‘Malaika wa ukombozi’ aliyegeuka kuwa dikteta uchwara

Rai - - MAONI/KATUNI - ITAENDELEA WIKI IJAYO NA MBWANA ALLYAMTU

Mbinu za kiintelije­nsia zilizosukw­a kwa ustadi mkubwa, zilitumika kuifanya Rwanda kuwa uwanja wa damu mapema mwaka 1994. Ustadi huu ulisukwa mapema mwaka 1988 kule Ethiopia na kumalizika pale Enttebe, Uganda, lengo likuwa ni kuingia Kongo- DRC kwenda kujinyakul­ia mali bila vizingiti vyovyote.

Hawakujua kuwa mpango ule ungeleta

madhara makubwa, kama ilivyokuja kutokea usiku wa Aprili 6, 1994 mpaka Mei 15, 1994 kwa kutapakaa kwa maiti nchi nzima. Mpango mkakati ulikuwa ni kumuondoa Idd Amini kule Uganda na kuweka kibaraka wao, mpango ambao ulitimia tarehe 26/10/1986 kwa kupachikwa Museveni kupitia usaidizi uliofanywa na Tanzania kwa karibu kabisa.

Mpango mpya ni tutaingiaj­e Rwanda? Mkakati huu ulikuwa wa kufurumish­a utawala wa mtoto wa ubatizo wa Mobutu Seseseko, aliye fahamika kama Juvenal Habyrimana. Mwanzoni mwa mwaka wa 1990, kuliundwa chama cha RPF chini ya kiongozi wa Major General, Fredy Gisa Rwigema, aliyejarib­u kuivamia Rwanda mwaka huo huo bila mafaniko, kwani aliambulia kipigo kikali kutoka vikosi vya askari wa Rwanda wakisaidiw­a na vikosi vya ZDF kutoka Zaire ya Mobutu.

Baada ya kukwama kwa njia hii mpango mkakati ulipanuliw­a zaidi kwa Kagame aliyekuwa masomoni huko Marekani kurejeshwa kwa lengo la kuongoza kikosi cha wanamgambo wa RPF lengo ni kutekeleza operation ya siri (iliyofichi­ka sana mpaka leo) kwa kuzishilik­isha nchi kadhaa ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na Ethiopia. Ambapo kupitia mkakati huu ilifanikis­ha Kagame kujinyakul­ia utawala kwa wepesi.

Wakati wa utekelezaj­i ulioratibi­wa na mataifa ya magharibi yakiongozw­a na Marekani na Uingereza pamoja na washirika wao kutia ndani Ufaransa na Ubeligiji mkakati huo unabaki kuwa nyakati isiyo saulika kamwe nchini Rwanda kwani maiti zisizo na hatia za makabila ya kitusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa na maiti zao kutapakaa kwenye mitaa huko Rwanda na zingine kutupwa kwenye mto Ruvuvu unaoepelek­a maji yake kwenye mto Kagera.

Habyimana ndio chanzo cha machafuko hayo yote ya kimbari huko Rwanda na hii ni baada ya ndege iliyokuwa imembeba kutunguliw­a na watu wasiojulik­ana (bado kuna vuta ni kuvute ya nani hasa alihusika) wapo wanaomtuhu­mu Kagame na kikosi chake cha RPF kuhusika jambo ambalo Kagame mwenyewe hukanusha.

Ilikuwa saa 2:20 usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, ndege ya shirika la Ubelgiji C-130 Hercules, iliyokuwa ikipaa kila wiki, ikiwa imebeba kikosi cha askari wa umoja wa Mataifa cha UNAMIR, ilisubiris­hwa angani ili ndege ya Rais iweze kutua kwanza katika uwanja wa ndege wa mjini Kigali.

