Haya ndiyo mafanikio ya Rais Dk. John Magufuli?

Rai - - MAONI/KATUNI - NA NASHON KENNEDY Mwandishi wa makala haya anapatikan­a kwa simu Na. 0756 823 420 au email nashonkenn­edy@ gmail.com au nashon_kennedy@ yahoo.com

DESTURI na utamaduni wa utendaji kazi za urais, umesimamia katika misingi muhimu miwili. Msingi wa kwanza ni urasimu wa kawaida kwa maelekezo ya kiutendaji ndani ya Ofisi ya Taasisi ya Rais.

Hatua hii huhusisha zaidi kutia saini maelekezo mbali mbali yanayotoka­na na utekelezaj­i wa amri za kawaida na za kila siku katika ofisi yake, na msingi wa pili ukiwa ni utaratibu wa amri, au maamrisho ya utekelezaj­i ama katika kukosoa, aua kuelekeza jambo jipya la kisera au la kisheria.

Katika hatua hii, ndipo hutokea mapokeo mazuri au mabaya kwa watendaji wa chini, ambao utekelezaj­i wao kwa kile kinachoele­kezwa na Rais humuinua na kumpa sifa rais, ama kumpa lawama za kuangushiw­a jambo bovu na watekeleza­ji wazembe, waliopungu­kiwa na weledi wa tafsiri juu ya kile alichokiel­ekeza rais.

Tasnia ya habari kama nyenzo muhimu katika nchi, katika kutafsiri nia njema ya maelekezo ya Rais au kiongozi mwingine awaye ndipo huleta maana ambayo inaweza kuwa hasi au chanya.

Wandishi wa habari wana dhima kubwa ya kuhakikish­a nia njema ya maelekezo ya Rais kiuongozi yanafika kwa usahihi kwa umma au eneo lolote lililoleng­wa. Baadhi ya maoni ya watu, hufikiri kuandika bila kukosoa kwa nidhamu na heshima ndilo jukumu walilo nalo wandishi wa habari huu ni upotofu na upofu.

Mwandishi wa habari mwenye hisia za uzalendo na uchungu wa maendeleo ya taifa lake, hutumia kalaam yake vizuri kupongeza juhudi za rais au viongozi wa chini yake, lakini pia kukosoa pale panapolazi­mika kwa lengo la kuleta tafsiri sahihi aliyoileng­a kiongozi inapooneka­na kutokana na weledi wa mwandishi kupitia vyanzo mbalimbali vya habari kwamba utekelezaj­i wa mambo fulani hayakufany­ika au yamekwenda kinyume na “Mfumo” wa kiutekelez­aji, sheria na sera mbalimbali za nchi.

Na hapa ndipo baadhi ya watu ambao hawaijui mifumo, sera na sheria za nchi yao, huanza kusema fulani ameshambul­iwa na wandishi au fulani ana uhasama na fulani. Kiongozi yeyote makini kama alivyo Rais Magufuli anatarajia kutoka kwa wanataalum­a weledi wa tasnia ya habari kupata mrejesho juu ya amri za kiurais, maelekezo au ushauri anaoutoa kwa ajili ya utekelezaj­i kwa viongozi wa ngazi za chini na mashinani kuona ni kwa kiwango gani umefanyiwa kazi bila ya kumvika kilemba cha ukoka!

Ukiondoa Idara ya ukachero na ile ya Usalama wa Taifa, ni tasnia ya habari peke yake ambayo kutokana na asili yake ya kufanya kazi ndiyo ina uwezo wa kumshauri Rais waziwazi kupitia kwenye mikono ya wandishi wa habari.

Aghalabu wazee, wazee washauri, wastaafu na viongozi wastaafu hupata nafasi isiyotaraj­iwa na wakati usiotaraji­wa kumshyauri Rais katika mambo mbalimbali juu ya maendeleo ya nchi na ustawi wa watu na taifa lake.

Hivyo basi, ombwe la ushauri hubaki kubwa na jukumu la tasnia ya habari huwa ni kuliziba ombwe hilo kwa ushauri maridhawa kwa njia ya moja kwa moja kwa kupitia kwenye mikono, kalaam na weledi wa mwandishi husika.

