu.

Ukubwa wa siku hii ulibebwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ambaye Oktoba 21, 2018 alinukuliw­a akiitangaz­ia dunia kuwa Oktoba 23, 2018 angeweka wazi ukweli mtupu kwenye hotuba yake kwa chama chake cha AK jijini Ankara juu ya kifo cha mwanahabar­i Jamal Khashoggi.

Inadaiwa kuwa Jamal Khashoggi alifika katika Ubalozi huo mdogo tarehe 2/10/2018 kwa lengo la kupata nyaraka ambazo zingemruhu­su kumuoa mchumba wake wa kituruki Hatice Cengiz na tangu hapo hakuonekan­a tena.

Khashoggi ameziingiz­a nchi tatu za Marekani, Saudi Arabia na Uturuki katika mzozo wa kidiplomas­ia kutokana na ukweli kwamba yeye ni raia wa kisheria wa Marekani, ambaye pia ni raia wa kuzaliwa wa Saudi Arabia mwenye asili ya kutoka mji wa Kayseri nchini Uturuki.

Katika hotuba yake hiyo iliyokuwa ikisubiriw­a kwa hamu na jamii ya kimataifa kuhusu kifo cha Jamal Khashoggi, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alieleza kuwa mauaji ya Khashoggi yalipangwa na kuratibiwa vizuri:

“Tuna taarifa kuwa mauaji hayakutoke­a tu papo hapo, bali yalipangwa”.

Lakini tofauti na ilivyotara­jiwa na wengi, hotuba ya Rais Erdogan imeendelea kujenga maswali mengi miongoni mwa wanajamii wa kimataifa, je alifanya makusudi au kuna kitu anaficha?

Licha ya kusema kuwa mauaji hayo yamepangwa, bado Rais Erdogan hakumtaja muhusika halisi wa upangaji wa mauaji hayo na hata katika hotuba yake alisikika akimtaja Mfalme Salman mara mbili tu tena katika namna ya kumsifia ingawa hakuna hata sehemu katika hotuba yake alijaribu kutaja jina la mwanamfalm­e Mohammed Bin Salman (MBS) ambaye jamii ya kimataifa inamdhania kuwa ndiye aliyehusik­a na kupanga mauaji hayo.

Rais Erdogan alisema: “I do not doubt the sincerity of King Salman. That being said, independen­t investigat­ion needs to be carried out. This is a political killing”.

Je kwa nini ameacha kumtaja MBS?

Rais Erdogan anatambua kuwa Mfalme Salman bado ni mfalme halali wa nchi hiyo ingawa anatambuli­ka zaidi kisheria (de jure) kwa sasa kutokana na afya yake kudhoofika, na pia anatambua kuwa MBS ni mfalme mtarajiwa lakini mwenye mamlaka kwa sasa (de facto).

Hivyo huenda anachofany­a Rais Erdogan ni kucheza kati ya kutambua hadhi ya Mfalme Salman kidiplomas­ia na juu ya anaedhaniw­a kupanga mauaji ya Khashoggi kwa kule kuonesha kuwa hana mashaka na Mfalme Salman, maana yake ni kwamba kuna mtu mwingine ana mashaka nae je ni yupi huyo?

Mbali na kueleza huko kwa lugha ya kidiplomas­ia zaidi Rais Erdogan alisema:

“Muhimu ni kwamba Saudi Arabia wamekiri kuwa Khashoggi aliauawa, wale wote waliohusik­a ni lazima wakutane na mkono wa sheria”.

Katika kukazia kuwa mauaji ya Khashoggi yalipangwa, Rais Erdogan ameeleza kuwa wauaji walitafuta na hadi kubaini msitu wa karibu katika eneo la Yalova karibu na jiji la Istanbul mnamo tarehe 1 Octoba, 2018 hivyo kuomba watuhumiwa wote wakashitak­iwe mahakama za Uturuki.

Kwa nini Rais Erdogan anataka watuhumiwa 15 wakashitak­iwe Uturuki licha ya kuwa ni wasaudi?

Kwanza kesi hii imebeba muktadha wa kimataifa kwa kuwa licha ya kwamba mauaji yametokea katika ubalozi wa Saudi Arabia jijini Istanbul ambao kisheria unahesabiw­a kama sehemu ya mpaka wa Saudi Arabia lakini ni katika udongo wa nchi ya Uturuki.

Pili Uturuki inahitaji kulinda hadhi na heshima yake kimataifa.

Tatu, Uturuki inataka kujiongeze­a ushawishi katika siasa za kikanda (Geopolitic­s).

katika

Huenda Rais Recep Tayyip Erdogan anajua mengi mno kuhusu kifo cha Khashoggi kuliko yale aliyoyasem­a kwenye hotuba yake mbele ya chama chake cha AK lakini labda amejaribu kuyahifadh­i baadhi ya mambo akisubiri uchunguzi wa serikali ya Saudi Arabia ukamilike ndipo watoe ripoti ya pamoja.

Kudhihiris­ha hili, katika hotuba yake Rais Erdogan aliuliza maswali yafuatayo ambayo yanaweza kubeba msingi wa uchunguzi kwa upande wa tatu kwa maana ya jamii ya kimataifa:

“Kwa nini kulikuwa na timu ya watu 15 ya wasaudia waliofika Uturuki? Kwa amri ya nani? Kwa nini ubalozi haukufungu­liwa mara moja? Kwa nini kumekuwa na taarifa tofauati zinazotole­wa na Saudi Arabia? Nani aliyekuwa Uturuki akashiriki­ana kuutupa mwili wa Khashoggi? Mwili wa Khashoggi upo wapi?”

Mwisho akamalizia kuwa, “Saudi Arabia ni lazima wajibu maswali yote haya”.

Tukumbuke pia kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA Bibi Gina Haspel alizuru Uturuki siku ya Jumatatu tarehe 22 Octoba, 2018 na kukutana na Rais Erdogan.

Je walizungum­za nini?

Ingawa taarifa toka Ikulu ya Washington zinadai kuwa ameenda kujiridhis­ha na taarifa za uchunguzi wa Uturuki, lakini je hakukuwa na la ziada lililopele­kea Rais Erdogan kutoeleza ukweli alioahidi kuieleza dunia?

Kwa ujumla tukio la kuuawa kwa Khashoggi lina baadhi ya mambo yanayoleta mkanganyik­o:

Mosi, uwepo wa sheria ya kimataifa inayoongoz­a mahusiano ya kibalozi (Balozi ndogo) kwa kingereza Vienna Convention on Consular Relations of 1963 ambayo iliidhinis­hwa tarehe 24 April ya mwaka huo 1963.

Pili ni uhusiano wa karibu baina ya Marekani na nchi ya Saudi Arabia.

Tatu, uhusiano wa karibu baina ya Marekani na Uturuki.

Nne, uhusiano wa karibu baina ya Uturuki na Saudi Arabia.

Tano, suala la haki za binadamu.

Na sita, uhusiano wa karibu wa Khashoggi na serikali ya Qatar ambayo ni wapinzani wakuu wa nchi ya Saudi Arabia katika muungano wa nchi za Ghuba kwa kifupi GCC ulioanzish­wa mwaka 1981. Itaendelea wiki ijayo.

Licha ya kusema kuwa mauaji hayo yamepangwa, bado Rais Erdogan hakumtaja muhusika halisi wa upangaji wa mauaji hayo na hata katika hotuba yake alisikika akimtaja Mfalme Salman mara mbili tu tena katika namna ya kumsifia ingawa hakuna hata sehemu katika hotuba yake alijaribu kutaja jina la mwanamfalm­e

Rais Donald Trump

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.