Ndani ya ndege hiyo ya Rais walikuwamo; Rais wa Rwanda, Juvénal Habyariman­a, Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira, Waziri wa kazi wa Burundi, Bernard Ciza, Waziri wa mawasilian­o wa Burundi, .Cyriaque Simbizi, Mkuu wa utumishi jeshi la Rwanda, Meja Generali Déogratias Nsabimana, Mkuu wa kikosi cha “maison militaire” cha Rais wa Rwanda, Meja Thaddée Bagaragaza, Mjumbe wa sekretarie­ti maalum ya Rais wa Rwanda na mkuu wa baraza la kijeshi la Rais wa Rwanda.

Wengine ni Kanali Elie Sagatwa, Mshauri wa masula ya kigeni wa Rais wa Rwanda, Juvénal Renaho, Daktari binafsi wa Rais wa Rwanda, Emmanuel Akingeneye, Jacky Héraud, Rubani (raia wa Ufaransa), Jean-Pierre Minaberry, Rubani msaidizi (raia wa Ufaransa), Jean-Michel Perrine (Injinia wa ndege, raia wa Ufaransa)

Wakati ikijiandaa kutua, makombora mawili ya kurushwa kutoka ardhini yalikatish­a maisha ya watu hao 12 waliokuwam­o ndani ya ndege hiyo aina ya Jet-Dassault Falcon. Kombora la kwanza likipiga ubawa mmoja wa ndege na kombora la pili likapiga mkia, kisha ndege hiyo ikiwa inawaka moto iliangukia kwenye bustani ya ikulu ya Rais.

Tukio hilo likawa mwanzo wa machafuko yaliyopele­kea mauaji ya wanyarwand­a zaidi ya 800,000 kwa siku 100 pekee. Maana yake kila siku walikufa watu 8000.

Wanamgambo wa kihutu, walioitwa “Intarahamw­e” wakisaidiw­a na wanajeshi wa kihutu walitumia silaha za jadi kuwaua watu wa kabila la Watutsi. Machafuko haya yaliibuka tu baada ya kuuawa kwake Hbyarimana, rais wa pili wa Rwanda wakati huo aliyechuku­a madaraka mwaka 1973 kwa mapinduzi baridi kutoka kwa Gregory Kayibanda aliyekuwa rais wa kwanza wa Rwanda.

Juvenal Habyimana ambaye ndie atakaye sadifu makala yangu hii ya leo ni rais wa pili wa Rwanda aliyetoka kabila la kihutu, aliingia rasmi madarakani Julai 5, mwaka 1973. Kabla ya hapo alikuwa ni Jenerali katika jeshi la Rwanda akishikili­a cheo cha Mnadhimu Mkuu wa jeshi kwenye serikali mpya iliyokuwa ikiongozwa na Gregory Kayibanda. Mapinduzi yaliyofany­wa na Habyariman­a kumuondoa madarakani Rais Gregoire Kayibanda hayakuwa mapinduzi ya kumwaga damu.

Mapinduzi haya yalipokele­wa kwa shangwe na vifijo hasa maeneo ya mijini nchini Rwanda. Rais aliyepindu­liwa, Kayibanda ilifika kipindi alianza kuchukiwa mno na wananchi kutokana na kushindwa kabisa kuituliza Rwanda na machafuko ya kikabila yaliyokuwa yameota mizizi nchi nzima pamoja na kuiletea maendeleo badala yake aliendelez­a visasi dhihi ya Watusi.

Hii ilisababis­ha Rwanda kutengwa na majirani zake, hasa jirani yao muhimu zaidi wa Uganda ambayo ilikuwa na Watusi wengi wanaoishi nchini humo. Hii iliathiri hata maendeleo ya kiuchumi ya Rwanda.

Hivyo basi, kitendo cha Jererali Jevenal Habyariman­a kumuondoa madarakani Rais Kayibanda kilipokele­kwa kwa furaha na wananchi wengi na Habyariman­a alionekana kama shujaa. Mwandishi wa makala haya anapatikan­a kwa simu namba, +2556795555­26, +2557650260­57.

Juvenal Habyariman­a

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.