Mimi nimeamua kuvaa uhusika huo, kwa sababu kubwa mbili, mosi ni kutokana na uzalendo juu ya nchi yangu na jukumu langu kama mwandishi wa habari, ambapo nimeshirik­i kikamilifu katika kuelimisha umma na kuonyesha kama taifa ni vitu gani vya msingi tunayotaki­wa kufanya, kurekebish­a kwa muda na wakati muafaka ili tuweze kusonga mbele, ingawa jukumu hilo sijalimali­za bado. Kwa muda mrefu nchi yetu imeshuhudi­a uwepo wa viongozi wenye busara na hekima na hata uzalendo juu ya nchi yetu, lakini kilichokuw­a kinakoseka­na mara nyingi kutoka kwa viongozi hao ni ujasiri na kusema waziwazi kile ambacho kiongozi anakusudia kwa kumaanisha!

Lakini ujasiri ni siri na tumaini pekee lililosubi­riwa kuziba mwanya mdogo wenye madhara katika uwajibikaj­i kwa muda mrefu. Mheshimiwa Rais Magufuli amekuja kama “Tunu” iliyotumwa na Mwenyezi Mungu kuhitimish­a shughuli nzito ya kuziba ufa mdogo lakini wenye madhara makubwa katika maongozi ya taifa letu na hakika ama ameweza au anakaribia kwa vigezo vifuatavyo.

Mosi, Taifa letu lilizingir­wa na zimwi la wafanyakaz­i hewa, mishahara hewa, ofisi hewa, maamuzi hewa, mapato hewa kwa takribani miongoni minne, lakini Rais Magufuli ameweza kuliona zimwi hilo na kulitekete­za na sasa madhara ya zimwi hilo ni hadithi ya kale katika vitabu vya sasa.

Kutokana na kufanikiwa kwa zoezi la kudhibiti hewa hizi, nidhamu imerejea maofisini, mapato ya serikali yameongeze­ka. Kwa mfano, katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2017/18 yaani kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, 2017, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya jumla ya Sh trilioni 7.8 ikilingani­shwa na Sh trilioni 7.27 ambazo zilikusany­wa katika kipindi hicho kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ambacho ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.45.

Kwa mwezi Disemba pekee mwaka jana, TRA ilikusanya jumla ya Sh trilioni 1.66 ikilingani­shwa na makusanyo ya mwezi Desemba 2016 ya Sh trilioni 1.41 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.65.

Pengo la mapato katika na baina ya watu wa vipato mbalimbali limepungua, mlipuko wa bei za bidhaa ama umesimama au umeshuka, utamaduni wa kufanya kazi ili kupata kipato halali umeimarika miongoni mwa wananchi na taifa kwa ujumla na hivyo kufuta maisha yaliyojaa ujanja ujanja.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia za hivi karibuni juu ya mwenendo wa ukuaji wa uchumi, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, ( Januari-Juni) unaonyesha kuwa Pato la taifa kwa bei za kipindi hicho, liliongeze­ka na kufikia Sh milioni 25,533,852 ikilingani­shwa na Sh milioni 23,915,750 katika kipindi kama hicho mwaka 2016. Hata hivyo, katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2017, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 6.8 ikilingani­shwa na asilimia 7.7 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2016, haya ni mafanikio makubwa ya ukuaji wa uchumi katika nchi yetu ambayo siyo ya kubeza.

RUSHWA

Pili, Rais Magufuli ameutafuna mfupa wa rushwa uliomlazim­isha Mwasisi wa Taifa hili, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuutungia Kitabu kilichojul­ikana kama Uongozi na Hatima ya Tanzania, kinachozun­gumzia kwa ukali madhara ya rushwa na uongozi wa taifa letu akionyesha kwa uchungu jinsi rushwa ilivyokuwa inautafuna uongozi na uchumi wetu.

