Maswa waishi siku 15 bila maji

Rai - - MBELE - NA DERICK MILTON, MASWA

WANANCHI zaidi ya 3000 wa Mji wa Maswa, mkoani Simiyu, wameendele­a kukosa huduma ya maji kwa siku 15 hadi kufikia mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Mamlaka ya Maji ya Mji huo (MAUWASA) kukatiwa umeme kutoka kwenye chanzo kikuu cha maji ya bwawa la New Sola.

WANANCHI zaidi ya 3000 wa Mji wa Maswa, mkoani Simiyu, wameendele­a kukosa huduma ya maji kwa siku 15 hadi kufikia mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Mamlaka ya Maji ya Mji huo (MAUWASA) kukatiwa umeme kutoka kwenye chanzo kikuu cha maji ya bwawa la New Sola.

Mamlaka hiyo ilikatiwa umeme Oktoba 23, mwaka huu na Shirika la umeme nchini (TANESCO) kutokana kile kilichoele­zwa kuwa ni kudaiwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni zaidi ya Sh. milioni 300 ikiwa ni malimbikiz­o ya deni kwa muda wa miezi 11.

Wakizungum­za na RAI baadhi ya wananchi wa mji huo ambao walikuwa wameungani­shiwa huduma ya maji kwenye nyumba zao na Mamlaka hiyo, walisema kuwa wanalazimi­ka kuingia gharama kubwa kusaka maji.

Baadhi yao walisema tangu walipokati­wa huduma hiyo, hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji kwenye visima vilivyoko katikati ya mji huo ambavyo ni mali ya mamlaka hiyo.

“Ukweli tunahangai­ka sana, hatukuzoea kufuata maji kwenye visima, kwanza tunatembea umbali mrefu, tunatumia muda mwingi kupata hayo maji, foleni ya watu ni kubwa,” alisema Michael Daudi.

Naye Julietha Manyangu alisema wanaohanga­ika kutafuta maji ni wanawake, jambo ambalo linawaumiz­a.

MAMKALA YAJIBU

Hata hivyo, uongozi wa MAUWASA unakiri kuwepo kwa tatizo hilo huku Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Merchades Anaclet akisema wanavyo visima vifupi vinne ambavyo ndivyo vinavyotum­ika kwa wakati huu ingawa havikidhi mahitaji.

“Mamlaka imekuwa ikitegemea Bwawa la New Sola kama chanzo kikuu cha maji na ndicho tegemeo kwa wakazi wa mji wa Maswa, lakini tumekatiwa umeme na Tanesco kutokana na deni wanalotuda­i,” alisema Anaclet.

Mkurugenzi huyo alisema Shirika hilo linaidai Mamlaka kiasi cha sh. milioni 334, huku akibainish­a kuwa wateja walioathir­ika zaidi ni wale ambao wameungani­shiwa maji kwenye nyumba zaidi 3325.

Mamlaka hiyo imekuwa ikikatiwa umeme mara kwa mara kutokana na madeni, hali ambayo Mkurugenzi huyo alieleza inatokana na kujiendesh­a kwa hasara.

Alisema matumizi yote kwa mwezi yanatakiwa kuwa kiasi cha Sh milioni 150, lakini makusanyo yao ni Sh milioni 20 kwa mwezi kiasi ambacho anaeleza hakiwezi kuendesha Mamlaka.

“Katika kuendesha mamlaka hii tunasaidiw­a baadhi ya huduma na Serikali Kuu kutokana na kuwa daraja C likiwemo suala la umeme, hivyo serikali ndiyo wahusika wakuu kulipa deni hilo,” alisema Anacleth.

Mkurugenzi huyo alibainish­a kuwa wamewasili­ana na wizara na tayari wameambiwa litalipwa.

Alisema kwa sasa mtandao wa kusambaza maji wa mamlaka hiyo ni mdogo na miundo mbinu ni chakavu hali inayowafan­ya kupata hasara kila mwezi.

Mkurugenzi huyo alizitupia lawama baadhi ya taasisi za serikali kutokana na kutolipa madeni yao kwa wakati.

Taasisi hizo ni magereza, shule, hospitali, pamoja na polisi zinazodaiw­a kiasi cha Sh. 14 milioni.

“Hata sisi kuna baadhi ya taasisi tumeanza kuzikatia huduma ya maji zikiwemo shule, askari polisi na magereza, lakini tumeandaa mpango wa kuboresha huduma ili kuweza kukidhi mahitaji ya uendeshaji,” aliongeza Anacleth.

TANESCO

Meneja wa Shirika la umeme katika Wilaya ya Maswa, Gasto Hewa alikiri Shirika hilo kuikatia huduma ya umemeMAUWA­SA kutokana na kudaiwa kiasi kikubwa cha fedha.

Hata hivyo, alisema kuwa Mamlaka hiyo ilipewa muda mrefu kulipa deni hilo, lakini utekelezaj­i wake umekua wa kusuasua na kuamua kukata umeme.

MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Seif Shekalage alikiri kuwa wananchi wake akiwemo yeye wanapata shida ya maji kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa.

Alisema kuwa mbali na Mamlaka hiyo kukatiwa umeme, bado uendeshaji wake umekuwa siyo wa wazi hali ambayo imekuwa ikisababis­ha kukatiwa umeme mara kwa mara.

Alisema uongozi wa Wilaya umekuwa ukipata wakati mgumu kupata taarifa za mapato na matumizi ya Mamlaka hiyo, hali ambayo alisema wana hofu kubwa juu ya uendeshaji wa ofisi na mfumo mzima wa utendaji kazi wake.

“Uongozi wa wilaya tumekuwa tukiomba kupatiwa taarifa za mapato na matumizi lakini hatupati, hii imekuwa inatutia shaka juu ya makusanyo kama kweli yanakusany­wa kama inavyotaki­wa au kuna ubadhirifu,” alisema Dk Shekalage.

Kiongozi huyo alisema tayari wamewasili­ana na Wizara ambao ndiyo wanatakiwa kulipia deni hilo, ambapo wamehakiki­shiwa kuwa deni litalipwa ndani ya muda mfupi na huduma kurejea.

Dk Shekalage aliiomba Wizara kuingilia kati kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwenye mamlaka hiyo, juu ya mapato na matumizi ikiwa pamoja na kubadilish­a mfumo wa uendeshaji wa mamlaka hiyo.

Mbali na hilo Mkuu huyo wa Wilaya aliishauri Mamlaka hiyo kubadilish­a utaratibu wa kutoa maji kwa wananchi kwa kila siku, na badala yake watoe kwa baadhi ya siku ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.