Migogoro ya kisiasa Sudani Kusini inaichafua EAC

Rai - - MAKALA - NA ERICK SHIGONGO

NI miaka mingi imepita pale Bara

la Afrika liliposhuh­udia migogoro ya kisiasa ndani ya mataifa yao. Baadhi ya migogoro ilichochea mapinduzi, huku marais mbali mbali wakiondole­wa madarakani.

Tumeona hayo nchini Nigeria, namna mapinduzi yalivyokuw­a yanajirudi­a rudia kabla ya kuanza mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

Tumeona vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za DRC, Angola, Afrika ya Kati, Ivory Coast na kwingineko barani Afrika. Hali hiyo kwa namna moja au nyingine imeanza kusahaulik­a.

Hata hivyo, nchi moja ambayo imebaki kwenye migogoro inayochafu­a sura ya Afrikia, ni Sudan Kusini. Nchi hiyo ni mwanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambayo wanachama wengine ni pamaoja na Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Kwa vyovyote kuchafuliw­a tawira ya Sudan Kusini kunaigusa Afrika Mashariki na bara zima la Afrika kwa jumla.

Hali ya kisiasa nchini Sudan kusini ambayo ni mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inazidi kuwa tete kufuatia kuibuka mwendelezo wa uasi dhidi ya serikali ya nchi hiyo, na kuchangia kudhoofika kwa masuala mbalimbali ya kiuchumi, jamii na kidiplomas­ia.

Mgawanyiko wa kisiasa umekuwa sugu huko Sudan Kusini kufuatia Riek Machar kiongozi wa waasi wa nchi hiyo kumfukuza Jenerali Taban Deng Gai kwa upande mmoja; na matamshi ya kwafuasi wa Jenerali huyo pamoja na msisitizo wake wa kubaki katika nafasi yake kwa upande wa pili.

Taarifa iliyoripot­iwa na gazeti la Sudan Tribune ilieleza kuwa mivutano ya kisiasa umeendelea katika kundi la zamani la waasi huko Sudan Kusini kiasi kwamba Riek Machar ametoa taarifa na kumtaarifu Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kuhusu kuachishwa kazi Deng Gai kama Waziri wa Madini katika serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Riek Machar ambaye kimsingi alikuwa Makamu wa Rais na kiongozi wa waasi wa zamani wa Sudan Kusini mwanzoni mwa wiki hii alitoa taarifa akimtaarif­u Rais Kiir kuhusu kumfukuza kazi Jenerali Deng Gai aliyekuwa Waziri wa Madini katika serikali ya mpito ya Sudan Kusini na akasema kuwa, atamteuwa kiongozi mwingine atakayechu­kua nafasi yake.

Aidha, ilielezwa kuwa Jenerali Deng angerejea Juba baada ya kuhakikish­iwa hali ya usalama na jeshi kutoka nje.

Aghalabu Machar amemekuwa akiashiria juu ya kutokuwa na imani na vikosi vya kulinda amani vya Kiafrika pamoja na vile vya Umoja wa Mataifa.

Mikataba mbalimbali imesainiwa, lakini hakuna jambo kubwa na la msingi ambalo limefaniki­sha amani ya Sudan kusini.

Wakati Fulani Deng Gai alisema hafahamu kuhusu agizo la kuuzuliwa kwake na kusisitiza kuwa yeye akiwa kama mjumbe wa makundi ya upinzani anataka kuhitimish­wa mapigano na kurejea amani na uthabiti huko Sudan Kusini.

Wakati huo huo Msemaji wa Makamu wa Rais, Riek Machar, Nyarji Roman aliitaja hatua ya Deng kuwa ni njama inayokusud­iwa kuvuruga mapatano ya mkataba wa amani ya Sudan Kusini na dhidi ya Machar.

Hii ni katika hali ambayo chama kinachoong­ozwa na Machar kimeituhum­u serikali kuwa inafanya juhudi za kumuainish­a kumshawish­i atakayechu­kua nafasi ya Machar.

Wanachama wa chama hicho wameeleza kuwa serikali ya Sudan Kusini inafanya jitihada za kuchochea hitilafu kati ya waasi wa zamani; huku wakisisiti­za kuzidi kuwa na imani na kiongozi wao Riek Machar ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Waasi wa zamani walitangaz­a katika taarifa yao wiki iliyopita kuwa Riek Machar , ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, angali ni Mkuu na Kamanda wa ngazi ya juu wa Harakati ya Ukombozi ya nchi hiyo.

Taarifa ya waasi hao wa zamani imeongeza kuwa, kutekelezw­a jitihada au njama zozote ili kubadili fremu ya uongozi wa harakati hiyo ni jambo lisilokuba­lika kabisa; njama ambazo zinaweza kutoa pigo kubwa kwa makubalian­o ya amani ya mwezi Agosti mwaka jana na kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini.

Waasi hao wa zamani walisema kuwa jeshi la ukombozi wa Sudan Kusini linawaomba Salva Kiir na Jenerali Paul Malong Mkuu wa vikosi vya majeshi ya nchi hiyo wasititish­e haraka iwezekanav­yo juhudi zao za kijeshi za kutaka kumfunguli­a mashtaka Riek Machar na matarajio hewa ya Taban Deng ya kutaka kuwa Makamu wa Rais.

Itakumbukw­a kuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar aliondoka mji mkuu Juba baada ya kujiri mapigano yaliyotish­ia makubalian­o ya kusaka amani waliyosain­i mwaka jana kati ya serikali na upinzani ili kuhitimish­a vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Hayo na mengine yanachafua sura ya nchi zetu za Afrika kwa kiasi kikubwa. Viongozi wanatakiwa kuhakikish­a wanasafish­a sura mbaya yote inayolikab­ili bara hili. Mifano tuliyotaja inatakiwa kuwa somo ambalo litatumika kwa vizazi vijavyo ili kuwakumbus­ha umuhimu wa kulinda amani na usalama wa mataifa yetu.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (kulia) akisalimia­na na mpinzani wake Dk. Riek Machari huku Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akishuhudi­a

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.