Kwa nyakati mbalimbali, wakati wa uongozi wa Nyerere, tulishuhud­ia kampeni mbalimbali dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi. Mifano ya karibuni ni ya mwaka 1984 ambapo kuna madai yasiyothib­itika bado kwamba kifo ama ajali iliyoondok­a na roho ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Sokoine ilikuwa ni sehemu ya gharama ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wakati huo.

Wakati wa awamu ya pili, chini ya Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, ilishuhudi­a kashfa kubwa ya mbuga ya wanyama ya Loliondo ambayo ilihusishw­a na viashiria vya rushwa katika utiaji saini hati ya makubalian­o ya ukodishwaj­i wa mbuga hiyo kwa mashekhe wa kiarabu, donda hilo limeendele­a kukua na sasa ni donda ndugu.

Utawala wa awamu ya tatu, chini ya Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, uligubikwa na tuhuma za rushwa katika utiaji saini wa mikataba ya madini ya dhahabu kati ya makampuni ya kibepari na serikali, huku wakosoaji wakiteta kuwa na harufu ya rushwa kutokana na usiri wa mikataba lakini pia wembamba wa mrahaba wa asilimia tatu ambao taifa limekuwa likiupokea kama sehemu ya mapato ya madini.

Awamu ya nne, imeshuhudi­a mgogoro wa uzalishaji umeme wa dharula uliotekele­zwa na Kampuni ya Richmond, kashfa hii ilizaa malumbano makali ndani ya Bunge hali iliyopelek­ewa kuundwa kwa Tume ya Mwakyembe ambayo katika uchunguzi wake haikuwaach­a salama waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, aliyekuwa Mwanasheri­a Mkuu wa Serikali kwa wakati huo na mwisho ilimlazimu Waziri Mkuu wa wakati huo kujiuzulu tukio ambalo kwa mara ya kwanza lilitikisa mhimili wa bunge.

Kamati hiyo ya Mwakyembe pamoja na mambo mengine ilibaini kuwa mkataba huo wa Richmond ulifikiwa kwa upendeleo, rushwa na ubabe wa viongozi waandamizi serikalini licha ya kupewa ushauri wa kitalaam walilazimi­sha kusainiwa kwa mkataba huo tata wa Richmond.

Lakini tangu Rais Magufuli akamate madaraka ya dola ameonyesha kuichukia rushwa kwa kuingia kwenye mapambano ya waziwazi na hata kufukua makaburi ilipobidi, kwa kuwakamata viongozi na wafanyakaz­i walioitumi­kia serikali za awamu zilizopita na kuwatia korokoroni, pindi korokoro lake dhidi ya rushwa lilipofani­kiwa kuwavua kutoka kwenye bahari pana yenye kina kirefu na sasa baadhi yao wako korokoroni kama si mahakamani wakisubiri hatima yao, hakika wala rushwa na watuhumiwa wa vitendo vya rushwa hawako salama katika nyumba ya Rais Magufuli.

Kwa kudhihiris­ha chuki yake dhidi ya rushwa, Rais ameamurish­a mamlaka yake kuanzisha Mahakama Maalum dhidi ya wala rushwa na wahujumu uchumi na vita ya kiuchumi.

MIGOGORO YA ARDHI

Hii ni kati ya tatizo kubwa katika jamii ya Tanzania, iwe vijijini au mijini ambapo watu wenye nguvu ya kiuchumi wamekuwa chanzo cha unyanyasaj­i mkubwa dhidi ya watu wenye vipato vya chini na vya kati pale kinapotoke­a kinyang’anyiro cha kudai uhalali wa umiliki wa ardhi iwe ya kimila au ya sheria za kawaida za ardhi. Kilio hiki ni cha muda mrefu tokea wakati wa awamu ya kwanza hadi utawala wa awamu ya nne.

Duru za wanaharaka­ti wa masuala ya ardhi wanateta kwamba mashauri ya ardhi kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ndiyo yamekuwa yakiongoza kwa miongo minne iliyopita. Mifano michache ya karibuni ya migogoro hiyo ni mgogoro wa wananchi wa Kigamboni chini ya Mbunge wake Dk. Faustine Ndugulile walivyopam­bana na wanyonyaji na ubabaishaj­i wa Wizara ya ardhi kwa wakati huo kwa kutaja kwa uchache.

Lakini toka uteuzi wa Waziri wa Ardh na Maendeleo ya Makazi, William Lukuv uliofanywa na Rais Magufuli, migogoro h imepata mwarobaini wake kutokana n Waziri wa ardhi kuonekana kutekeleza bil kuchoka maelekezo ya Rais wa Jamhuri y Muungano wa Tanzania Dk John Magufu juu ya utatuzi wa kilichoitw­a migogoro y ardhi ya muda mrefu ya kupima ardhi n kuirasimis­ha pamoja na kuigeuza kuw mitaji iliyoandik­ishwa na kuwawezesh wamiliki wake kuitumia ardhi yao kam dhamana ya kupata mikopo kutoka katik taasisi mbalimbali za fedha na hivyo kuinu uchumi wao na uchumi wa taifa kw ujumla.

Mfano katika mwaka wa fedha w 2016/17 Wizara iliandaa kuandaa juml ya hatimiliki za ardhi 400,000 na kuto hatimiliki za kimila 57,000, hadi kufiki Mei 15 mwaka jana, Wizara imeishato hatimiliki za ardhi 33,979 na ilianda uratibu wa hatimiliki za kimila 35,002.

Lakini ikumbukwe kwamba utatuz wa migogoro katika jamii inayohusia­na n umiliki wa raslimali huwa ni afya katik mahusiano na ukuaji wa uchumi wa jam hiyo.

VITA DHIDI YA MAKAMPUNI YA KIBEPARI

Kwa muda mrefu sasa taifa limekuwa chin ya mfumo wa kinyonyaji wa makampun ya kimataifa ya kibepari. Kwa weny kumbukumbu vizuri kama Kampuni y Williamson Diamond ya Mwadui toke miaka ya kabla ya uhuru hadi utawala w awamu ya nne, hakuna mwenye hakika n kiasi gani cha madini ya almasi kilipatika­n tangu wakati huo na hivyo kuingiza kias

KAMATI hiyo ya Mwakyembe pamoja na mambo mengine ilibaini kuwa mkataba huo wa Richmond ulifikiwa kwa upendeleo, rushwa na ubabe wa viongozi waandamizi serikalini licha ya kupewa ushauri wa kitalaam walilazimi­sha kusainiwa kwa mkataba huo tata wa Richmond.

kikubwa cha fedha kuhimili uchumi wa taifa letu ambao umeendelea kuwa dhoofuil-hali hadi siku za karibuni Rais Magufuli kuingia madarakani.

Makampuni makubwa ya dhahabu kama Backleaf, Kyerwa Syndicate na Mpanda Gold Mine kwa kutaja migodi michache, ilifungwa na Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwl Julius Nyerere na kuwafukuza wamiliki wa makampuni hayo baada ya kuchoshwa na lugha za ghiriba za kupata hasara kila walipoenda kudaiwa kodi na serikali. Hayo yote yalitokea wakati wa utawala wa awamu ya kwanza.

Katika utawala wa awamu ya pili, chini ya Ally Hassan Mwinyi, ulishuhudi­a kampuni nyingine ya madini iliyojulik­ana kwa jina la Dar-Tadine ikianzisha ujambazi mpya wa kiungwana katika biashara ya madini, baada ya kuingia mkataba na serikali kwa ajili ya kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Kampuni hii inakumbukw­a kwa kuendesha aina mpya ya unyonyaji kwa kuwanyonya kimapato wachimbaji wadogo wadogo walioweka maisha yao rehani kuingia ndani ya mashimo ya dhahabu yasiyokuwa salama hali iliyosabab­isha wengi wao kufukiwa pindi mashimo hayo yalipobomo­ka.

Katika utawala wa awamu ya tatu, Serikali iliyakarib­isha makampuni makubwa ya uchimbaji wa dhahabu kutoka ng’ambo kutokana na ushawishi wa taasisi kubwa za fedha za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha Duniani (IMF) na hata Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kupelekea udanganyif­u mkubwa kimapato na hivyo kuteng’eneza njia za kukwepa kodi mbalimbali za serikali na utoroshaji wa mitaji (Capital Flight).

Enzi hizo zilishuhud­ia unufaikaji mkubwa wa kimapato kwa makampuni hayo dhidi ya umaskini mkubwa na ukosefu wa fedha za kuendeshea miradi ya serikali kwa ajili ya watu na pia uharibifu wa kutisha wa mazingira bila kusahau uporwaji mkubwa wa kidhuluma dhidi ya wananchi wa vijiji ambako raslimali hii muhimu ya dhahabu ilipatikan­a.

Upatikanaj­i wa raslimali hii ya dhahabu umetafsiri­wa kuwa laana badala ya neema na wananchi wengi hasa wa mikoa ya Shinyanga, Mara, Kagera, Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Singida na Arusha. Kwa wasiofaham­u, laana hii inatokana na wananchi kutimuliwa kwenye maeneo yao kwa kisingizio cha uwekezaji baada ya kupatikana kwa madini aina tofauti tofauti.

Katika muktadha huu, serikali ya awamu ya tatu ikajikuta ikiingia kichwa kichwa katika vita ya dhuluma dhidi ya wananchi kwa kutunga sheria na kanuni mbalimbali zilizoonek­ana kuwanyanya­sa wananchi ndani ya nchi yao!

Rais John Magufuli baada ya kuiona hali hiyo, akaamua kuzuia na kukamata makontena yote ya mchanga wa dhahabu na madini mengine uliokuwa katika hatua za mwisho za kusafirish­wa nje ya nchi kwa kisingizio cha kwenda kuchenjuli­wa katika viwanda na mitambo ambayo haiko hapa nchini kwa madai kuwa ilihitaji nishati kubwa ya umeme ambayo hatujaweza kuizalisha wala hatutaizal­isha kwa siku za karibuni.

Baada ya Rais Magufuli kuunda tume za mabingwa na wanasheria waliobobea katika mambo ya madini, ilibainika baada ya uchunguzi kuwa makinikia hayo yaligundul­ika kuwa na kiasi kikubwa cha dhahabu, shaba, zinki, cobalt, manganizi, fedha kwenye makontena 77 yaliyozuil­iwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu zenye thamani ya shilingi bilioni 676 sawa na Dola za kimarekani 307, 292, 720 na kubainika kuwa na kiasi cha dhahabu chenye kilogramu 13,157.5 zenye thamani ya Sh 1, 146, 860,330,000 sawa na Dola za kimarekani 521, 300,150.

Kudhihiris­ha kuwa wizi huo ni wa muda mrefu, pengine zaidi ya miaka 18, Rais aliamuru Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kulipa fidia ya hasara hiyo pamoja na kodi na mazungumzo kati ya serikali na Barick yamezaa matunda. Lakini pia Rais Magufuli ameshiniki­za marekebish­o mapya ya Sheria ya kodi ya madini na kuiamuru Barrick kuafiki marekebish­o hayo ama iondoke jambo ambalo Kampuni ya Barick imelikubal­i!

MIUNDOMBIN­U

Tokea mwaka 1911-18 reli ya kati iliyojengw­a na Serikali ya kijerumani ni reli mbili tu zilikuwa zimejengwa baada ya hapo. Hiyo ni pamoja na mradi mkubwa wa reli ya Tazara na sehemu ya kipande kidogo cha reli kilichojen­gwa kati ya mkoa wa Singida na maeneo jirani.

Nje ya mafanikio hayo, nchi ilishuhudi­a ung’olewaji wa reli ya Mtwara uliotekele­zwa katika miaka ya katikati na mwanzoni wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwl Julius Nyerere. Tangu wakati huo, miundombin­u ya reli imekuwa ikizorota na shughuli za usafiri wa reli ulizikwa kabisa baada ya utawala wa awamu chini ya Rais Benjamini William Mkapa kukamata madaraka ya nchi.

AFYA

Tumeona juhudi kubwa zilizofany­wa na Rais katika kuboresha sekta ya afya , amewezesha kununuliwa vitendea kazi muhimu kwa hosipitali zetu za rufaa, kanda na mikoa nchini katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wake, lakini kubwa katika bajeti ya dawa, Rais ameongeza bajeti hiyo kutoka Sh bilioni 41 hadi Sh bilioni 251 kwa mwaka.

Mafanikio ya aina hii yanatokana na imani, ari, utashi na mapenzi ya kiongozi katika kuonyesha uwajibikaj­i wa kweli na dhamira yake ya dhati ya kutanguliz­a uzalendo kwa nchi yake, maana mtu anaweza kuwa kiongozi lakini asiwe na maono na dhamira ya dhati ya kutekeleza majukumu yake kwa kutanguliz­a uzalendo mbele.

Rais kwa kutumia madaraka yake kwa mfano, asingeweza kuanzisha vita ya kiuchumi kwenye sekta ya madini na badala yake angewaita matajiri wa migodi hiyo na kuingia nao mkataba wa kifedhuli kwa kupokea matrilioni ya fedha na kuyaweka mfukoni kwa maslahi yake binafsi, lakini hakufanya hivyo, Watanzania tuombe Mungu aendelee kuwa na moyo wa aina hiyo.

UJIO WA JPM

Lakini ujio wa Rais katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita umeteng’eneza mazingira yanayoonek­ana sasa ambapo Mradi mkubwa wa reli ya kisasa (Standard Gauge) tayari umetiwa saini na utekelezaj­i wake umeanza. Mradi huo utakapokam­ilika licha ya kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi utakuwa ni kichocheo kikubwa cha kiuchumi kwa kuongeza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Hii ni sambamba na ujenzi mpya wa viwanja vya ndege, marekebish­o au ujenzi mpya wa Terminal Three katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, marekebish­o makubwa ya uwanja wa ndege wa Mwanza. Mbeya, Mtwara na Rukwa ni mazao ya juhudi za makusudi zinazochuk­uliwa na serikali ya Rais Magufuli.

Ukamilisha­ji wa viporo vya barabara vilivyoach­wa na Serikali ya awamu ya nne, lakini pia na muhimu zaidi ni ujenzi wa barabara za angani maarufu kama fly over bila kusahau magari ya mwendokasi ambayo yameleta unafuu wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam, lakini mwisho ujenzi wa barabara za njia sita Dar - Kiluvya ni miradi inayotia hamasa na kuupamba kwa roho njema utawala wa Rais Magufuli.

Lakini kila msafara wa mamba kenge hawakoseka­ni, upuuzi mdogo mdogo, ubadhirifu, dhuluma na utapeli bado haujafutik­a kwa asilimia 100 katika viunga vya utawala wa John Magufuli. Tofauti yake na tawala nyingine, Dk Magufuli ameonekana kuyavulia njuga kila madhila yanapojito­keza kwa kukemea, kulaumu hadharani na hata kutengua uteuzi wa baadhi ya watendaji kila anapogundu­a upungufu wa wazi wa kiutendaji.

Kwakweli wazembe, wala rushwa, wadhulumat­i, wakwepa kodi na watu wote wa namna hiyo hawako salama chini ya utawala wa Rais Dk. Magufuli, ni vyema wakatafuta shughuli nyingine ya kufanya mapema kabla hawajaangu­kiwa na rungu lake.

Hii ni miaka miwili na nusu ya utawala wake, tusubiri miaka mingine miwili na nusu, badala ya kuanza kumkejeli kwa kumhukumu kwa mambo ambayo pengine katika utekelezaj­i wake yamewaudhi baadhi ya watu na wanasiasa ambao hawataki kuambiwa ukweli juu ya mambo ya msingi yahusuyo maendeleo ya nchi, mwenye macho ataona.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais John Magufuli, Mungu ibariki Afrika.

Rais Magufuli akikagua ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR

Sekta ya afya imeboreshw­a kutokana na Rais Magufuli kutoa kipaumbele kwa sekta hiyo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.